TL. Marandu
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 3,625
- 5,810
Nilikuwa kabla ya Uchaguzi mkuu 2015 Nikimpenda sana Magufuli, Kiasi Tangu 2012 Nilikuwa Nikimfuatilia. Nilimheshimu sana kama mchapa Kazi asiye na Mchezo.
Wakati wa Kampeni 2015 Niliendelea kumheshimu ila Nilitaka Lowassa ashinde kwa Kuwa Niliamini Ni lazima Tanzania iwe na real Political equilibrium baada ya Miaka zaidi ya hamsini ya Utawala wa chama Kimoja.
Baada ya Uchaguzi na Jinsi Computer za Ukawa zilivyoporwa na Matokeo ya Uchaguzi wa Zanzibar Kuhujumiwa, nilitiwa kichefu chefu kiasi nilianza kumdharau kwa kutumika katika Maswala ya aibu! Lakini Nilipoona anaenda Muhimbili nusu atokwe na Machozi kwa Wamama kulala Chini, Nikaanza kuwa na Matumaini Kwake! Alipomtuma Majaliwa Pale Bandarini akamwagiza IGP ang'oke na Akina Masamaki ndio Kabisa nikasema Asante Yesu.
1)Kisha akakutana na Wazee Dar es salaam, Makonda! Nilistuka sana sana.
2)Kisha akafungia Matangazo ya TBC ya Bunge kwa hila Nikastuka sana.
3)Sakata la Kuletwa Polisi wa FFU na Mbwa bungeni Kuwapiga Wabunge Likanisononosha sana!
4)Alipomchagua Mwkonda Kuwa Mkuu wa Mkoa Nikanawa Mikono Kama Pilato, Nikaanza kutilia Mashaka Judgement zake.
5)Akakataza Mahafali ya UKAWA wakati ya CCM yanafanyika kwa Nyimbo, Uniform na Bendera za Chama, Nikaanza sasa Kumdharau.
6) Akazuia amikutano ya Vyama isipokuwa Yeye tu. Nikamdharau sana!
7) Akatimua Watoto 7000 wa Masikini Kisa hawana Vyeti au sifa Huku akiwatukana.
8) Atawaagiza NHC watupe vitu vya Mbowe Nje huku akijitapa Nikaendelea kudharau sana!
9) Akasema Jecha apewe Tuzo
10) Akamsaidia Lipumba Kuvunja Ofisi za Cuf na Kuagiza apewe Ruzuku!
11) Akaagiza Lema akamatwe Kisa Lema aliona Maono kuwa Atakufa kama hatabafilika!
12) Sasa Anamtetea Makonda Mdanganyifu, na Aliyevamia Kijambazi Kituo cha Habari!
Sasa sio Tu Kuwa Magufuli simpendi, Bali Namwona kama ni hasara kwa Taifa ni Mnafiki, Au Makonda Kuna Mambo Machafu anamfanyia na Akimfukuza anaona siri zitatoka au Atakosa wa Kumwamini Kumtendea Mambo ya hila?
Magufuli alishawahi Kusema Atauza Majengo ya Wizara Zote za Dar ili Serikali Ihamie Dodoma na anataka Kufanya hivyo Kabla ya Awamu yake ya Miaka mitano haijaisha, Isije Kuwa Lengo ni Kujipatia Kihalifu Majengo ya Wizara za Serikali zilizopo Dar!
Hivi Kweli Mtu Mwaminifu Angekuwa Rais Leo Angeruhusu Makonda hata Amtazame Usoni? Swali langu ni Kuwa Ni nini hasa Kinachowafanya wananchi wawe na imani na Rais anayemlinda Jambazi? Na Mtu anayefanya Corruption na shake up ya Kujipatia Rushwa kwa anaowayuhumu. Huu kwangu ni Wazimu na Rais wa Namna hii hatufai. Nadhani hata kama Makonda akiua mtu hadharani Huyu Mhalifu Mwenzake atamtizama tu!
Wanaccm hasa Wabunge, Msidhani hapa wanaohatibiwa ni Wapinzani! Vyama Zaidi ya Kimoja Imara ni Faida ya Kila Mbunge, Chama chako Ki!ikuonea na Kukufanyia hujuma Kama Bingine vyote Bimekufa hata kama wewe ni Mzuri kama Dhahabu Utafanya nini, Utakimbilia wapi? Kukuwepo na vyama Imara hata kukutisha wataogopa maana wanajua utahama chama na Jimbo bado utalichukua. Kama hamna Akili CCM kubalini Upinzani uuwawe, Kila Mbunge Mwenye Msimamo CCM atakuwa chini ya Rehema za Maguguli.
Mimi nadhani Kutaka CCM ife ni Upofu na Kutaka Upinzani Ufe nchini ni ujinga. Hivyo Wabunge Wote Unganeni Mumdhibiti Magufuli, kabla hamtachelewa maana Nimeshamsoma kwa Mwaka na Zaidi sasa huyu Bwana ni Kiburi, Much know na Msitegemee atabadilika kitu Bila Kumbana asiwe na Uwezo wa Kufanya hila hila zake.