MKWEPA KODI
JF-Expert Member
- Nov 28, 2015
- 28,707
- 71,003
Habari wakuu,
Naamini wote tumemsikia mkuu wa mkoa wa Dar alipokuwa akitoa agizo kwa vijana wetu wa JKT, kuwa mtu mwenye gari akitupa taka barabarani asipigwe fine bali apewe adhabu ya kupiga deki barabara kwa kilomita isiyopungua moja, kuna wakati huwa tunatembea na watoto wetu kwenye magari au wagonjwa, kuna wengine hawana taarifa juu ya adhabu hii ambayo sijawahi kuisikia popote dunia nzima, sio kwamba nataka kutetea uchafu hapana, ninachotaka kusema ni kuwa tuheshimu sheria, adhabu hii nina hakika kuna siku itakuja kuleta matatizo, kwa sababu JKT ni wanajeshi, hayo maji ya kupigia deki madereva watayatoa wapi?, urefu wa barabara kilomita moja sio mchezo, foleni za Dar ni hatari, hii sio adhabu kabisa kwenye nchi iliyostaarabika kama Tanzania naomba matamko haya ya mkuu wa mkoa Dar yatenguliwe haraka sana kabla madhara hayajatokea
N.B Sio kila mwenye gari ana hela