Rais Magufuli: Waliopo mahabusu kwa kesi za uhujumu uchumi, kama wapo tayari kuomba msamaha na kurejesha pesa, kama Sheria inaruhusu nashauri waachiwe

hii ni uchaguzi mdogo tu wa serikali za mitaa.naimani uchaguzi mkuu utatolewa hadi msamaha wa kodi hapa nchini
 
Wanabodi, Tangu aingie madarakani hii ni moja ya hotuba zuri na za kupendeza sana sana

Leo Rais amegusa kauli ya tuishi kwa msamaha, Kwa wanaoamini Katika ukatoliki kuishi kwa msamaha ndio mafundisho makuu

Neno msamaha kwa Wakatoliki linabeba Maana kubwa na hutamkwa kwenye sala ya Baba yetu kila jumapili

Katika sherehe ya kuwaapisha makatibu tawala, makatibu wakuu na manaibu wao. Rais Magufuli amemshauri mwendesha mashtaka wa serikali kuwafikiria wale wote ambao wapo tayari kutubu na kukubali kulipa pesa zote walizokwapua serikalini yaani mafisadi

Hii ni dalili mpya kuelekea uchaguzi wa mwaka 2025,

Uamuzi wa Rais Magufuli Leo naunga mkono asilimia Mia moja, Kwa watu waliopo mahabusu kwa wizi au dhuluma kwa zaidi ya miaka kadhaa ni muda wa kutubu na kusamehewa

Lakini kwa jicho la tatu namuangalia mkwe wa lowasa kwa mbali akitoka mahabusu

Naunga mkono hoja kauli ya Rais asilimia Mia moja

Wanaoamini kwenye Imani ya kikatoliki msamaha ndio msingi wa kukiri kuwa kila mtu ni dhaifu na anahitaji toba

Hongera Rais Magufuli
Nadhani hizi ni kauli za mpito tu! ukimalizikia uchaguzi zitabadilika tu.
 
Mhe. Rais anasema hajamwagiza DPP wala hataki kuingilia Uhuru wa mahakama ila kwa ukweli kabisa na kwa kuzingatia taratibu za kimahakama mtu akikiri kosa kesi inakwisha na wala haiitaji Rais aseme, Wale wanaoamini walitenda wapo uraia tayari au wanatumikia vifungo na wale wanaoamini hawakutenda wanataka kesi zao zisikilizwe mapatikane na hatia au watoke bila hatia.

Kesi za uhujumu uchumi zinatumika kisiasa kukandamiza watu, hakuna dhamana lakini maelekezo yakitoka ikulu tayari watu wanatolewa. Hizi kesi miaka yote zinaelezwa ushahidi ujakamilika Leo wanakiri vipi kwamba wametenda kosa? Walifanya huu mchezo wale jamaa wa madini Mwanza na pia mdogo wake Rostam, wakafanyiwa hivi Vodacom baada ya wakurugenzi wake kukamatwa na Sasa mchezo umenoga imekuwa uhujumu uchumi ni kesi za majadiliano ukiri ununue Uhuru wako...hii si sawa kabisa.

Nataman Mhe. Rais angesimamia kuviagiza vyombo vya dola kukamata watu baada ya uchunguzi kukamilika na kesi zikifika mahakaman ndani ya muda mfupi zisikilizwe hapa tungetenda haki. Tukiendelea kuwaweka na kuwatoa watu ndani kwa sbabu za kisiasa hatutendi vyema.

Lowasa kasifia juzi si kwamba anapenda ila anatamani mkwe wake apate Uhuru baada ya kuona ndani ya miaka mitatu hakuna uhakika wa mkwewe kusikilizwa. Kila kukicha uhujumu uchumi ukiangalia Nani kahujumu uchumi na hasara gani kasababisha upati majibu.

Serikali inatumia muhimili wa mahakama vibaya na kuufanya ushuke thamani, 4 yrs uchunguzi haujakamilika na mahakimu wanahairisha kesi uchunguzi gani huo au unafanyika mwezini? DPP anatakiwa kuwajibishwa siyo kubembelezwa au kushauriwa kuziondoa kesi mahakamani.
👏
 
Napata shida kidogo. kama wakikiri na kutubu? kwani tayari wamepatikana na hatia ya uhujumu uchumi? kesi ,kuwa mahakamani haimaanishi mshtakiwa anakosa .labda walio patikana na hatia .lakini pia pengine walio shtakiwa watashindsa kesi na na kuachiwa huru hapo J P M hakulioona hilo? ushauri
1 waendesha mashtaka wawe na ushahidi wa kutosha ili mtu wampeleke mahakamani na wawe wa memaliza upelelezi ili kupunguza mlundikano wa mahabusu
2 pia mahakimu waajiriwe wengi ili kesi zikienda mahakamani zisikilizwe mapema na kutolewa uamuzi
3 Tatu kesi za kubambika kwa wanao kosoa serkari zisiwepo ili kupunguza mashauri yasiyo na maana mahakani hivyo mahabusu watapungua
 
Mimi siwezi kuunga mkono maana Kikwete aliwasamehe wale wa EPA baada ya kulipa ila nikaongoza mashambulizi kumlipua. Shida yangu kwa Magufuli ni kuwa anawasotesha huko mahabusu huku kukiwa hakuna nyuma wala mbele. Any way wiki hii majabali yote yanarudi uraiani.
Bora EPA walisamehewa bila kukaa ndani. Hawa wengine ni kama vile wametumikia vifungo vyao na kutoa pesa bila hukumu ya mahakama.
 
Kama mchungaji atoavyo na kuongoza sala ya Toba mzee baba jmp amewaomba wezi watubu ndani ya siku 7 na kurudisha walichoiba.

Akisisitiza kuwa hapendi kuingilia mahakama ameomba ikiwezekana ushauri wake upokelewe kwa mtu kurudisha na kujiapiza hatarudia.
Jamani tubuni mrejee Mungu anashauri pia watu watubu wakamrudie Mungu wao

=====


UPDATES:

“viongozi mlioapishwa hapa fuateni sheria katika utendaji wenu wa kazi, tumieni vyombo vyetu vya kisheria, nawatakieni kazi njema”- Prof. Ibrahim Juma- Jaji Mkuu

“Mabadiliko ni sehemu ya kazi, tunawaomba mkafanye kazi za watu, mkawasikilize, tumieni uzoefu mliopata maeneo mliyokuwa awali kutekeleza majukumu yenu-Makamu wa Rais Samia

“Nawapongeza sana mlioteuliwa na kuapishwa leo”-Rais Magufuli

“Tupo hapa kufanya kazi za watu, sisi ni watumishi wa watu”-Rais Magufuli

“Unapopewa madaraka lazima uyabebe na uwajibike kwa kila litakalotokea, nchi hii tumekabidhiwa wote kwa ajili ya kuwatumikia watanzania”-Rais Magufuli

“Wapo watu wamekaa mahabusu kwa kesi za uhujumu uchumi,inawezekana wapo tayari kuomba msamaha,nakurejesha pesa, DPP katika kipindi cha siku 7 ningeshauri kama sheria inaruhusu wakatoke humo ndani,haya nimapendekezo sijaingilia mahakama” rais Magufuli


“Viongozi wa dini endeleeni kutuombea, msichoke, nchi hii inakwenda mbele, changamoto lazima ziwepo”-Rais Magufuli

“Nawapongeza sana watanzania kwa kulipa kodi, ndio mnasababisha tunatekeleza miradi mikubwa ya kimaendeleo”-Rais Magufuli
Ruge lodn
Patel ldn
Ruge gg &ov6.5
Patel UND 3.5
Maxb
 
YYLE MAMA WA PEMBE ZA NDOVU TUSHAANZA BARABARA ZA SINZA NAHISI ANAPUMUA AKIWA CHINA NOW

KWANN WENGINR WASIACHIWE KAZI Nzuri
 
kilichosemwa leo kipya ni kipi???

mdogo wa Rostam alitokaje?

wahindi wa madhahabu Shinyanga walitokaje?

tajiri wa mabasi ya Muro (Kimaro) alitokaje?

wahujumu uchumi na ma criminal wa kila aina miaka ya karibuni wamekuwa wakiachiwa kwa kutemeshwa walichoiba au kwa kupewa alternative sentence ya faini badala ya kifungo

watu ambao hawafuatilii national affairs ama wana upeo mdogo wa uchambuzi ama kumbukumbu finyu ndio wamechukulia hili tamko la leo kama ni breaking news

DPP has been under the thralls of the State House since the day he was tapped, tumeshalisemea sana hili.
 
Wanabodi, Tangu aingie madarakani hii ni moja ya hotuba zuri na za kupendeza sana sana

Leo Rais amegusa kauli ya tuishi kwa msamaha, Kwa wanaoamini Katika ukatoliki kuishi kwa msamaha ndio mafundisho makuu

Neno msamaha kwa Wakatoliki linabeba Maana kubwa na hutamkwa kwenye sala ya Baba yetu kila jumapili

Katika sherehe ya kuwaapisha makatibu tawala, makatibu wakuu na manaibu wao. Rais Magufuli amemshauri mwendesha mashtaka wa serikali kuwafikiria wale wote ambao wapo tayari kutubu na kukubali kulipa pesa zote walizokwapua serikalini yaani mafisadi

Hii ni dalili mpya kuelekea uchaguzi wa mwaka 2025,

Uamuzi wa Rais Magufuli Leo naunga mkono asilimia Mia moja, Kwa watu waliopo mahabusu kwa wizi au dhuluma kwa zaidi ya miaka kadhaa ni muda wa kutubu na kusamehewa

Lakini kwa jicho la tatu namuangalia mkwe wa lowasa kwa mbali akitoka mahabusu

Naunga mkono hoja kauli ya Rais asilimia Mia moja

Wanaoamini kwenye Imani ya kikatoliki msamaha ndio msingi wa kukiri kuwa kila mtu ni dhaifu na anahitaji toba

Hongera Rais Magufuli
Je wataruhusiwa
A. Kurejesha kidogo kidogo?
B. Kurudishwa kazini?
 
Pesa walipora kwenye,maduka ya kubadili fedha zimeisha sasa wamerudi na ujinga huu . mpaka January hawatakuwa na pesa za kulipa mshahara
 
Kwa upande wangu hili ni jambo jema, heko kwa Mh Rais, walio kuwa wakihujumu kama akina Rugemalira na akina Malinzi walikuwa wanasaidia sana kumwaga pesa huku chini, jambo hili liliwawezesha sana vijana wa huku chini kujiongezea kipato, bora waje uraiani waendeleze mishe zao na wengine wanufaike kama ilivyokuwa awali. Bado kuna wezi na wahujumu uchumi wengi na hawaguswi wanaguswa wale dagaa dagaa tu, mi papa ipo mtaani inadunda
 
Pengine ushindi ni mkubwa kwa hawa watu, pengine ushaidi usingepatikana mahakamani, pengine walionewa na kubambikiwa kesi. Haya yote tuyasahau lakini tuukumbatie msamaha wa kweli hii ndiyo hoja ya msingi. Lakini angalizo wange fast track kesi husika pengine wengi wao wangeshakutwa na hatia au bila hatia.
 
Back
Top Bottom