Rais Magufuli, tuache tupumzike

Rais Magufuli, tuache tupumzike

Ciprofloxacin.

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2015
Posts
1,583
Reaction score
2,702
Mungu amejibu maombi yako, na haja ya moyo wako, ni nani asiyejua kuwa wewe hutaki kabisa upinzani Tanzania?

Hujifichi kuonyesha chuki yako hadharani dhidi ya upinzani.
Naomba nikuulize Tafadhali mheshimiwa Rais, Kama nitakukosea nisamehe bure .

Risasi alizomiminiwa Tundu Lissu na watu wanaoitwa "wasiojulikana ". ingekuwa risasi hizo kwa mfano kamiminiwa mkuu wa mkoa au waziri yoyote, hao wahalifu wangekuwa hawajapatikana?

Tuna makovu ya mateso mengi, kuwa mpinzani hapa Tanzania ni kuchagua kifo, bado tunamwomboleza mawazo, Ben Saanane, Kanguye, Azori Gwanda na wengine wengi.

Mheshimiwa Rais, hatutaki kupiga kura ili tukipishe chama chako kitawale milele Kama wewe unavyotaka sasa wakuu wa mikoa na wilaya watatufanyaje?

Tumeamua kupumzika ili nyie mnaopendwa sana muendelee kupendwa na kutawala milele, ajabu tena imekuwa kero.

Na 2020 pia hatutapiga kura, tuache tupumzike, Tafadhali Tumechoka.
Wana CCM wapo wengi watapiga kura na kujipatia ushindi mnono.
Tumeshajua hata tukipiga kura hatushindi kwa sababu CCM huwa inashinda hata kabla ya kupiga kura sasa tunapiga kura za nini?
Tuache tupumzike.
 
Anatuona mazuzu sana lakini yote yana mwisho. Hakuna mtawala aliyekuwa katili kama Jean Baptise Bhokasa. Wapinzani wake aliwakamata na kuwalisha mamba wake.
Leo tunamsoma kwenye vitabu tu. Amepumzika anaposahili.
 
Tumechoka kwa kweli kuchagua wafungwa watarajiwa, tumechoka kusababisha vilio kwa watoto wazazi wanapopata ulemavu unaosababishwa na vipigo vya polisi na risasi za wasio julikna, tumechoka kuona wanatekwa na wakurudi wana majeraha makubwa, tumechoka kusababisha wajane kwenye taifa hili, tumechoka kukuona ukikebehi na kutukana waliochagua wapizani, naunga mkono hoja atuache tupumzike.
 
Anatuona mazuzu sana lakini yote yana mwisho. Hakuna mtawala aliyekuwa katili kama Jean Baptise Bhokasa. Wapinzani wake aliwakamata na kuwalisha mamba wake.
Leo tunamsoma kwenye vitabu tu. Amepumzika anaposahili.
Mwanzo Watu Waliamini Wanaweza Kuleta Mabadiliko Kupitia Sanduku La Kura.

Ila Kwa Kuwa Tumaini Limepotea.

Altenative Itakayotokea Ni Mbaya Zaidi,

Sijui Kwanini System Imemwacha Kibwengo Huyo Wa Chato Avuruge Nchi Kabisa !
 
Mungu amejibu maombi yako, na haja ya moyo wako, ni nani asiyejua kuwa wewe hutaki kabisa upinzani Tanzania?
Hujifichi kuonyesha chuki yako hadharani dhidi ya upinzani.
Naomba nikuulize Tafadhali mheshimiwa Rais, Kama nitakukosea nisamehe bure .
Risasi alizomiminiwa Tundu Lissu na watu wanaoitwa "wasiojulikana ". ingekuwa risasi hizo kwa mfano kamiminiwa mkuu wa mkoa au waziri yoyote, hao wahalifu wangekuwa hawajapatikana?
Tuna makovu ya mateso mengi, kuwa mpinzani hapa Tanzania ni kuchagua kifo, bado tunamwomboleza mawazo, Ben Saanane, Kanguye, Azori Gwanda na wengine wengi.
Mheshimiwa Rais, hatutaki kupiga kura ili tukipishe chama chako kitawale milele Kama wewe unavyotaka sasa wakuu wa mikoa na wilaya watatufanyaje?
Tumeamua kupumzika ili nyie mnaopendwa sana muendelee kupendwa na kutawala milele, ajabu tena imekuwa kero.
Na 2020 pia hatutapiga kura, tuache tupumzike, Tafadhali Tumechoka.
Wana CCM wapo wengi watapiga kura na kujipatia ushindi mnono.
Tumeshajua hata tukipiga kura hatushindi kwa sababu CCM huwa inashinda hata kabla ya kupiga kura sasa tunapiga kura za nini?
Tuache tupumzike.
Mkuu upo sahihi kabisa, binafsi naumia kila ninapomuona mbunge niliemchagua anahangaika na kesi za kisiasa mahakamani , naifikiria familia ya Akwilina, Azory, Ben Saa nane, Tundu Lissu na wengine waliopoteza wapendwa wao moyo unaniuma sana, kama yote haya ni kwa sababu ya siasa ni heri nisiwe sehemu ya laana hii
 
Anatuona mazuzu sana lakini yote yana mwisho. Hakuna mtawala aliyekuwa katili kama Jean Baptise Bhokasa. Wapinzani wake aliwakamata na kuwalisha mamba wake.
Leo tunamsoma kwenye vitabu tu. Amepumzika anaposahili.
Na wewe tutakusoma kwenye vitabu tu dada Mungu akikuchukua!
 
Mkuu upo sahihi kabisa, binafsi naumia kila ninapomuona mbunge niliemchagua anahangaika na kesi za kisiasa mahakamani , naifikiria familia ya Akwilina, Azory, Ben Saa nane, Tundu Lissu na wengine waliopoteza wapendwa wao moyo unaniuma sana, kama yote haya ni kwa sababu ya siasa ni heri nisiwe sehemu ya laana hii
Ujinga wao ndiyo uliopelekea kufikishwa mahakamani mkuu.
 
Back
Top Bottom