MWananyati
Senior Member
- Feb 3, 2011
- 160
- 53
Uzi huu hauna lengo la kukashifu wala kuchochea,bali kutaka kujua tu orodha kamili ya kile alichokisema Mheshimiwa sana na mzalendo pekee kwa sasa katika Taifa hili.
Nanukuu sehemu ya hotuba yake ambayo ndio ilibeba dhima nzima ya hotuba yake leo Ikulu...."
"Hawa majaji ni waadilifu sana. Huwezi kumsikia jaji Chande anazungumza chochote au majaji wengine. Tofauti na wastaafu wa sehemu nyingine, wanawashwa washwa sana. Nawapongeza sana waheshimiwa majaji"
Najaribu kuwaza,kuwashwa huko anakokutaja mheshimiwa mtukufu sana ni kule kukosoa utawala wake ama muwasho wa wapi na kwa wakati gani?!
Benjamin Mkapa ambae haishi kuita Watanzania wajinga na wapumbavu ni sehemu ya wastaafu haowanaowashwa washwa?! Ama hahusiki kwa kuwa amekuwa akisifia utawala huu na kwa kuwa kama ni mhunzi basi alishiriki kuchonga kinyago cha sebuleni?!!
Dhana ya wanaowashwa washwa ni kwa wanaosifu utawala huu na raisi wake pia ama ni kwa wakosoaji tu?! Mfano raisi Mwinyi alisema anatamani Magufuli atawale milele,nae alikuwa anawashwa washwa?! Je ni kosa la jinai ama uhaini kuwashwa katika awamu hii?!!!
Watu wakisema raisi hashauriki na wala haambiliki na ukitoa maoni yako tarajiwa kushutumiwa ama kufunguliwa kesi kama za Lissu na ikibidi mitutu juu,ni kosa?!!!
Hotuba hizi za rasha rasha na jumla jumla,huandaliwa na muandishi wa hotuba wa raisi ama ni mahaba yake msemaji kadri imfaavyo?!! Kama ni maneno ya muandishi wa hotuba wa raisi,kwa nini nae asikamatwe na kufunguliwa kesi za uchochezi za kumchochea muongeaji mbele ya umma?! Kama hotuba hizi ni za msemaji mwenyewe,mwandishi wa hotuba wa raisi sio mtumishi hewa?!!
Hahahahahaaaaaa!
Labda tumuulize RZ1 atakuwa ameelewa