Shujaa Mwendazake
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 3,735
- 6,281
Dar es Salaam. Siku moja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla kuagiza wenye mabasi kuyaingiza ndani ya kituo cha mabasi cha Magufuli wakati wa kupakia na kushusha abiria, baadhi ya wananchi wamekuwa na maoni tofauti kuhusiana na uamuzi huo.
Makalla alitoa agizo hilo jana Ijumaa Julai 9,2021 wakati akisikiliza kero za wafanyabiashara katika stendi hiyo, ambao walisema miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo ni pamoja na kukosa wateja kwa kuwa baadhi ya mabasi hupakia na kushusha abiria maeneo mengine.
Hata hivyo, mchambuzi wa masuala ya siasa, Richard Mabala kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika: Sijui kwanini watu wa mipango wanapenda kuangalia urahisi kwao badala ya kuangalia urahisi kwa ajili ya wateja, wamejenga barabara nzuri hadi Ubungo kwanini mabasi yasiwafikishe abiria karibu zaidi na nyumbani”.
Naye Hajia Soza katika ukurasa wake wa Instagram ameandika: Sahihi sana mkuu Amos Makala, na Dodoma tusione aibu kulisimamia hili kwani mabasi mengi yatokayo safari siku hizi huingia stendi kuu Dodoma wanapojisikia, sasa hizi stendi zilijengwa za nini? Halafu uongozi unalichukuliaje suala hili?”
Kwa upande wake Tanzania Bound Buses Flag of Tanzania wameandika: “Fikiria gari limetoka Mwanza limefika stendi ya Magufuli saa 7 usiku, na wewe kama abiria unaishi Ilala, unalazimishwa ushuke hapo hapo stendi wakati basi linaelekea kupaki maeneo ya Shekilango”.
Hata hivyo, akizungumza na Mwananchi, Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa), Joseph Priscus amesema watatekeleza agizo hilo lakini, changamoto iliyopo ni baadhi ya stendi kuwa mbali na makazi ya watu.
Amesema kumekuwa na kilio cha muda mrefu kutokana na stendi nyingine kuhamishiwa nje ya mji, na kusababisha usumbufu kwa abiria ikiwemo kuwagharimu fedha nyingi kwa ajili kupanda bajaji au bodaboda.
Awali, kituo cha mabasi Ubungo kilihamishiwa hadi eneo la Mbezi ambako ndio kumejengwa stendi mpya ya Magufuli ikiwa ni umbali wa kilomita 11.7 (Ubungo-Mbezi) huku kutoka katikati ya Jiji la Dar es Salaam kwenda Mbezi ni umbali wa kilomita 20.
Tangu kuzinduliwa na kuanza kazi kwa stendi ya Magufuli ambayo inatajwa kuwa na ubora nay a kisasa kwa nchi za Afrika Mashariki, baadhi ya wamiliki na abiria wamekuwa wakilalamikia umbali hasa kwa safari za masafa ya mbali ambazo nyingi huanza saa 12:00 alfajiri.
Mwananchi Gazeti.