Rais mstaafu wa Korea Kusini aachiwa huru

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,379
8,123
Rais wa zamani wa Korea Kusini, Lee Myung-bak amepata msamaha wa Rais na kukatiza kifungo chake cha miaka 17 jela kwa ufisadi.

Rais wa Korea Kusini, Yoon Seok-yeol ametoa msamaha huo kwa Lee, leo Jumanne ya Desemba 27, 2022 kama sehemu ya msamaha wa watu wengi ambao ni kawaida katika nchi hiyo ya Asia Mashariki karibu na sikukuu za kitaifa.

Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la habari ‘Aljazeera’ wameeleza kwamba Waziri wa Sheria wa Korea Kusini, Han Dong-hoon aliwaambia waandishi wa habari kwamba Yoon ametoa msamaha kwa zaidi ya watu 1,300 ili kukuza umoja wa kitaifa kupitia maridhiano, kuvumiliana na kuzingatia.

Yoon mapema mwaka huu alielezea kutoridhishwa kwake na Lee kukaa gerezani kwa muda wote wa kifungo chake, ambacho kingemweka gerezani hadi miaka yake ya 90.

Watu wengine mashuhuri waliojumuishwa katika msamaha huo ni pamoja na Kim Kyoung-soo, gavana wa zamani wa mkoa, na Choi Kyoung-hwan, waziri wa zamani wa fedha.

Lee ambaye alihudumu kama Rais kati ya 2008 na 2013, alipatikana na hatia ya rushwa na ubadhirifu mwaka 2018.

Lee ambaye ni mtendaji mkuu wa zamani wa kampuni ya ‘Hyundai Engineering and Construction’ alikanusha mashtaka yanayomkabili, likiwemo la kupokea rushwa kutoka kwa kampuni kubwa ikiwemo Samsung na kutakatisha fedha katika moja ya kampuni zake.

Mahakama ya Juu ya Korea Kusini iliidhinisha kifungo cha miaka 17 kwa Lee Oktoba 2020, na kumrudisha gerezani baada ya mahakama ya chini kumwachilia kwa dhamana.

Juni 2021, Lee mwenye umri wa miaka 81, aliachiliwa kwa muda baada ya waendesha mashtaka kusema afya ya Rais huyo wa zamani ilikuwa mbaya.

Akiwa madarakani, Lee aliiongoza Korea Kusini kutoka katika msukosuko wa kifedha duniani huku uchumi ukiwa haujaathirika lakini alikabiliwa na mvutano mkubwa na Korea Kaskazini na kukosolewa kwa kuwakandamiza wakosoaji.

Tangu kuanzishwa kwa demokrasia nchini Korea Kusini mwaka wa 1987, marais wote wa zamani isipokuwa mmoja, wamepatikana na hatia ya uhalifu wa kizungu au kumuona mwanafamilia wa karibu akitiwa hatiani.

Desemba 2021, Rais wa zamani, Park Geun-hye alipata msamaha wa Rais kutoka kwa mrithi wake, Moon Jae-in baada ya kuhukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka 20 jela kwa makosa yakiwemo rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.

Agosti 2022, Yoon alitangaza awamu yake ya kwanza ya msamaha tangu aingie madarakani Mei 2022 kuadhimisha siku ya ukombozi wa nchi hiyo.

Orodha hiyo ilijumuisha baadhi ya wafanyabiashara mashuhuri wa Korea Kusini, akiwemo mwenyekiti wa Samsung, Lee Jae-yong na mwenyekiti wa zamani wa STX Group, Kang Duk-soo.

==================

Jailed former South Korean president Lee Myung-bak received a presidential pardon Tuesday, cutting short his 17-year sentence on corruption charges, the justice minister said.

Lee was on a list of more than 1,300 people who received special pardons "from the perspective of broad national unity through reconciliation, tolerance and consideration", Han Dong-hoon told reporters after a Cabinet meeting with President Yoon Suk-yeol.

The 81-year-old Lee, who in June was granted a temporary release from jail due to his age and deteriorating health, is serving 17 years for bribery and embezzlement.

It was effectively a life sentence as he was not due for release until 2036, when he would be 95.

The former Hyundai CEO-turned-president was charged with 16 criminal allegations in 2018 and sentenced in 2020.

He was found guilty of creating slush funds of tens of millions of dollars and accepting bribes from Samsung Electronics in return for a presidential pardon for its late chairman, Lee Kun-hee, who was jailed for tax evasion.

A self-made man who was appointed head of a major construction firm at age 35 before entering politics, Lee served as president from 2008 to 2013.

He steered the country through the global financial crisis and won its bid for the 2018 Winter Olympics but was criticized by opponents for undermining the nation's democratic standards and freedoms of speech.

The pardons, effective at midnight Wednesday, mark the second time Yoon has exercised his clemency power since taking office in May.

In August, Samsung Electronics executive chairman Lee Jae-yong was among the beneficiaries of Yoon's first pardons.

South Korean presidents have frequently ended up in prison after their time in power, usually once their political rivals have moved into the presidential Blue House.

Chun Doo-hwan and Roh Tae-woo, former army generals who served jail terms in the 1990s for corruption and treason after leaving office, received presidential pardons after serving about two years.

Ex-president Roh Moo-hyun killed himself in 2009 after being questioned over graft allegations involving his family.

Lee's conservative successor Park Geun-hye was pardoned last year while she was serving 20 years in jail for bribery and abuse of power after being ousted in 2017 over a corruption scandal that prompted massive street protests.​
 
Na ndio maana wameendelea maana hawacheki na kima,huku kwetu majizi ya chama cha mambuzi yanalindana yameshatengeneza kamfumo kao wanarithishana nchi tu mara baba rais mtoto waziri,mara baba alikuwa mpiga domo wa chama mtoto nae kapewa uwaziri na hana uwezo.MAENDELEO TUTAYAONA KWA WENZETU TU
 
Back
Top Bottom