Spika Tulia awaonya CCM waache kigeugeu, adai wapo Watu ndani ya CCM Wanamvuta Shati Rais Samia. Awaambia 2025 Siyo Mbali!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,004
142,036
Spika wa Bunge la JMT Dkt. Tulia PhD amewataka Wana CCM kuacha kigeugeu na badala yake wajikite kutekeleza Ilani

Tulia amesema wako Watu ndani ya CCM Wanamvuta Shati Rais Samia, hawaeleweki

Amewaonya watambue kuwa 2025 Wana deni kama watakuwa hawajatekeleza Ilani ya CCM ya 2020

Source: Mwananchi

Mlale Unono 😃😃🔥
---
Tulia.jpeg
Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson, amewaonya baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuepuka tabia ya kuwa kigeugeu kwa kuunga mkono upande wa pili, huku akiwasihi kutokubali ubaguzi na ukabila.

Dk Tulia ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini, ametoa kauli hiyo leo Jumatano Agosti 2, 2023 wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Iyela, baada ya kukagua ujenzi wa miradi ya mabweni mawili ya wanafunzi wa kike katika Shule ya Sekondari Samora uliogharimu Sh60 milioni fedha za mfuko wa Jimbo.

“Wapo watu ndani ya chama wanataka kumvuta shati Rais Samia Suluhu Hassan, hawaeleweki. Watambue wana deni katika uchaguzi mkuu 2025,” amesema.
 
Akina Nani SASA. Awataje kama anawajua
Akina Nani SASA. Awataje kama anawaju
Tulia ndiye alimkaanga Mwenyekiti wa Mkoa wa Mbeya kwa Makamo wa rais kiasi na Makamo wa rais akaingia mkenge kiasi badala ya kusimsikiliza kwa utulivu Mwenyekiti wa Mkoa alipokuwa akielezea changamoto, yeye akawa anamsubiri amalize kuongea ili amjibu kwa style aliyomjibu. Kutu ambacho was very strange.

Aliacha hoja akamvamia mtoa hoja.

Hiyo ni kazi ya Tulia na sasa anamalizia baada ya kuona kuwa ameshatafuniwa.
 
Katika watu/wanawake vichwa hapa nchini kwenye uongozi huyu alikuwa mmoja wapo. Nilimuona mara ya kwanza wakati wa bunge lile la katiba la JKM.

Ni lijisemea moyoni huyu atakuwa Spika. Na ikawa hivyo. Lakini katuangusha sana, ndio katuangusha bigtime kusema ukweli.

Kupitiasha huu mkataba wa bandari namna ile tulioishuhudia bungeni na mapungufu yake yote aah inasikitisha sana.

Hivi Spika hana nafasi ya kumshauri Mh Rais? Kwa taaluma yake ya sheria hakuona popote pa kumshauri Mh Rais kwenye huu Mkataba? Nani anamvuta Mh Rais Shati/Blauzi mpaka hapo?

Si Bunge wala Serikali waliobahatika kujua nini kitatokea baada ya Mkataba huu kupitishwa na Bunge kama ulivyo?
 
Spika wa Bunge la JMT Dr Tulia PhD amewatama Wana CCM kuacha kigeugeu na badala yake wajikite kutekeleza Ilani

Tulia amesema wako Watu ndani ya CCM Wanamvuta Shati Rais Samia, hawaeleweki

Amewaonya watambue kuwa 2025 Wana deni kama watakuwa hawajatekeleza Ilani ya CCM ya 2020

Source: Mwananchi

Mlale Unono
Mbeya ccm vipande vipande

Screenshot_2023-08-02-15-41-11.jpg
 
hawaeleweki

Tayari chama kongwe dola kimetikisika.

Wataalamu wa taasisi / organisation/ kampuni kubwa kama hii ya CCM hukisia kuwa uhai wake ni ngumu kupindukia miaka 60 ya uhai lazima kitapitwa na wakati kwa sababu mbalimbali.

Upetevu wa mawazo, kuishiwa pumzi, mazowea, kuishiwa gamba la kujivua kwani hakuna tena ngozi mpya kwenye mwili kongwe n.k ni sababu nyingi zinazosababisha kufikia ukomo wake kiasilia na hakuna tena jinsi ya kuweza kuji-brand upya zaidi ya kifo cha taasisi hii iliyojivika uchama dola kongwe.

Toka uhuru sasa ni vizazi 3 vya miaka ishirini ishirini zimepita na CCM hakika imepitwa na wakati sasa ni zamu ya chama kingine cha siasa kushika ndola imefika.

Huko Mexico bara la Latin Amerika chama dola kongwe PRI nacho kinafunga virago vyake.
1691018288143.png

Chama kikongwe tawala nchini Mexico kilivunjika Jumatatu, huku maseneta wanne wakuu wakijiuzulu kutokana na mizozo ya ndani na kupoteza jimbo kuu la mwisho ambalo chama kilitawala.

Chama hicho kongwe cha Mapinduzi vya Kitaasisi cha Mexico PRI kilishikilia urais na takriban majimbo yote nchini Mexico bila usumbufu kwa miaka 70.

Lakini PRI, kama chama hicho kinavyojulikana, kimepunguzwa na kubakia kivuli cha ukale wake wa zamani kutokana na kuibuka kwa chama cha Morena Andres Manuel Lopez Obrador, ambacho kilishinda ugavana wa ngome kuu ya mwisho ya PRI, Jimbo la Mexico, mwezi uliopita.

Siku ya Jumatatu, maseneta wanne wakuu wa PRI na wafuasi kadhaa walitangaza kukihama chama hicho. Maseneta wakiongozwa na aliyekuwa katibu wa mambo ya ndani Miguel Osorio Chong walitangaza kuwa wataunda kundi jipya liitwalo "Congruence for Mexico." Kundi hilo jipya halitaweza kushindana katika uchaguzi wa urais wa 2024.

PRI, ambayo sasa inatawala majimbo mawili pekee yenye wakazi wachache, sasa ni chama cha nne kwa ukubwa nchini Mexico, ikifuatiwa na Morena, chama cha kihafidhina cha National Action Party na Citizen's Movement chenye msimamo mkali.

Chong na maseneta wengine walikuwa wamepinga majaribio ya kiongozi wa sasa wa chama cha PRI Alejandro Moreno kushikilia mamlaka.
 
Back
Top Bottom