Bowie
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 4,372
- 6,078
Kwa muda wa miaka mingi nimekuwa nikifatilia chaguzi mbali mbali za Marekani lakini kuna kitu kimoja ambacho nimekuja kukifahamu hawa jamaa pamoja wanatulazimisha sisi nchi za dunia ya tatu tuwe Demokrasia lakini wao hawana demokrasia, viongozi wengi wa Marekani huwa selected not elected mfumo wao wa kutumia Electornic voting machine ndio huwa unatumika kuiba kura, kwa mfano uchaguzi wa mwaka 2000 Al-Gore alimshinda George Bush lakini system haikumtaka Al-Gore ashinde ikibidii waiibe kura huko Florida. John F Kennedy alipochaguliwa mwaka 1960 haikuwa chaguo lao ikabidii Serikali hiyo hiyo ya Marekani kupitia shirika lake la ujasusi wakaamuua mwaka 1963, katika kampeni za mwaka 1968 baada ya kuona Robert Kennedy anaelekea kushinda urais wa urais nao walimuua pia. Katika kampeni za mwaka 1984 Gary Hart ambaye alikuwa anagombea urais kupitia chama cha Democtratic alifanyiwa hujuma za kumchafulia jina akajioondoa. Kwasasa Donald Trump naye haikuwa chaguo lao na kwa sababu anaweza kushinda urais wameanza kumwekea kila aina ya mikwara mpaka wanachama wenzanke wa chama cha Republican wamempa kisogo kwasababu sio chaguo la system. Nimesoma ripoti ya Wikileaks Rais Obama alikuwa ametayarishwa kuwa rais wa Marekani kabla hata ya uchaguzi ni ndio maana alipoingia ikulu ile kauli mbiu yake ya Change We Can Believe In haikutekelezwa.
Kwa kampeni hizi zinazoendelea Marekani picha kamili itapatikana.
Kwa kampeni hizi zinazoendelea Marekani picha kamili itapatikana.