Rais Magufuli, Tengua uteuzi wa Mbunge mmoja mwanaume umteue Aggrey Mwanry na kisha umteue waziri wa Nishati na Madini

Kama ni mchapa kazi aache kazi ya uRC ajiajiri kwa kuanzisha kiwanda kidogo naamini ana mtaji wa kutosha maana amekuwa mbunge/waziri. Ni wakati sasa wa kuanza kutokutegemea kuteuliwa muanze kujiajiri sio mnawaambia vijana tu

BTW: Sipangiwi
 
Wabunge wa kuteuliwa na Rais kisheria na kikanuni wanaweza kusitishiwa Ubunge wao na Rais kweli? Baada ya kuapishwa?
Wamekubali kila kinachofanywa na bwana yule kiwe ndio sheria mpya.. Inashangaza na kusikitisha sana!
 
haa haa kwani wakinga wamekukosea nini jamani
Sio Wakinga nadhani amemaanisha Renatus Mkinga, huyu hapa:

Mkinga.png
Hiyo mishipa ya uso jinsi ilivyosimama wala usidhani Mwandishi alikuwa ametoka na Mkinga alitaka amsikie huko huko aliko; wala :D:D!! Yuko hapo hapo na akinyoosha kidogo tu huo mkono atamgusa! Na wala usidhani labda Mwandishi aliongea jambo ambalo limemfanya Mkinga akasirike; hamna kitu kama hicho; ndo ka-relax hapo!
 
Habari zenu familia ya JF. Mi sio mnafiki wala sina undugu na wala ukabila na Agrey Mwanry. Wote mtakubali hii ni nyota iliyozimwa na Mafuriko ya UKAWA.

Sahivi ni RC Tabora na anafanya mambo mazuri tu ikiwa ni pamoja na mkoa wake kuvuka lengo ktk kutengeneza Madawati kwa shule za Msingi.

Pia alipokuwa Naibu waziri TAMISEMI alikuwa akifanya kazi vizuri sana kuliko hata waziri Kasim Majaliwa aliyekuwa juu yake.

Hivyo kwa heshima na taadhima namshauri Rais kama atapita humu, atengue uteuzi wa Mbunge mwanaume na kumpa Mwanry nafasi hiyo ili baada ya hapo ateuliwe Waziri wa Nishati na Madini.

Nafasi ya RC Tabora apewe mtu mwingine na Mbunge aliyetenguliwa uteuzi wake apewe pia kazi nyingine.

Agery Mwanry alikuwa Mbunge wa Siha- Kilimanjaro kabla ya kusombwa na mafuriko ya UKAWA mwaka 2015.

Naomba ushauri wangu ufanyiwe kazi. Naomba kuwasilisha.
Self-Promo at Work
 
Ukianzisha Uzi na kuanza kujitetea ya kuwa wewe sio mnafiki inaashiria ya kwamba wewe ni MNAFIKI 1st class with honour mkuu.
Kweli mkuu, huyu mnafiki tuu toka lini mtu anagombea ubunge kupitia JF? Majitu mengine yana akili za kenge maana mkuu alishasema hapangiwi hayataki kuelewa.
 
Sio Wakinga nadhani amemaanisha Renatus Mkinga, huyu hapa:
Hiyo mishipa ya uso jinsi ilivyosimama wala usidhani Mwandishi alikuwa ametoka na Mkinga alitaka amsikie huko huko aliko; wala :D:D!! Yuko hapo hapo na akinyoosha kidogo tu huo mkono atamgusa! Na wala usidhani labda Mwandishi aliongea jambo ambalo limemfanya Mkinga akasirike; hamna kitu kama hicho; ndo ka-relax hapo!
haa haa nahisi alikimaliza kuongea lazima ameze panadol..
 
Magu hana mamlaka ya kutengua ubunge wa mtu mkuu ,mkuu muwe mnajipa hata muda kidogo wa kupitia katiba ya nchi
 
Hah! Hakuna kitu kama hicho,jamaa anakaba mpaka penalti.
Kule hazina kaweka wajomba,yaani huku migodini aache kumuachia home boy mbunge wa Chatto

Thubutu!
 
mwanry akiwa tamisemi alikuwa ananifurahisha kila eneo kafika, kayaona matatizo hayo na atatatua.

jamaa yuko vizuri kwenye kuongea, na porojo.
 
Wizara ya nishati, ni nuksi. Wizara haimuachi mtu salama.
Mikataba mibovu, tamaa binafsi ya viongozi imedhoofisha sekta ya nishati(TANESCO),madini(mirahaba isiyo na tija).
Usimuombee mtu kupelekwa wizara hii, Simbachawene alikaa kwa muda mfupi, lakini, naye ametajwa katika taarifa ya uchunguzi.
Teuliwa katika Wizara zingine sio, Nishati na madini.
 
Back
Top Bottom