WanaCCM ni Wanamapinduzi?

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
227
333
"Nitasema ukweli daima fitna kwangu mwiko".

Ni kaulimbiu inayoeleza wajibu na sifa ya kweli ya mwanaCCM kwa mujibu wa katiba ya chama hicho.

WanaCCM wengi wamekuwa wakitumia kauli hii kuonyesha uzalendo wao na sifa yao pamoja na chama chao.

Kauli hii ni msisitizo wa uwazi, ujasiri na wajibu wa kusema ukweli kwa kila mwanachama wa chama hicho tawala na kikongwe nchini.

Pia kauli hii inasanifu msimamo na jina la chama chenyewe "Chama Cha Mapinduzi" chenye dhima ya mabadiliko na mageuzi ya mifumo kutoka kwenye udhaifu kwenda kwenye ubora zaidi ili kuchochea maendeleo na uhuru wa watu.

Hata hivyo kwa nyakati tofauti inaweza kuonekana kuwa dhima ya mageuzi kupitia kuusema ukweli ndani ya chama hicho tawala imekuwa mwiba mchungu kwa watu wake hasa pale wanapohusisha ukweli huo na chama chao.

Kauli za wanachama wake hazina msimamo wa kimapinduzi muda wote bali hufuata upepo na mitazamo ya Viongozi wao wakuu waliopo madarakani.

Kabla ya mwaka 2014 wanaCCM wengi waliunga mkono mabadiliko ya katiba kwa kipindi hicho Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete akiwa kinara kwenye mchakato huo ambao ulivurugika baada ya kugawanyika kwa wajumbe wa bunge la katiba.

Baada ya uchaguzi Mkuu wa 2015 hayati John Magufuli aliingia madarakani akiwa Rais wa awamu ya tano, baada ya kuapishwa alisisitiza kwa uwazi kuwa suala la kupata katiba mpya halikuwa kipaumbele kwake.
WanaCCM wengi walimuunga mkono na kumsifia walikubaliana nae pasipo kuzingatia mahitaji ya mageuzi ya mifumo ya utawala, siasa na sheria nchini.

Kwa mara nyingine baada ya kifo cha Magufuli, Samia Hassan akachukua madaraka kama Rais wa sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Baada ya muda alitangaza kuunga mkono mabadiliko ya katiba hivyo kuahidi kuufufua mchakato wa katiba mpya.
WanaCCM kama kawaida walishagilia na kumuunga mkono mabadiliko hayo wakiwa ni walewale waliomuunga mkono Magufuli.

Unaweza kujiuliza kuwa je WanaCCM ni wanamapinduzi kweli na wanauopenda ukweli pasipo fitna Kama wameshindwa kuwa na mtazamo wa kudumu kuhusu katiba ya nchi bali wanayumbishwa na mawazo binafsi ya Viongozi wao?

Si hivyo tu WanaCCM wanalalamikiwa kukosa kuunga mkono hoja mbalimbali zisizo za kiitikadi za vyama bali zenye maslahi kwa Taifa na zenye kuutafuta ukweli.

Mapinduzi ya kweli hayawezi kujitenga na kusema ukweli kama inavyodhihirishwa kwenye kanuni na katiba ya chama hicho lakini wanachama wake wengi wamekuwa kama fuata upepo wasio na upeo wa kimsimamo na kuujua ukweli.

Hata leo hii bado kuna WanaCCM wanao wanyoshea vidole wananchi wanaohoji Mkataba wa makubaliano ya uendeshaji wa bandari nchini baina ya Mamlaka ya bandari TPA na serikali ya Dubai.

WanaCCM hao hawahoji hoja za msingi wanazozitoa wananchi na wanaharakati wanaopinga mkataba huo bali wao huwatuhumu kuwa hawana uzalendo na hawaitakii mema serikali.
Mpaka Leo hii Kuna WanaCCM wanaoamini kuwa serikali ipo sahihi na haipaswi kuhojiwa katika kila ifanyacho lakini moyoni mwao wanakuwa na maswali ya kujiuliza.

WanaCCM ni Wanamapinduzi wa kweli?
 
Back
Top Bottom