mechard Rwizile
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 1,571
- 875
Nyani Ngabu urais ni taasisi ukimuona rais anatoa maamuzi ujue information zote anazo
Sio kweli Rich, juzi Rais Mkapa alikiri kuwa katika kipindi chake alikosea sana ubinafsishaji wa mashirika ya umma. Miaka kumi baadae. Nakumbuka katika kipindi chake aliwaona watu wajinga na wachochezi sana waliolipinga zoezi hili. Kama sio akina Jenerali Ulimwengu, Mzee Kaduma na baadhi ya watu wengine hata NMB isingekuwepo alitaka kuiuza bank yote ya NBC kwa bei ya pipi. Leo hii anajuta, anajilaumu, lakini hana atakachosaidia; viwanda vyetu viliuzwa na sasa hivi havifanyi kazi; afadhali kabla ya zoezi.
Makosa anayoyafanya Rais wetu siyo ya taasisi ni ya binafsi na ndio maana hatambui hata baadhi ya mambo yaliyokubaliwa na mtangulizi wake. Hukumbuki kahama alisema nini kwa wananchi walioahiwa kujegewa nyumba na Mhesh. Kikwete? Amekataa na amesema aliyewahaidi ameisha ondoka! Kama rais ni taasisi kwa nini asitekeleze ahadi za rais aliyemtangulia?
Urais ni taasisi kwa nchi nyingine sio Tanzania na watawala wetu.