Rais Magufuli: Waliopo mahabusu kwa kesi za uhujumu uchumi, kama wapo tayari kuomba msamaha na kurejesha pesa, kama Sheria inaruhusu nashauri waachiwe

Omulasil

JF-Expert Member
May 5, 2015
7,424
9,358
Kama mchungaji atoavyo na kuongoza sala ya Toba mzee baba jmp amewaomba wezi watubu ndani ya siku 7 na kurudisha walichoiba.

Akisisitiza kuwa hapendi kuingilia mahakama ameomba ikiwezekana ushauri wake upokelewe kwa mtu kurudisha na kujiapiza hatarudia.
Jamani tubuni mrejee Mungu anashauri pia watu watubu wakamrudie Mungu wao

=====

UPDATES:

“viongozi mlioapishwa hapa fuateni sheria katika utendaji wenu wa kazi, tumieni vyombo vyetu vya kisheria, nawatakieni kazi njema”- Prof. Ibrahim Juma- Jaji Mkuu

“Mabadiliko ni sehemu ya kazi, tunawaomba mkafanye kazi za watu, mkawasikilize, tumieni uzoefu mliopata maeneo mliyokuwa awali kutekeleza majukumu yenu-Makamu wa Rais Samia

“Nawapongeza sana mlioteuliwa na kuapishwa leo”-Rais Magufuli

“Tupo hapa kufanya kazi za watu, sisi ni watumishi wa watu”-Rais Magufuli

“Unapopewa madaraka lazima uyabebe na uwajibike kwa kila litakalotokea, nchi hii tumekabidhiwa wote kwa ajili ya kuwatumikia watanzania”-Rais Magufuli

“Wapo watu wamekaa mahabusu kwa kesi za uhujumu uchumi,inawezekana wapo tayari kuomba msamaha,nakurejesha pesa, DPP katika kipindi cha siku 7 ningeshauri kama sheria inaruhusu wakatoke humo ndani,haya nimapendekezo sijaingilia mahakama” rais Magufuli

“Viongozi wa dini endeleeni kutuombea, msichoke, nchi hii inakwenda mbele, changamoto lazima ziwepo”-Rais Magufuli

“Nawapongeza sana watanzania kwa kulipa kodi, ndio mnasababisha tunatekeleza miradi mikubwa ya kimaendeleo”-Rais Magufuli

Zaidi soma....

027a34d1d03c62b1b71264dc5404a82a

RAIS John Magufuli ameshauri wafungwa walioko mahabusu kwa tuhuma za uhujumu uchumi, kama wako tayari kuomba radhi na kuzirudisha fedha walizotafuna, watolewe.
Miongoni mwa wafungwa waliopo mahabusu kwa tuhuma hizo ni pamoja na wafanyabiashara wakubwa nchini Harbinder Seth na James Rugemalira.
Sethi na Rugemarila wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi ikiwemo kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu, kughushi, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kutakatisha fedha na kusababisha hasara ya Dola za Marekani 22 milioni.

Watuhumiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo mwaka 2013 ambapo walikamatwa na kupandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza mwaka 2017.

Rais Magufuli ameshauri hayo leo tarehe 22 Septemba 2019, wakati anawaapisha viongozi mbalimbali aliowateuwa hivi karibuni, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Magufuli amemshauri Biswalo Mganga, Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DPP) kama sheria inaruhusu, awasikilize watuhumiwa watakaokuwa tayari kuomba msamaha na kuzirejesha fedha hizo.

“Wapo watu wamekaa mahabusu kwa kesi za uhujumu uchumi,inawezekana wapo tayari kuomba msamaha na kurejesha pesa, DPP katika kipindi cha siku saba ningeshauri kama sheria inaruhusu wakatoke humo ndani, haya nimapendekezo sijaingilia mahakama,” amesema Rais Magufuli
 
Kama mchungaji atoavyo na kuongoza sala ya Toba mzee baba jmp amewaomba wezi watubu ndani ya siku 7 na kurudisha walichoiba.

Akisisitiza kuwa hapendi kuingilia mahakama ameomba ikiwezekana ushauri wake upokelewe kwa mtu kurudisha na kujiapiza hatarudia.
Jamani tubuni mrejee Mungu anashauri pia watu watubu wakamrudie Mungu wao
Aanze yeye!
 
Wanabodi, Tangu aingie madarakani hii ni moja ya hotuba zuri na za kupendeza sana sana

Leo Rais amegusa kauli ya tuishi kwa msamaha, Kwa wanaoamini Katika ukatoliki kuishi kwa msamaha ndio mafundisho makuu

Neno msamaha kwa Wakatoliki linabeba Maana kubwa na hutamkwa kwenye sala ya Baba yetu kila jumapili

Katika sherehe ya kuwaapisha makatibu tawala, makatibu wakuu na manaibu wao. Rais Magufuli amemshauri mwendesha mashtaka wa serikali kuwafikiria wale wote ambao wapo tayari kutubu na kukubali kulipa pesa zote walizokwapua serikalini yaani mafisadi

Hii ni dalili mpya kuelekea uchaguzi wa mwaka 2025,

Uamuzi wa Rais Magufuli Leo naunga mkono asilimia Mia moja, Kwa watu waliopo mahabusu kwa wizi au dhuluma kwa zaidi ya miaka kadhaa ni muda wa kutubu na kusamehewa

Lakini kwa jicho la tatu namuangalia mkwe wa lowasa kwa mbali akitoka mahabusu

Naunga mkono hoja kauli ya Rais asilimia Mia moja

Wanaoamini kwenye Imani ya kikatoliki msamaha ndio msingi wa kukiri kuwa kila mtu ni dhaifu na anahitaji toba

Hongera Rais Magufuli
 
Ben Saa Nane yuko wapi atarudishwa?
 
Mimi siwezi kuunga mkono maana Kikwete aliwasamehe wale wa EPA baada ya kulipa ila nikaongoza mashambulizi kumlipua. Shida yangu kwa Magufuli ni kuwa anawasotesha huko mahabusu huku kukiwa hakuna nyuma wala mbele. Any way wiki hii majabali yote yanarudi uraiani.
 
Kwa hutuba ya Leo nahakika kuna viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam wamekalia kuti kavu hii ilikuwa Last warning kwani likijirudia lingine kama la COCO BEACH na La Vingunguti mtakuja kuniambia katika huu Uzi.
 
Mhe. Rais anasema hajamwagiza DPP wala hataki kuingilia Uhuru wa mahakama ila kwa ukweli kabisa na kwa kuzingatia taratibu za kimahakama mtu akikiri kosa kesi inakwisha na wala haiitaji Rais aseme, Wale wanaoamini walitenda wapo uraia tayari au wanatumikia vifungo na wale wanaoamini hawakutenda wanataka kesi zao zisikilizwe mapatikane na hatia au watoke bila hatia.

Kesi za uhujumu uchumi zinatumika kisiasa kukandamiza watu, hakuna dhamana lakini maelekezo yakitoka ikulu tayari watu wanatolewa. Hizi kesi miaka yote zinaelezwa ushahidi ujakamilika Leo wanakiri vipi kwamba wametenda kosa? Walifanya huu mchezo wale jamaa wa madini Mwanza na pia mdogo wake Rostam, wakafanyiwa hivi Vodacom baada ya wakurugenzi wake kukamatwa na Sasa mchezo umenoga imekuwa uhujumu uchumi ni kesi za majadiliano ukiri ununue Uhuru wako...hii si sawa kabisa.

Nataman Mhe. Rais angesimamia kuviagiza vyombo vya dola kukamata watu baada ya uchunguzi kukamilika na kesi zikifika mahakaman ndani ya muda mfupi zisikilizwe hapa tungetenda haki. Tukiendelea kuwaweka na kuwatoa watu ndani kwa sbabu za kisiasa hatutendi vyema.

Lowasa kasifia juzi si kwamba anapenda ila anatamani mkwe wake apate Uhuru baada ya kuona ndani ya miaka mitatu hakuna uhakika wa mkwewe kusikilizwa. Kila kukicha uhujumu uchumi ukiangalia Nani kahujumu uchumi na hasara gani kasababisha upati majibu.

Serikali inatumia muhimili wa mahakama vibaya na kuufanya ushuke thamani, 4 yrs uchunguzi haujakamilika na mahakimu wanahairisha kesi uchunguzi gani huo au unafanyika mwezini? DPP anatakiwa kuwajibishwa siyo kubembelezwa au kushauriwa kuziondoa kesi mahakamani.
 
Wanabodi, Tangu aingie madarakani hii ni moja ya hotuba zuri na za kupendeza sana sana

Leo Rais amegusa kauli ya tuishi kwa msamaha, Kwa wanaoamini Katika ukatoliki kuishi kwa msamaha ndio mafundisho makuu

Neno msamaha kwa Wakatoliki linabeba Maana kubwa na hutamkwa kwenye sala ya Baba yetu kila jumapili

Katika sherehe ya kuwaapisha makatibu tawala, makatibu wakuu na manaibu wao. Rais Magufuli amemshauri mwendesha mashtaka wa serikali kuwafikiria wale wote ambao wapo tayari kutubu na kukubali kulipa pesa zote walizokwapua serikalini yaani mafisadi

Hii ni dalili mpya kuelekea uchaguzi wa mwaka 2025,

Uamuzi wa Rais Magufuli Leo naunga mkono asilimia Mia moja, Kwa watu waliopo mahabusu kwa wizi au dhuluma kwa zaidi ya miaka kadhaa ni muda wa kutubu na kusamehewa

Lakini kwa jicho la tatu namuangalia mkwe wa lowasa kwa mbali akitoka mahabusu

Naunga mkono hoja kauli ya Rais asilimia Mia moja

Wanaoamini kwenye Imani ya kikatoliki msamaha ndio msingi wa kukiri kuwa kila mtu ni dhaifu na anahitaji toba

Hongera Rais Magufuli

Tunawasamehe wengine na kutaka watubu, je na sisi hatuna tuliowakosea tuwaombe msamaha na tutubu!?
 
Hakuna Msamaha kama huo Kwenye Kanisa Katoliki.
Na wala usijaribu kuchezea Imani za watu Kwa kuzilinganisha na Politics
 
Mkuu hapa duniani msamaha ndio kila kitu

Wewe ulitaka asisamehe

Tukiacha ushabiki Leo Rais ameongea point kubwa sana

Back
Top Bottom