Rais Magufuli, tuache tupumzike

Rais Magufuli, tuache tupumzike

You can control your actions, but not the consequences of your actions. Ndivyo ambavyo ilivyo kuwa sasa. Viongozi wa CCM wametumia miaka minne kukandamiza demokrasia na uhuru wa kujieleza vitu ambavyo vipo kikatiba. Waliona faraja na furaha kubwa kuyafanya mambo hayo kwa mbwembwe zote wakisaidiwa na vyombo vya dola. Haya sasa waalikwa wamelisusia pilau, wenyeji wajifurahishe wenyewe.
 
Sababu ni kuwa wananchi wamewachoka wapinzani kwa kuwa ni waongo sana kwa kuwa sasa wanatetea mafisadi wakati walikuwa wanawapinga hapo awali.
Ndo maana wamewaachia mjitangazie ushindi nyie kipenzi cha watu sasa mbona Rais wenu anawatishia tena wakuu wa mikoa?
 
Kuwaita watendaji wa kata nchi zima ikulu na kuwapa maelekezo, lilioneka jambo jema kwa baadhi ya watu hapa jukwaani, na hata wakaliunga mkono kwa nguvu zote. Hawakujua kuwa lilikuwa ni "preconceived idea" na kibaya zaidi kwa wale wenye ufahamu mpana wanatambua ya kwamba tayari "it has already formed consequences of which the impacts have intreciable maze"
 
Jpm umefanikiwa kuuwa vyama Pinzani(CHADEMA,CUF,ACT) lakini bila kujua umetengeneza mpinzani mmoja anaeitwa UMMA WA WATANZANIA.
Wanaokusifu wana acces na media ila wanakukosoa wanatafuta timing tu
 
Mungu amejibu maombi yako, na haja ya moyo wako, ni nani asiyejua kuwa wewe hutaki kabisa upinzani Tanzania?
Hujifichi kuonyesha chuki yako hadharani dhidi ya upinzani.
Naomba nikuulize Tafadhali mheshimiwa Rais, Kama nitakukosea nisamehe bure .
Risasi alizomiminiwa Tundu Lissu na watu wanaoitwa "wasiojulikana ". ingekuwa risasi hizo kwa mfano kamiminiwa mkuu wa mkoa au waziri yoyote, hao wahalifu wangekuwa hawajapatikana?
Tuna makovu ya mateso mengi, kuwa mpinzani hapa Tanzania ni kuchagua kifo, bado tunamwomboleza mawazo, Ben Saanane, Kanguye, Azori Gwanda na wengine wengi.
Mheshimiwa Rais, hatutaki kupiga kura ili tukipishe chama chako kitawale milele Kama wewe unavyotaka sasa wakuu wa mikoa na wilaya watatufanyaje?
Tumeamua kupumzika ili nyie mnaopendwa sana muendelee kupendwa na kutawala milele, ajabu tena imekuwa kero.
Na 2020 pia hatutapiga kura, tuache tupumzike, Tafadhali Tumechoka.
Wana CCM wapo wengi watapiga kura na kujipatia ushindi mnono.
Tumeshajua hata tukipiga kura hatushindi kwa sababu CCM huwa inashinda hata kabla ya kupiga kura sasa tunapiga kura za nini?
Tuache tupumzike.
Hata wananchi hatutaki upinzani feki...jpm endelea kukanyaga sisi watanznia tutawamalizia zaidi kama tunavyowamalizia sasa.
 
Anatuona mazuzu sana lakini yote yana mwisho. Hakuna mtawala aliyekuwa katili kama Jean Baptise Bhokasa. Wapinzani wake aliwakamata na kuwalisha mamba wake.
Leo tunamsoma kwenye vitabu tu. Amepumzika anaposahili.
huyu ataliwa na simba wa bugiri
 
Jpm umefanikiwa kuuwa vyama Pinzani(CHADEMA,CUF,ACT) lakini bila kujua umetengeneza mpinzani mmoja anaeitwa UMMA WA WATANZANIA.
Wanaokusifu wana acces na media ila wanakukosoa wanatafuta timing tu
Mlibisha weee sasa mmekaaa.....operation tokomeza upinzani feki.
 
Tume ya uchaguzi ina washinda wake kwapani, kwenda kupiga kura ni kujichosha tu
 
Sina muda wa kupoteza kukaa kwenye foleni 2020 labda 2025 panapo MAJALIWA ya mungu,,, kwa nachokiona
 
Safari hii kila mtu kajifungia kwake sasa kama ana ubavu atufate majumbani, tutampa kipigi cha mbwa koko mpaka bosi wake akae chini
Muroto toa kipigo cha mbwa koko kwa wasiojiandikisha kupiga kura
 
Sababu ni kuwa wananchi wamewachoka wapinzani kwa kuwa ni waongo sana kwa kuwa sasa wanatetea mafisadi wakati walikuwa wanawapinga hapo awali.
Ni kweli kabisa upo sahihi bwana mkubwa
 
Back
Top Bottom