'Rais' Miss Utalii ameiaibisha Tanzania!

Kamura

JF-Expert Member
Apr 26, 2011
506
52
Nimesikitishwa kusoma na kuona habari katika picha katika gazeti la Mwananchi la leo ukurasa wa saba (7) Rais wa Miss Utalii, Gidion Chipungahelo akipigana na mmoja wa Majaji wa Shindano hilo kwa kutaja mshindi tofauti.

Miss Utalii kama lilivyo shindano hilo ni moja ya njia za kutangaza utalii nchini na nje ya nchi sasa kama utalii unageuka kuwa masumbwi na sehemu ya kudhalilisha kuna haja ya kuendelea kuwapo?
 
Walipeana makonde niiliiona kwenye tv. Hawa watu wa ajabu sana jamani. Tanzania kuna kila aina ya aibu!!
 
hii ni aibu sana.. nafikiri wizara haina strategy nzuri.. kama lengo ni kutafuta watu wanaoweza kutangaza nchi yao vyema haya mashindano HAYANA TIJA!!!
 
hii ni aibu sana.. nafikiri wizara haina strategy nzuri.. kama lengo ni kutafuta watu wanaoweza kutangaza nchi yao vyema haya mashindano HAYANA TIJA!!!
Mimi naona mashindano yakifanywa kwa weledi tija itakuwepo, kiasi fulani huwa wanasaidia kutangaza utalii japo utalii wenyewe hauwasidii watanzania.
 
eti 'RAIS' ndo maana Nyerere alipiga marufuku watu kujiita m 'rais'.....

siku hizi kuna mpaka Rais wa FM ACADEMIA.....LOL
 
Hao wote wapuuzi flani. Wanatumia miili ya dada zetu kama vitega uchumi vyao.
 
Kumbe huwa wanakuwa tayari na jina la mshindi kabla ya shindano?
 
Kaka Chipunga umejidhalilisha kweli,uliyemwahidi Ushindi akutanganzwa na ulikuwa umeshamtumia Aibu kweli kwako.
 
Uchakachuaji na rushwa kila pahali. Pengine huyu muheshimiwa "Rais Chipunga" alihonga mamilioni (pengine ya kukopa) ili mtu wake apite. Sasa kaona hakupitishwa unatarajia afanye nini? Kwanza mmeona hili jina, Chipunga, limekalia la kiulajiulaji vile na njaa!
Aaaaah Tanzania, Tanzania, Tanzania! Tunaelekea wapi na mfumo huu?
 
Huyo ndiye Chips bwana... watu wakimsema kwua huyu jamaa ni bure inaonekana kama anaonewa hivi. sasa ameamua kujisema mwenyewe, tena kwa vitendo
 
Back
Top Bottom