Rais Magufuli unatufanya CCM tuonekane kama wafuata mkumbo

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,053
114,519
Mwenyekiti watu Ndugu John Pombe ametufanya CCM tuonekane kama watu wasijitambua.

Pale serikali au rais anapotoa tamko sisi CCM tunajikuta kutokana na mahaba ya chama chetu tunaliunga mkono. Hili ni suala la kawaida hata kama kimoyomoyo huungi mkono lakini mitandaoni na kwenye media na vilingeni huna budi kutoa povu kuunga mkono tamko na maagizo kutoka juu.

Hivyo ndivyo wamekuwa akifanya hata karibu wa uenezi Comrade Polepole Hamphrey. Tunaunga mkono matamko ili kumtia moyo rais watu. Hivyo kwenye mitandao inakuwa vurugu "Safi sana rais watu,hapa kazi tu,tumbua baba tumbua......"

Lakini kesho yake linapokuja kanusho au kutengeua kauli ya jana inabidi tena tuiunge mkono kibandidu bila kujali kama ili ya jana ambayo kimsingi inakinzana na ya leo tuliiunga mkono.......Mh.Rais unatudhalilisha sana,tunachekwa

Mfano mzuri ni ifuatayo:-
1. Suala la Msanii Ney wa Mitego
Mwanachama wako tulilipuka kukuunga mkono tuliposikia nyimbo ile imekatazwa. Tumekesha kwenye mitandao tukibushana. Jana umeruhusu wimbo upigwe,tunalazimika tena kuunga mkono tamko lako,sasa hapa ndio tunapoonekana makondoo

2. Suala la Vyeti vya kuzaliwa kwa wanandoa
Tamko lilipotolewa na Dr.Mwakyembe hatukuwa na budi kuliunga mkono,maana tuliamini unasema wewe kupitia waziri. Kesho umetengua kauli hivi tuliounga mkono tunaficha wapi sura zetu?

Kifupi mkuu rais tutakunyamazia. Watu tunalazimika kuwa na ID mbilimbili kwenye mitandao,ya kuunga mkono kauli ya jana na ile ya kuunga mkono tamko la kukanusha lile la jana

Muonee huruma mwenezi Humphrey Polepole anavyodhalilishwa kwenye TV kutetea matamko yanayokinzana........Haiwezekani leo unasema 1+2=3, kesho unasema hapana 1+2=12 halafu unataka majibu yote tuyaunge mkono
 
Ndo ujue madhara ya kuwa bendera fata upepo na kuwa na akili za kushikiwa.

Unatakiwa utathimini mambo sio kusifiasifia tu. Sasa leo mwenyekiti wako akisema "tangu leo ni kutembea uchi"basi ungekuja hapa kama mwendawazimu na vibwagizo vya " safi sana JPM, nguo zenyewe za kikoloni...bongo yenyewe joto tu...hapa kazi tu" .

Ni vema umeanza kujitambua. Jirekebishe.
 
1. Mnatakiwa msikurupuke
2. Mkubaliane pamoja cha kufanya kabla hamjaja kwenye public coz nimegundua mnapenda attention ya Media sana
3. Muache double standard, iweje kosa hilohilo lakini A anaadhibiwa alafu B anaachwa
 
Kama kichwa cha habar kinavojieleza hapo juu, watz ni watu wa kubadilika kila ck kuendana na, maslah yake
Juz kat alikamatwa msanii ney wa mitego wakaongea sana, asa iv kaachiwa hur wamigeuka kama bendera ifuatayo upepo wamianza kusema kuna mtego cio bure jaman

Nawasilisha
 
Wewe ni lini umekuwa mwanachama wa ccm? Acha kujitekenya na kucheka!!!!
Jamaa katoa kauli wakilishi....
Ina kiima...
Ina kiarifu...

Ahahahahahahaaa

Kwani wewe una ID ngapi? maana kwa hali halisi kutumia ID moja kutetea kauli kinzani lazima uonekane hamnaxo
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Serikali: Tumemshikilia Ney wa Mitego kwa sababu ya wimbo wake wenye maneno ya Kichochezi.

Vijana wa Lumumba: Safi sana!! Huu Utawala wa Magu, hakuna kucheka na mtu.

Serikali: Ney wa mitego aachiwe kwasababu wimbo wake hauna tatzo na auboreshe zaidi na upigwe radio na Tv zote.

Vijana wa Lumumba: Safi sana!! Rais wa wanyonge, anajali sana wananchi wake

.
 
Hata hivyo ni mataahira kweli
Sema tu anawazidishia level ya utaahira zaidi

1. Mnatakiwa msikurupuke
2. Mkubaliane pamoja cha kufanya kabla hamjaja kwenye public coz nimegundua mnapenda attention ya Media sana
3. Muache double standard, iweje kosa hilohilo lakini A anaadhibiwa alafu B anaachwa
Halafu wr Lin, unajuwa hiyo namba tatu, A ba B zote zipo kwenye BASHITE.. ungeenda tu straight to the point
 
Back
Top Bottom