Rais Magufuli Yuko sawa Kweli? | Page 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Magufuli Yuko sawa Kweli?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TL. Marandu, Mar 21, 2017.

 1. TL. Marandu

  TL. Marandu JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2017
  Joined: Jul 12, 2015
  Messages: 3,428
  Likes Received: 5,124
  Trophy Points: 280


  Nilikuwa kabla ya Uchaguzi mkuu 2015 Nikimpenda sana Magufuli, Kiasi Tangu 2012 Nilikuwa Nikimfuatilia. Nilimheshimu sana kama mchapa Kazi asiye na Mchezo.
  Wakati wa Kampeni 2015 Niliendelea kumheshimu ila Nilitaka Lowassa ashinde kwa Kuwa Niliamini Ni lazima Tanzania iwe na real Political equilibrium baada ya Miaka zaidi ya hamsini ya Utawala wa chama Kimoja.

  Baada ya Uchaguzi na Jinsi Computer za Ukawa zilivyoporwa na Matokeo ya Uchaguzi wa Zanzibar Kuhujumiwa, nilitiwa kichefu chefu kiasi nilianza kumdharau kwa kutumika katika Maswala ya aibu! Lakini Nilipoona anaenda Muhimbili nusu atokwe na Machozi kwa Wamama kulala Chini, Nikaanza kuwa na Matumaini Kwake! Alipomtuma Majaliwa Pale Bandarini akamwagiza IGP ang'oke na Akina Masamaki ndio Kabisa nikasema Asante Yesu.

  1)Kisha akakutana na Wazee Dar es salaam, Makonda! Nilistuka sana sana.

  2)Kisha akafungia Matangazo ya TBC ya Bunge kwa hila Nikastuka sana.

  3)Sakata la Kuletwa Polisi wa FFU na Mbwa bungeni Kuwapiga Wabunge Likanisononosha sana!

  4)Alipomchagua Mwkonda Kuwa Mkuu wa Mkoa Nikanawa Mikono Kama Pilato, Nikaanza kutilia Mashaka Judgement zake.

  5)Akakataza Mahafali ya UKAWA wakati ya CCM yanafanyika kwa Nyimbo, Uniform na Bendera za Chama, Nikaanza sasa Kumdharau.

  6) Akazuia amikutano ya Vyama isipokuwa Yeye tu. Nikamdharau sana!

  7) Akatimua Watoto 7000 wa Masikini Kisa hawana Vyeti au sifa Huku akiwatukana.

  8) Atawaagiza NHC watupe vitu vya Mbowe Nje huku akijitapa Nikaendelea kudharau sana!

  9) Akasema Jecha apewe Tuzo

  10) Akamsaidia Lipumba Kuvunja Ofisi za Cuf na Kuagiza apewe Ruzuku!

  11) Akaagiza Lema akamatwe Kisa Lema aliona Maono kuwa Atakufa kama hatabafilika!

  12) Sasa Anamtetea Makonda Mdanganyifu, na Aliyevamia Kijambazi Kituo cha Habari!

  Sasa sio Tu Kuwa Magufuli simpendi, Bali Namwona kama ni hasara kwa Taifa ni Mnafiki, Au Makonda Kuna Mambo Machafu anamfanyia na Akimfukuza anaona siri zitatoka au Atakosa wa Kumwamini Kumtendea Mambo ya hila?

  Magufuli alishawahi Kusema Atauza Majengo ya Wizara Zote za Dar ili Serikali Ihamie Dodoma na anataka Kufanya hivyo Kabla ya Awamu yake ya Miaka mitano haijaisha, Isije Kuwa Lengo ni Kujipatia Kihalifu Majengo ya Wizara za Serikali zilizopo Dar!

  Hivi Kweli Mtu Mwaminifu Angekuwa Rais Leo Angeruhusu Makonda hata Amtazame Usoni? Swali langu ni Kuwa Ni nini hasa Kinachowafanya wananchi wawe na imani na Rais anayemlinda Jambazi? Na Mtu anayefanya Corruption na shake up ya Kujipatia Rushwa kwa anaowayuhumu. Huu kwangu ni Wazimu na Rais wa Namna hii hatufai. Nadhani hata kama Makonda akiua mtu hadharani Huyu Mhalifu Mwenzake atamtizama tu!

  Wanaccm hasa Wabunge, Msidhani hapa wanaohatibiwa ni Wapinzani! Vyama Zaidi ya Kimoja Imara ni Faida ya Kila Mbunge, Chama chako Ki!ikuonea na Kukufanyia hujuma Kama Bingine vyote Bimekufa hata kama wewe ni Mzuri kama Dhahabu Utafanya nini, Utakimbilia wapi? Kukuwepo na vyama Imara hata kukutisha wataogopa maana wanajua utahama chama na Jimbo bado utalichukua. Kama hamna Akili CCM kubalini Upinzani uuwawe, Kila Mbunge Mwenye Msimamo CCM atakuwa chini ya Rehema za Maguguli.

  Mimi nadhani Kutaka CCM ife ni Upofu na Kutaka Upinzani Ufe nchini ni ujinga. Hivyo Wabunge Wote Unganeni Mumdhibiti Magufuli, kabla hamtachelewa maana Nimeshamsoma kwa Mwaka na Zaidi sasa huyu Bwana ni Kiburi, Much know na Msitegemee atabadilika kitu Bila Kumbana asiwe na Uwezo wa Kufanya hila hila zake.
   
 2. minji

  minji JF-Expert Member

  #21
  Mar 21, 2017
  Joined: Sep 2, 2016
  Messages: 1,345
  Likes Received: 1,416
  Trophy Points: 280
  Yanayoendelea yanasikitisha sana
   
 3. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #22
  Mar 21, 2017
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 8,771
  Likes Received: 2,885
  Trophy Points: 280
  umesahau kuhusu alivopiga michango ya tetemeko kagera na baadae Sana alivyoenda akawaongelea maneno ya shombo na kuwakejeli
   
 4. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #23
  Mar 21, 2017
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,077
  Likes Received: 6,155
  Trophy Points: 280
  Hapana, hayuko sawa...yuko kama alivyo Bashite. Hilo nililisema akiwa Waziri wakati wa Mkapa, nikalirudia alipokuwa Waziri wa Kikwete na nikalisema tena alipoteuliwa kugombea Urais na vipofu wa CCM. Mimi hata sijashtuka wala kumshangaa kwa kauli zake wakati wa ufunguzi wa flyovers, kinachonishangaza ni kuwaona baadhi ya Watanzania eti wakishangaa. Huwezi kupanda maharage ukavuna karanga...wachagua hovyo wasilalamike hovyo wakitendewa hovyo. Huyo ndiye Magufuli...hayuko sawa, period.
   
 5. TL. Marandu

  TL. Marandu JF-Expert Member

  #24
  Mar 21, 2017
  Joined: Jul 12, 2015
  Messages: 3,428
  Likes Received: 5,124
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo Unadhani Tukimshika Jambazi Tunataka Tukumbuke Mema yake na Kumwachia,Kama ni Hivyo hata Amin , na Osama nao wangeachwa waendelee na Maisha yao Kwani na Wao walikuwa na Mazuri yao, Mfano Id Amin alipinga sana Makaburu wa SA na alitetea sana Harakati za Watu weusi Marekani. Hakuna asiye na Jema hata waliokuwa Wanawaua Malbino Walikuwa hawana mambo mema? Kwama mawazo yako ni sahihi basi hata Waumiani hao waachiwe. The hell Just Move on!
   
 6. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #25
  Mar 21, 2017
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,795
  Likes Received: 3,395
  Trophy Points: 280
  Hahaha!
   
 7. M

  Mama Obama JF-Expert Member

  #26
  Mar 21, 2017
  Joined: Mar 5, 2016
  Messages: 1,494
  Likes Received: 986
  Trophy Points: 280
  Kwa uwamuzi wake wa kumtetea Makonda Rais Magufuli hawezi kutetea haki alikuwa anatudanganya kama hawa wengine. Sina imani na Huyu Rais ati at Aleta mabadiliko, hawezi hata kidogo kwa uwamuxi wake wa jeuri kama Kuwa Rais ni kama tumemuuzia nchi. Kwa kuwa Tanzania ni yetu wote sitaacha kukutetea haki.
   
 8. TL. Marandu

  TL. Marandu JF-Expert Member

  #27
  Mar 21, 2017
  Joined: Jul 12, 2015
  Messages: 3,428
  Likes Received: 5,124
  Trophy Points: 280

  Hivi Mungu hawezi Kufanya hii Manuva kwenye Gulfstream, Akatwanga Kwenye Tank, Namkumbuka Rip J. Damian Komba Nyie! ..... " Ndugu Watanzania Leo yametimiaaaaa , Yalioandikwa na Mwenyezi Mungu.... Taifaaaa Lahuzunikaaa, Duniaaa yahuzunikaaa... Hebu na Mimi Niache kumba Nyimbo za Huzuni! ... Usishangae Mitaani Njemba zikaimba Bambambabam babam Eeeeee Kidedea!
   
 9. e

  eddy JF-Expert Member

  #28
  Mar 21, 2017
  Joined: Dec 26, 2007
  Messages: 9,123
  Likes Received: 3,560
  Trophy Points: 280
  kwahiyo ulitakaje? Tundulissu ndio hayuko sawa, hajui tofauti ya rais wa jmt na wa tls
   
 10. TL. Marandu

  TL. Marandu JF-Expert Member

  #29
  Mar 21, 2017
  Joined: Jul 12, 2015
  Messages: 3,428
  Likes Received: 5,124
  Trophy Points: 280
  Demokrasia, Uhuru wa Jamii na Utawala wa Kisheria Ndio Nguzo Kuu ya Haki, Maendeleo na Uwajibikaji. Nje ya hapo ni Moto wa Mabua! There is no substitute for freedom that is why people are willng to die defending freedom the Earlier this Fellow get it in his head the better!
   
 11. e

  eddy JF-Expert Member

  #30
  Mar 21, 2017
  Joined: Dec 26, 2007
  Messages: 9,123
  Likes Received: 3,560
  Trophy Points: 280
  mawazo ya kijinga
   
 12. e

  eddy JF-Expert Member

  #31
  Mar 21, 2017
  Joined: Dec 26, 2007
  Messages: 9,123
  Likes Received: 3,560
  Trophy Points: 280
  mbona hujaandika la mbowe kumkimbia mkemia mkuu?
   
 13. TL. Marandu

  TL. Marandu JF-Expert Member

  #32
  Mar 21, 2017
  Joined: Jul 12, 2015
  Messages: 3,428
  Likes Received: 5,124
  Trophy Points: 280
  "Mbona" sio Lugha ya Utetezi au Argumentation. Futa kabisa Neno hilo ni la Kijinga mno limebakishwa tu kwa mabishano ya Watoto wa chekechea!
   
 14. d

  demulikuy JF-Expert Member

  #33
  Mar 21, 2017
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 678
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 80
  Mkuu Marandu usisahau pia kuwa kwa matukio ya wiki chache zilizopita Tanzania iko iko kwenye "psychological crisis". Kwanza kulikuwa na issue ya uhakiki wa vyeti Tanzania nzima, hatma ya zoezi hili haieleweki na hatuelezwi kwa nini? Ikaja issue ya madawa ya kulevya, ikaanza kutiliwa mashaka sana pale watu kama TID na Wema Sepetu kuanza kukamatwa kwa mbwembwe, hatma ya "vita" hii nayo iko mashakani. Tatu imekuja issue ya uadilifu wa kutiliwa mashaka wa baadhi ya viongozi wetu wakuu. Sakata hili nalo bado halina majibu na kwa bahati mbaya sana limeachwa "lielee" kwenye vichwa vya watanzania na kila kukicha linazua maswali na sintofahamu nyingi? At least Mheshimiwa Nape Nauye ameonyesha ukomavu wa uongozi kwa kuunda tume kitu ambacho kingefanyika kwenye masuala hayo hapo juu angalau kuleta matumaini kwamba serikali inachukua hatua. Ombi langu kwa Viongozi wenye dhamana, leo utafiti umeonyesha Watanzania ni kati ya watu wasiokuwa na furaha ya maisha duniani (Ni kati ya nchi tatu za mwisho duniani ya kwanza ikiwa Norway), chonde chonde kaeni chini na mtafakari kwa kina hii hali hatarishi ya sintofahamu na muipatie ufumbuzi wa kudumu ili watanzania wajue kesho maisha mazuri zaidi yanakuja. Niwatakie kila la heri!
   
 15. e

  eddy JF-Expert Member

  #34
  Mar 21, 2017
  Joined: Dec 26, 2007
  Messages: 9,123
  Likes Received: 3,560
  Trophy Points: 280
  mkuu hilo ni jalamba la 2020, dar lazima pachimbike lengo ni kulirudisha jiji mikononi mwetu hapo na rais atakuwa dom, lazima mkome.
   
 16. e

  eddy JF-Expert Member

  #35
  Mar 21, 2017
  Joined: Dec 26, 2007
  Messages: 9,123
  Likes Received: 3,560
  Trophy Points: 280
  dua la popo usiku wa manane, kamuulize kwanini mange kafunga account ya kumchafua makonda kwanza.
   
 17. kluger

  kluger JF-Expert Member

  #36
  Mar 21, 2017
  Joined: Jun 16, 2016
  Messages: 1,118
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Namkumbuka sana Mwalimu nyerere, babu yetu hakika upuuzi huu ungekemewa kwa kila hali, wazee wa sasa hv hawana busara wala ubavu wa kusema chochote.
   
 18. aminiusiamini

  aminiusiamini JF-Expert Member

  #37
  Mar 21, 2017
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 3,353
  Likes Received: 1,231
  Trophy Points: 280
  i need some financial support wakuu,nitende.
   
 19. WilliK10

  WilliK10 JF-Expert Member

  #38
  Mar 21, 2017
  Joined: Jul 22, 2016
  Messages: 611
  Likes Received: 266
  Trophy Points: 80
  Hivyo ni vionjo tu..picha kamili lipo.
   
 20. jerrytz

  jerrytz JF-Expert Member

  #39
  Mar 21, 2017
  Joined: Oct 10, 2012
  Messages: 5,631
  Likes Received: 3,059
  Trophy Points: 280
  Here we are......
   
 21. kisu cha ngariba

  kisu cha ngariba JF-Expert Member

  #40
  Mar 21, 2017
  Joined: Jun 21, 2016
  Messages: 19,553
  Likes Received: 42,577
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
Loading...