OMh. Rais Magufuli natumai hujambo na ni mwingi wa afya njema, hata mimi mwananchi wako niko salama na wa afya njema nikiendelea kujivunia kuwa mtanzania nnaeheshimika kwa sasa kwa sababu ya uongozi wako mathubuti.
Mh. Rais sitaki nikuchoshe sana acha nikujuze tu jambo hili linalotukera sana huku mtaani japo nafahamu huenda unafahamu pia.
Mh. Rais kwa maadili ya kitanzania na jamii nzima ya watanzania mdada au mwanamke kuvaa nguo zinazobana na kuchola mwili hutafusiliwa ni kukosa heshima kwa jamii, lakini pamoja na hilo dada zetu huku mjini ndio wanazidi kuvaa hivi vinguo vya aibu kiasi kwamba akipita usoni pengine umekaa na mama au baba huenda ukalazimika kufumba macho ili apite kwani ni fedhea na aibu ya aina yake.
Mh. Rais natambua kuwa kauli yako ni sheria kwetu na ukitamka sie lazima tutekeleze hivyo basi nakuomba kwa niaba ya wapenda maadili utoe kauli inayozuia uvaaji huu wa aibu, zaidi nikutakie afya njema na nnazidi kukuombea kwa mungu aendelee kukupa nguvu nyingi na kheri katika utumishi wako.
Nenda kwenye nyumba za makumbusho ili uone mila za mavazi ya kitanzania au kiafrika. Wasichana hawakuvaa chochote juu, walijifunga gome la mti chini basi.Kama unataka turudi kwenye maadili ya kitanzania ni hapo kila mtu atakavyokaa uchi. Angalia picha za wasichana wa Swaziland ndivyo wadada wa Tanzania walikuwa wakivaa. Sisi si waarabu wala wazungu wa miaka ya 30s ambao walikuwa wanafunika miili yao yote.