Rais Magufuli Yuko sawa Kweli?

Rais Magufuli Yuko sawa Kweli?

Hoja yako imefika.Hata hivyo sikubaliani na wewe unapomuita Binadamu mwenzio Kunguni.
 
Screenshot_2017-03-20-23-09-55.png
 
Kasema kapewa namba binafsi ya simu ya Rais wa benki ya dunia, na kutoa ahadi kuwa atamsumbua sana kuhusu maendeleo.

Maswali: 1. hivi benki ya dunia hawana governance, na mambo yao kuamuliwa na team? Hivi misaada na mikopo ya benki ya dunia haiangalii democracy? Hivi wadau wakubwa wa benki ya dunia anawafahamu?
Hahahahahaha,
Alisema wapi hii tena jamani?
Tanzania imepatwa na uwendawazimu
 
Tumesha muacha adi amevuka mto mamba hawana speed nchi kavu🙂🙂🙂🙂🙂
 
Kumbe bado viroba wengine wamekatazwa wengine wanavipata na kuvinywa!
Kumbe bangi wengine wamekatazwa wengine wanazipata na kuvuta, sijui wanatoa afghanistan!
 
Jamani I wish watanzania wote tungekuwa km Wanasheria wasomi halafu huyu kaboka mchizi nahisi angejua wasomi wakoje
Lakini Tz vilaza na kina Bashite ni wengi kupita maelezo believe or not kuna watu wapo maofisini ni maofisa lakini kinachoendelea hata hajui.
Kuna maofisa wapo ofisini ni waoga mpaka unapata wasiwasi km hawa watu ni wasomi au?
Tungekuwa tunajielewa kwa wingi na umoja wetu hata polisi waje na mitutu huyo Bashite angeshang'oka.
 
Nilikuwa kabla ya Uchaguzi mkuu 2015 Nikimpenda sana Magufuli, Kiasi Tangu 2012 Nilikuwa Nikimfuatilia. Nilimheshimu sana kama mchapa Kazi asiye na Mchezo.
Wakati wa Kampeni 2015 Niliendelea kumheshimu ila Nilitaka Lowassa ashinde kwa Kuwa Niliamini Ni lazima Tanzania iwe na real Political equilibrium baada ya Miaka zaidi ya hamsini ya Utawala wa chama Kimoja.

Baada ya Uchaguzi na Jinsi Computer za Ukawa zilivyoporwa na Matokeo ya Uchaguzi wa Zanzibar Kuhujumiwa, nilitiwa kichefu chefu kiasi nilianza kumdharau kwa kutumika katika Maswala ya aibu! Lakini Nilipoona anaenda Muhimbili nusu atokwe na Machozi kwa Wamama kulala Chini, Nikaanza kuwa na Matumaini Kwake! Alipomtuma Majaliwa Pale Bandarini akamwagiza IGP ang'oke na Akina Masamaki ndio Kabisa nikasema Asante Yesu.

1)Kisha akakutana na Wazee Dar es salaam, Akamsifia Kunguni Makonda! Nilistuka sana sana.
2)Kisha akafungia Matangazo ya TBC ya Bunge kwa hila Nikastuka sana.
3)Sakata la Kuletwa Polisi wa FFU na Mbwa bungeni Kuwapiga Wabunge Likanisononosha sana!
4)Alipomchagua Mwkonda Kuwa Mkuu wa Mkoa Nikanawa Mikono Kama Pilato, Nikaanza kutilia Mashaka Judgement zake.
5)Akakataza Mahafali ya UKAWA wakati ya CCM yanafanyika kwa Nyimbo, Uniform na Bendera za Chama, Nikaanza sasa Kumdharau.
6) Akazuia amikutano ya Vyama isipokuwa Yeye tu. Nikamdharau sana!
7) Akatimua Watoto 7000 wa Masikini Kisa hawana Vyeti au sifa Huku akiwatukana.
8) Atawaagiza NHC watupe vitu vya Mbowe Nje huku akijitapa Nikaendelea kudharau sana!
9) Akasema Jecha apewe Tuzo
10) Akamsaidia Lipumba Kuvunja Ofisi za Cuf na Kuagiza apewe Ruzuku!
11) Akaagiza Lema akamatwe Kisa Lema aliona Maono kuwa Atakufa kama hatabafilika!
12) Sasa Anamtetea Makonda Mdanganyifu, na Aliyevamia Kijambazi Kituo cha Habari!

Sasa sio Tu Kuwa Maguguli namfharau, Bali Namwona kama ni hasara kwa Taifa ni Mnafiki kama Uozo, Au Makonda Kuna Mambo Machafu anamfanyia na Akimfukuza anaona siri zitatoka au Atakosa wa Kumwamini Kumtendea Mambo ya hila? Magufuli alishawahi Kusema Atauza Majengo ya Wizara Zote za Dar ili Serikali Ihamie Dodoma na anataka Kufanya hivyo Kabla ya Awamu yake ya Miaka mitano haijaisha, Isije Kuwa Lengo ni Kujipatia Kihalifu Majengo ya Wizara za Serikali zilizopo Dar!

Hivi Kweli Mtu Mwaminifu Angekuwa Rais Leo Angeruhusu Makonda hata Amtazame Usoni? Swali langu ni Kuwa Ni nini hasa Kinachowafanya wananchi wawe na imani na Rais anayemlinda Jambazi? Na Mtu anayefanya Corruption na shake up ya Kujipatia Rushwa kwa anaowayuhumu. Huu kwangu ni Wazimu na Rais wa Namna hii hatufai. Nadhani hata kama Makonda akiua mtu hadharani Huyu Mhalifu Mwenzake atamtizama tu!

Wanaccm hasa Wabunge, Msidhani hapa wanaohatibiwa ni Wapinzani! Vyama Zaidi ya Kimoja Imara ni Faida ya Kila Mbunge, Chama chako Ki!ikuonea na Kukufanyia hujuma Kama Bingine vyote Bimekufa hata kama wewe ni Mzuri kama Dhahabu Utafanya nini, Utakimbilia wapi? Kukuwepo na vyama Imara hata kukutisha wataogopa maana wanajua utahama chama na Jimbo bado utalichukua. Kama hamna Akili CCM kubalini Upinzani uuwawe, Kila Mbunge Mwenye Msimamo CCM atakuwa chini ya Rehema za Mahuguli. Mimi nadhani Kutaka CCM ife ni Upofu na Kutaka Upinzani Ufe nchini ni ujinga. Hivyo Wabunge Wote Unganeni Mumdhibiti Magufuli, kabla hamtachelewa maana Nimeshamsoma kwa Mwaka na Zaidi sasa huyu Bwana ni Kiburi, Much know na Msitegemee atabadilika kitu Bila Kumbana asiwe na Uwezo wa Kufanya hila hila zake.
Nilidhani maelezo yako yanasaidia lakini nimegundua ww ni kati ya wale wakaririshwaji, pia naamini hulijui bunge vizuri-hilo bunge ndo lilikuwa linatumia pesa za walipa kodi bila huruma-ila kwao ni rahisi kucheza na akili yako na kuwaamini-hata JPM aliwahi kuwa mbuge pia-ila naamini tumeishi muda mwingi kimajungu na ndio tabia ya baadhi yetu-so kwa awamu hii tunaona shida kubwa sana kwani majungu hayana nafasi tena, na ndo maana ajenda yetu kuu ilikuwa ni madawa ya kulevya, kinachoendelea ni kuvuruga ajenda husika, kwa utaratibu kama huu ni ngumu sana kuendelea.
 
Hizi Lawama Zote Ziwaendee Akina Mzee MKAPA na Wazee wote wa CCM bila Kuwasahau TISS kwa Kutuletea na Kutupitishia Huyu Mtu<SIZONJE> mwaka 2015.
 
Hata Farao alikua kiburi lkn Mungu alidili nae hatimae kifo na pia hata kwa huyu sisimizi Mungu atasema naye siamelewa madaraka bhana.
He required to remember there is no everlasting power/rule
 
Hata Farao alikua kiburi lkn Mungu alidili nae hatimae kifo na pia hata kwa huyu sisimizi Mungu atasema naye siamelewa madaraka bhana.
He required to remember there is no everlasting power/rule
Tuombe sana Mungu
 
mkuu wa mkoa ana uwezo wa hata kuja kwako usiku wa manane as long as ana watu wa usalama nyuma yake bila kuzuiliwa na mtu yeyote! acheni unyumbu nyie fanyeni kazi mlishe familia zenu maneno ya kwenye kanga hayawasaidii
 
Back
Top Bottom