Rais Magufuli: Wanafunzi UDOM waliofeli wakatafute vyuo vya saizi yao

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968
Rais John Pombe Magufuli amesema idadi kubwa ya wanafunzi waliofukuzwa hivi karibuni katika Chuo kikuu cha Dodoma waliokua wakisoma kozi maalum hawakua na sifa stahiki za kudahiliwa kusoma kozi hiyo na kwamba wanaostahili watatafutiwa nafasi kupata elimu hiyo.

Amesema pia alikuwa anasubiria wanafunzi wengine wa UDOM kugoma na wote wangeondoka. Na ametaka watu kuacha siasa kwenye masuala ya msingi

Rais John Pombe Magufuli amesema idadi kubwa ya wanafunzi waliofukuzwa hivi karibuni katika Chuo kikuu cha Dodoma waliokua wakisoma kozi maalum hawakua na sifa stahiki za kudahiliwa kusoma kozi hiyo na kwamba wanaostahili watatafutiwa nafasi kupata elimu hiyo.

Mbona kwenye video uliyo weka hakuna hayo maneno? Lakini ni kweli amesema kuna baadhi yao walikuwa vilaza wamepata four na wengine hawana vigezo lakini kuna walio pata 1 na 2 wameambiwa watapangiwa pa kwenda!
 
Watanzania mu watu wa ajabu sana.Kwa hiyo mnataka work force yetu iendelee kuwa na vihiyo.No way.Tutafikaje kwenye nchi ya viwanda?Na wote waliojipenyeza haijalishi wako wapi, watang'olewa bila huruma!Haiwezekani vihiyo wachukue nafasi za watoto wa maskini eti kwa kuwa wana ndugu zao wenye uwezo.
Huyu ndio rais wa Tanzania! Heshima kufukuza watoto kama mbwa! Magu Magu uwe na akiba ya maneno!
 
Rais John Pombe Magufuli amesema idadi kubwa ya wanafunzi waliofukuzwa hivi karibuni katika Chuo kikuu cha Dodoma waliokua wakisoma kozi maalum hawakua na sifa stahiki za kudahiliwa kusoma kozi hiyo na kwamba wanaostahili watatafutiwa nafasi kupata elimu hiyo.

Umaarufu wa Magu umejengwa juu ya msingi wa kuwadhalilisha wengine. Ubinifu wa kutumia udaktari wake wa UDSM katika kuleta mawazo ya maendeleo endelevu ni zero. Ukimpeleka nchi ya watu ambao hakuna udhaifu atatunukiwa nishani ya ububu.
 
Jamaa kakurupuka tena kama kawaida yake. Hawa wamepewa msaada na Serikali wa kulipia gharama zao zote za masomo na kujikimu. Kwanini Serikali badala ya kukurupuka isingeangalia ni chuo kipi hawa wanastahili kuhamishiwa na wakafanya hivyo? Wakatafute chuo size yao nani atawalipia hawa hasa ukitilia maanani wanatoka kwenye familia maskini? Huyu jamaa hana sifa hata chembe ya kuiongoza Tanzania. Sera zake za kukurupuka zinaishia kwenye majanga tu.

Huyu ndio rais wa Tanzania! Heshima kufukuza watoto kama mbwa! Magu Magu uwe na akiba ya maneno!
 
Umaarufu wa Magu umejengwa juu ya msingi wa kuwadhalilisha wengine. Ubinifu wa kutumia udaktari wake wa udsm katika kuleta mawazo ya maendeleo endelevu ni zero. Ukimpeleka nchi ya watu ambao hakuna udhaifu atatunukiwa nishani ya ububu.
Magu siku zote ni msema kweli. Hanaga unafiki hata kidogo. Leo tumejua kuwa kumbe Mbowe ni kilaza na ndo maana anawasupport vilaza
 
Back
Top Bottom