Rais Magufuli umetufikisha hapa...

Rais Magufuli umetufikisha hapa...

Chukulia chekechea wewe unampandia miti anakuwa nayo, akifikisha muda wa kwenda chuo huna hata sababu ya kwenda Heslb kuomba mkopo
Sio kwa kizazi hiki mtoto akijua tu mama/baba anamiti, inakatwa mmoja baada ya mwingine ili anunue iPhone 30 yamwaka huo chuoni!!!

Wapo wa zee wali invest kujenga majumba mjini kati, kwa maisha ya watoto wao vijana wameuzauza yoote na shule Hamna kitu wanakula bata tu mpaka umasikini umewarudia

Mfumo wetu wamaisha na elimu yetu ni ovyoooo sana, unaitaji kuangaliwa upya
 
Tunapaswa kuwafikirisha watoto wetu nje ya AJIRA wakiwa bado wadogo.
Leo Unampangia Miaka 25 ijayo mwanao aje aajiliwe alipwe Laki saba?
Wakati unaweza kumpandia shamba la miti kwa shilingi kama hata millioni tatu miaka 10 sio 25 unayopanga akawa ni Millionea.

Wazazi mtutendee haki acheni siasa.
Nimeipenda hiyo kitu japo elimu ni muhimu zaidi.
 
Mwanangu utamaliza chuo baada ya miaka 25......

Jumla ya ada yako ni tsh milion 16,800,000/= .

Tanzania itakupa Mshahara laki Tsh.700,000/= .... kwa degree yako....ila toa asilimia 10% Nssf (70,000/=)...kodi asilimia 9% (63,000/=)...Helsb asilimia 15% (105,000/=)...NHIF asilimia 3% (21,000/=)...utabakiwa na laki Tsh.441,000/=.....toa nauli kwa mwezi Tsh 90,000/=..toa chakula cha mchana Tsh.90,000/=..toa pango Tsh.100,000/=...toa chakula cha nyumbani elfu Tsh.90,000/= toa gharama za kiwi na doby + nguo za ofisi Tsh. 30,000/=.......utabakiwa. na elfu "Tsh. 41,000/=".. .Aya jitahidi Mwanangu shule njema angalia usigongwe na magari!
Hahaha, Duuu ataenda shule na mawazo lukuki!!![emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kwani umeanza kukatwa awamu hii hayo makato? Kuhusu ongezeko la HELSB sio milele ukimaliza mkopo utarudi kweny mshahara wako ule ule na utasahau!
Anashangaa hii lakini hajiulizi wanaolipwa 350,000 na wanaishi hapa Tz. Yeye atwambie amekuwa akasoma mpaka amefika hapa wazazi wake walikuwa wanapataje?
 
Nilianza kazi ya kufundisha shule za msingi 1996 Julai!Nakumbuka waziri mkuu alikuwa Sumaye alitoka mbele ya vyombo habari akashauri kwa kuwa serikali kuu haina fedha za ajira mpya(1996/97) halmashari ziwape japo posho hao walimu wapya!Nakumbuka nilikuwa nalipwa tsh20000/- na ilinitosha.Mwaka uliofuata nikaingizwa kwenye payroll za serikali tangu hapo sikuwahi kunyimwa 'annual increament' hadi 2016/17!sikuwahi kulipwa mshahara pasi kupatikana salary slip hadi 2016/17 kwa Mara ya mwisho nimefika kwenye ofisi ya mkurugenzi mwezi February 2017 nipate japo hati yangu ya mshahara nikaambiwa hazijatoka.Nawashauri wazazi na vijana someni mwongeze maarifa nyakati zimebadilika fikiria kujiajiri kama unategemea kuajiriwa siyi vibaya jiandae kisaikolojia kuishi maisha ya matakwa mwajiri wako
Umesema vyema mkuu, na hakuna tajiri/mwajiri yeyote awaye atakupa mshahara wa kukutosha, never. Achia mbali serikalini ambako ki uharisia si sehemu ya kukufanya uwe tajiri objective ya wewe kuitumikia serikali yako ni kuihudumia nchi yako na watu wako, full stop. Wewe kuwa tajiri ni complimentary tu.
 
Na ili nchi iwe salama tuache kulalamika tuache kuwaona viongozi wetu hawafai kwa kila jambo kila kiongozi ana vision yake!hata Mimi na wewe tuna vision tofauti so kila mmoja awajibike.
 
Mwanangu utamaliza chuo baada ya miaka 25......

Jumla ya ada yako ni tsh milion 16,800,000/= .

Tanzania itakupa Mshahara laki Tsh.700,000/= .... kwa degree yako....ila toa asilimia 10% Nssf (70,000/=)...kodi asilimia 9% (63,000/=)...Helsb asilimia 15% (105,000/=)...NHIF asilimia 3% (21,000/=)...utabakiwa na laki Tsh.441,000/=.....toa nauli kwa mwezi Tsh 90,000/=..toa chakula cha mchana Tsh.90,000/=..toa pango Tsh.100,000/=...toa chakula cha nyumbani elfu Tsh.90,000/= toa gharama za kiwi na doby + nguo za ofisi Tsh. 30,000/=.......utabakiwa. na elfu "Tsh. 41,000/=".. .Aya jitahidi Mwanangu shule njema angalia usigongwe na magari!

Umeiweka vizuri sana Jelavic.

Inataka watu watafakari na kujiuliza.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom