Rais Magufuli yashamshinda?

Now yuko very desperate, he was supposed to have someone on top of him kum-control huyu jamaa, bahati mbaya hata makamu wake hamuwezi
 
Well said.

Mheshimiwa amekosea kwa treatment aliyompa Nape. Naamini nape ni one of the best loyalist kwenye chama cha CCM.

Lakini wanasiasa wajifunze, in politics gombaneni kwa hoja, ila huko nje maisha yaendelee kama kawaida.

Baada ya huu uongozi kupita, Makonda atapata tabu sana, aombe tu atakayekuja awe na huruma na asikumbuke.
 
Mkuu nakubaliana na wewe kwa asilimia mia moja, hapa ccm wametuwekea mnyampara sio kiongozi hata kidogo
 

Siku hizi narrative imebadilika kabisa.

Hatujadili tena mambo ya vipaumbele kama kuacha masafari ya Ulaya yasiyo na kichwa wala miguu na kuelekeza rasilimali kwenye matatizo sugu kama ukosefu wa madawati, vitanda mahospitalini, n.k.

Badala yake tunajadili mambo ya utawala wa mabavu, majungu, udaku, na upuuzi wa kila aina.

Ni kama vile tumeshapoteza kabisa lengo [lost focus].

Na yeye mwenyewe rais naye anahusika moja kwa moja katika ku shape narratives.
 
Duh!

Hivi kumbe nilishawahi kuandika kuhusu 'kushindwa' kwa rais Magufuli....?

Nilikuwa nimeshasahau.

Ahsanteni sana mods kwa kunikumbusha.
 
.Hata ndani ya chama chake ukiangalia vizuri utaona nyuso nyingi tu za manung'uniko toka kwa wakereketwa. Wengi wao siku hizi wanashindwa hata kumtetea. Wapo kimyaaaa utadhani wagonjwa. CCM hawana furaha kabisa.
Mbadiliko ya katiba ya CCM yanayolazimisha 'm/kiti' kugombea mhula wa pili bila kupingwa yanaeleza hoja yako
 
Now yuko very desperate, he was supposed to have someone on top of him kum-control huyu jamaa, bahati mbaya hata makamu wake hamuwezi

Namlaani huyo alompigia debe kuchukua form,huyu si wa ku control Bali wa kupelekwa milembe,na alaaniwe yeyote alompigia kura
 
Nyani Ngabu urais ni taasisi ukimuona rais anatoa maamuzi ujue information zote anazo
Hilo suala la rais ni taaisi ni kweli kabisa, lakini si wote wenye intelligence ya kutambua kuwa nafasi zao ni taasisi, ndiyo maana wanathubutu kujinasibu kuwa hawashauriwi na mtu kuhusu cha kufanya, kitu ambacho kinapingana na ninyi watetezi wake.
Information 'zote' unazodai kuwa anazo unapswa kutamua kuwa ana uwezo wa kuzipuuza kama alivyokwisha jinasibu halafu akaja na za kwake au madude ake anayoyaamini yeye kwa kadili aonavyo inafaa.
Katiba yetu inahitaji mtu mwenye busara tu. Otherwise hata SHILAWADU kwa rais wetu ni information zote.
 
Rais ni Magufuli na ataendelea kuwa magufuli. huko anakopita ni shangwe na vigelegele. wananchi wanatamani aseme neno roho zao zifrahi. huku mko busy kutunga ngonjera na hadithi zisizo na vichwa wala miguu......
Upigwe bani wewe kwani unadhani kila kitu ni ushabiki badala ya kungalia fact
Subiri Jingalao na MOTOCHINI waisome post yako utakoga matusi.

Huko kunatakiwa kusifu na kuabudu tu
 
Mzee sijakupata hapo...ulitaka kusema nini?
Hoja yako kwamba CCM haina raha, ina ukweli. Na upande mwingine umebaini huenda kukatokea 'kupingwa'
Katiba ikafanyiwa marekebisho kuzuia kupingwa na waliotaka kukataa wakawekwa 'mahali salama'

Hili nadhani lina ukweli usiopingika, hata ndani ya CCM hakuna raha
 
kweli kabisa
 
Kabla ya raisi kushindwa majukumu yake, naamini watanzania as a society tulishashindwa mda mrefu. Tumebaki na mipasho, majungu, fitina, udaku na uzombi.

Ukisoma archives za jf(posts za miaka mitano-nane iliyopita) utagundua kuwa hili ni taifal inaloenda kwa mihemko, kuanzia top officials hadi mtu wa chini. In no time issue ya Bashite na vyeti itakuwa historia(actually tangu tupate habari za yeye kuvamia Clouds Media tumesahau kuhusu vyeti).
 
Ukipita mitaani watu washachoka na story zake...
biashara haziendi.....mood iliyopo ni kusubiri labda mambo yatanyooka soon...
sasa sijui yasiponyooka itakuaje....
yaan kama hii ya kuonyeshana mguu wa kuku, huku zanzibar chochoro zote mji mkongwe ni nape na bastola
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…