Rais Magufuli, tengua haraka agizo la Makonda kabla halijaleta madhara yoyote

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,708
70,998
Habari wakuu,

Naamini wote tumemsikia mkuu wa mkoa wa Dar alipokuwa akitoa agizo kwa vijana wetu wa JKT, kuwa mtu mwenye gari akitupa taka barabarani asipigwe fine bali apewe adhabu ya kupiga deki barabara kwa kilomita isiyopungua moja, kuna wakati huwa tunatembea na watoto wetu kwenye magari au wagonjwa, kuna wengine hawana taarifa juu ya adhabu hii ambayo sijawahi kuisikia popote dunia nzima, sio kwamba nataka kutetea uchafu hapana, ninachotaka kusema ni kuwa tuheshimu sheria, adhabu hii nina hakika kuna siku itakuja kuleta matatizo, kwa sababu JKT ni wanajeshi, hayo maji ya kupigia deki madereva watayatoa wapi?, urefu wa barabara kilomita moja sio mchezo, foleni za Dar ni hatari, hii sio adhabu kabisa kwenye nchi iliyostaarabika kama Tanzania naomba matamko haya ya mkuu wa mkoa Dar yatenguliwe haraka sana kabla madhara hayajatokea
N.B Sio kila mwenye gari ana hela
 
Weka Dustin kwenye gari lako, mtu akipanda unamtangazia kuwa ni marufuku kutupa taka nje
Mkuu nazungumzia utekelezaji wa hiyo adhabu, hebu tulia uusome uzi vizuri halafu ndiyo urudi tena
 
Ukitaka kujua swala la kumfunza mwanao umuhimu wa kutunza mazingira ni jukumu lako mzazi, pita makongo kuelekea tegeta mtoto wako atupe uchafu pale. Ndo utajua moto wake
Habari wakuu,

Naamini wote tumemsikia mkuu wa mkoa wa Dar alipokuwa akitoa agizo kwa vijana wetu wa JKT, kuwa mtu mwenye gari akitupa taka barabarani asipigwe fine bali apewe adhabu ya kupiga deki barabara kwa kilomita isiyopungua moja, kuna wakati huwa tunatembea na watoto wetu kwenye magari au wagonjwa, kuna wengine hawana taarifa juu ya adhabu hii ambayo sijawahi kuisikia popote dunia nzima, sio kwamba nataka kutetea uchafu hapana, ninachotaka kusema ni kuwa tuheshimu sheria, adhabu hii nina hakika kuna siku itakuja kuleta matatizo, kwa sababu JKT ni wanajeshi, hayo maji ya kupigia deki madereva watayatoa wapi?, urefu wa barabara kilomita moja sio mchezo, foleni za Dar ni hatari, hii sio adhabu kabisa kwenye nchi iliyostaarabika kama Tanzania naomba matamko haya ya mkuu wa mkoa Dar yatenguliwe haraka sana kabla madhara hayajatokea
N.B Sio kila mwenye gari ana hela
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom