Rais Marekani Anakuwa Selected Ama Elected ?

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,372
6,078
Kwa muda wa miaka mingi nimekuwa nikifatilia chaguzi mbali mbali za Marekani lakini kuna kitu kimoja ambacho nimekuja kukifahamu hawa jamaa pamoja wanatulazimisha sisi nchi za dunia ya tatu tuwe Demokrasia lakini wao hawana demokrasia, viongozi wengi wa Marekani huwa selected not elected mfumo wao wa kutumia Electornic voting machine ndio huwa unatumika kuiba kura, kwa mfano uchaguzi wa mwaka 2000 Al-Gore alimshinda George Bush lakini system haikumtaka Al-Gore ashinde ikibidii waiibe kura huko Florida. John F Kennedy alipochaguliwa mwaka 1960 haikuwa chaguo lao ikabidii Serikali hiyo hiyo ya Marekani kupitia shirika lake la ujasusi wakaamuua mwaka 1963, katika kampeni za mwaka 1968 baada ya kuona Robert Kennedy anaelekea kushinda urais wa urais nao walimuua pia. Katika kampeni za mwaka 1984 Gary Hart ambaye alikuwa anagombea urais kupitia chama cha Democtratic alifanyiwa hujuma za kumchafulia jina akajioondoa. Kwasasa Donald Trump naye haikuwa chaguo lao na kwa sababu anaweza kushinda urais wameanza kumwekea kila aina ya mikwara mpaka wanachama wenzanke wa chama cha Republican wamempa kisogo kwasababu sio chaguo la system. Nimesoma ripoti ya Wikileaks Rais Obama alikuwa ametayarishwa kuwa rais wa Marekani kabla hata ya uchaguzi ni ndio maana alipoingia ikulu ile kauli mbiu yake ya Change We Can Believe In haikutekelezwa.
Kwa kampeni hizi zinazoendelea Marekani picha kamili itapatikana.
 
amer.jpg
amer.jpg

Selected by Rothschild and Rockerfeller Family.
 
Marekani system ndio uandaa Rais lakini mshindwa uwa anajijua kuwa atashindwa .......

Mshindi pia ujijua kuwa atashinda......

Tofauti na Tanzania ambapo uwa tunawatisha wananchi kwa kutumia vyombo vya Dora na kulinda utawala uliopo usiondoke madarakani kwa garama yeyote....
 
Baada ya Marekani kuchafuka sana kwny Taswira ya Ulimwengu hasa Ulimwengu wa Kiislam na Africa kutokana na Siasa za Kibabe za George Walker Bush hasa vita vya Ugaidi kule Middle East Wamarekani wakawa wanasakwa kwa Mia Ovu popote walipo ikabidi Wazee wa Kazi wakakutana wakaibuka na Mtu wanaeweza kumtumia kuhadaa Waislam na Watu weusi wajione sehemu ya Marekani ndipo wakamleta Barack Hussein Obama kwny Siasa za Marekani kwa kuanza kugombea U seneta 2005!
Siasa za Obama ziliwezesha kuuawa Osama na kuangusha Tawala Kongwe za Kiarabu kwa Msaada Mkubwa wa Waarabu wenyewe. Chuki ya Marekani pia imepungua sana Ulimwenguni ukilinganisha na wakat wa Bush!
Sasa ni zamu ya Hillary Clinton japo dalili zinaonesha Vijana wengi wahafidhina wapo pamoja na Mzalendo mwenzao Donald Trump
 
Siyo kweli, kuna jumla ya 538 Electors kutoka majimbo yote ya Marekani! Mshindi anatakiwa apate 270+ ya hao Electors ili aweze kuwa mshindi wa urais!
Hujanielewa namaanisha ukitakuwa Rais wa Marekani unatakiwa kuwa sio chini ya kura ya 270 electors.
 
Marekani hakuna wizi wa kura hilo ni dhahiri. Tatizo ni kujiingiza kwa makampuni na lobby groups kwa pesa na kila kitu ili watu wanaowataka tu ndio wawe washindani kwenye sanduku la kura - kwa hiyo yeyote atakae shinda atalinda maslahi yao na walala hoi wanabaki walalahoi wanauwana mitaani kwa madawa ya kulevywa
 
Huyu anaelekea ktk kupona kutoka kwa wale wa4
Hivi huu utafiti ulifanywa na watu wa ngapi?
Kama hao watafiti nao walizidi wanne INA maana utafiti ulifanywa na machizi,Sasa mkuu unauamini vipi utafiti uliofanywa na machizi?
Achana nao huo utafiti.
Nalog off
 
Kwa hiyo Al Gore allibiwa kura mwaka 2000 lakini leo Trump akitoa tahadhari za wizi wa kura anaonekana majinuni, siyo?

Siasa kweli zimejaa unafiki.

Al gore alitangaza kurudisha Nyumbani wapiganaji kutoka Mapambanoni Kama angeshinda hili lilikuwa tangazo la kushindwa vita kitu ambacho Majenerali na Majasusi wasingekubali kitokee!
 
Hivi huu utafiti ulifanywa na watu wa ngapi?
Kama hao watafiti nao walizidi wanne INA maana utafiti ulifanywa na machizi,Sasa mkuu unauamini vipi utafiti uliofanywa na machizi?
Achana nao huo utafiti.
Nalog off
WHO
 
Demokrasia ni usanii tuu,kwanza raia wa marekani huwa wanachagua tu raisi lkn kuamua nani awe raisi sio uamuzi wao.ni kama hapa kwetu mambo ya NEC,nyie hata mumpende vp,ataenda kukatwa Dodoma
 
Back
Top Bottom