Rais Magufuli yashamshinda?

Baba j hapendi mawazo kinzani yeye anajiona correct, ana create situation ambayo ikija kubuma itakua hatari. Na anaweza sema kweli ifungwe mana hulka ya wasiotaka kukosolewa huwa kuwanyamazisha opponents wao.
Sema wewe Diva wangu.

Maana wengine tushasema sana mpaka salio tumemaliza. Tukisema hata kwa kukopa tunaweza kuonekana "huyo Kiranga kawaida yake tu".
 
Ni kweli jingalao,hapo nakubaliana nawewe mkuu
 
Sema wewe Diva wangu.

Maana wengine tushasema sana mpaka salio tumemaliza. Tukisema hata kwa kukopa tunaweza kuonekana "huyo Kiranga kawaida yake tu".
Na watu wengi hawajamsoma hulka yake tu anko ni zaidi ya tumjuavyo ukitaka ukosane naye mwambie ukweli. Kazi tunayo Watanzania maana wengi watapotezwa.
 
Nyani Ngabu, mwaka 2005 niligombana si na marafiki tu bali hata ndugu nikipinga Kikwete kugombea Urais kwamba hana sifa wala uwezo wa kuongoza, nikaambiwa niache kumkashifu chaguo la mungu, tumaini lililokuwa likisubiriwa!

Miaka kumi baadaye, 2015, nikagombana tena na marafiki wale wale, ndugu wale wale nikionya yale yale kuwa Magufuli hana sifa, busara wala hekima ya kuongoza labda kuliko hata Kikwete, nikarushiwa maneno yale yale kama ya mwaka 2005!

Ajabu ni kwamba wale wale ambao mwanzoni walishinda mtandaoni wakimsifia Kikwete hivi sasa hawamsifii tena badala yake wanamsifia Magufuli kama mkombozi na kukosa kabisa uvumilivu kwetu tunaomkosoa kwa ukurupukaji wa hovyo.

Kikwete aliingia madarakani na kifurushi cha kashfa, lakini huyu mwenzetu kaingia madarakani na gunia zima la kashfa lakini washikaji wake hili hawalioni, badala yake wanawalaumu ambao hawajawahi hata kukamata madaraka ya nchi hii!

Naam, ndio Tanzania yetu hii, nchi inayodaiwa kuwa ya amani na utulivu huku polisi na vyombo vyote vya usalama vikiwa mkononi mwa dikteta uchwara ambaye hajawahi kuheshimu mipaka yake ya uongozi kikatiba, kisheria wala kikanuni!

Lakini baya kuliko yote ni kwamba wapo raia wa nchi hii, walio tayari kumsifia kwa vifijo na nderemo mfalme wao hata kama anatembea uchi, wakitumia ushawishi wa nguvu kujaribu kutuaminisha jinsi alivyovaa! Cry my beloved country!
 
Vumilieni tu.
Mlizoea vya kunyonga vya kuchinja hamviwezi.
Magufuli kabana njia zote hakuna sehemu ya kuiba,dili hakuna,hakuna kusafiri hovyo hovyo.
Vumilieni ingawa mnaumia ipo siku mtazoea kuishi bila kutegemea fedha za semina,warsha,makongamano,safari nk.
 
Hahahaaa mzee wa 'mfumo'...
Ndugu yangu wee acha tu! cart in front of the hose (track number ya Rosetta ninayo by the way).

Kuhamia Dodoma ni suala la kisera, ghafla watu wanahama halafu sheria ndiyo ipitishwe !!!

Taratibu watatuelewa
 

Hebu changia acha viroja ...
 
No sense ' in jpm voice'
 

..hili la kukurupuka kwa kweli JPM litamgharimu sana.....hii ya kufukuzafukuza tayari kuna watu wanarudishwa kwa siri makazini....yeye anakurupukia mambo alafu hayamalizi....huko mahospitali mfano vitanda kaenda muhimbili...lakini hajui huduma za afya ubora wake ukoje...ama huko kwenye mahospitali mikoani....na wilayani....

...ukija kwa watumishi wa umma (ambao wengi hawakumpa kura) ndio kabisaa.....watu wanaugulia maumivu maana watu vyeo hawapandi....wa kuhama hawaami....ajira mpya ndio hivyo zimesimama....hivi kwa utendaji huu watu watamsaidiaje kujenga nchi???...hivi anafikiri nchi itajengwa na wana ccm majukwaani???....alafu anapokataza wenzake wa upinzani anafikiriaje??...yeye hakupata asiimia 100% ya kura.....na kwa maana hiyo hao wenzake wa upinzani nao wana wanasiasa wao wanaotaka kuwasikia....yeye anapohangaika kuhutubia mikutano peke yake anategemea nini???...simwelewi kabisa huyu president...
...anapobana uhuru wa wengine kuji expresss anajenga bomu ambao siku likipasuka hali itakua mbaya sana...na damu inaweza kumwagika...maana atatuma watu wake kuumiza watu kama alivyotishia...na kupelekea majanga....jambo ambalo litamjengea taswira mbaya sana duniani...iko siku watu watatoka tu bila kujali....
 
tusiwe wajinga..hata yeye mwenyewe alisema kwa hali ilivyosasa ni bora kufanya maamuzi kama kunamakosa basi yatarehekebishwa kuliko kutofanya maamuzi yeyote kwa kuogopa
Mbona hajaitumbua IPTL kama kweli haogopi kufanya maamuzi, mbona hajaenda kukaba kwenye madini..huko...
 
nilijua mwisho 180 kumbe ni mpaka 360 ndo kwanza mr prezdent yupo 140 akifika 180 cjui itakuaje; kama haoni hii bara bara ni mbovu yeye speed tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…