Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,949
- 74,431
Sawa tuseme mleta mada kumbe ni muoga ndio maana anakuja na jina bandia. Jee hiyo inafuta mantiki ya swali kuwa kwa nini Rais na mwenyekiti wa chama anaogopa wapinzani wake wakati yeye ana sema anatenda mambo bora haijapata kutokea? Membe si atakuwa anajisumbua tuu ili kudhihirisha demokrasia ndani ya chama wakati akipata kura hazizidi 2%?Wewe unaogopa nini kuja na jina lako halisi halafu ndio umnyooshee kidole mtu mwingine una fikiri anaogopa?
Na hawa wapinzani watafanya nini kwa huyu ambaye ni "chaguo la Mungu"?
Au anajua kuwa kuna mahali wanatupiga fix hivyo kuruhusu upinzani waseme basi wapiga kura watajuwa kuwa tunachezewa kekundu keusi?