Rais Magufuli, somo la managing diversity kwa Serikali yako linahitajika

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,604
Wanabodi,

Kwa kilichotokea leo Arusha, Watendaji wa serikali wanahitaji kupigwa msasa wa somo linaloitwa "Managing Diversity " ila wapinzani nao waache mambo yao ya kijinga jinga! .

Kiukweli kabisa nina mashaka na IQ ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, ila tabia za Mbunge wa Arusha, Mhe. Godbless Lema pia ni za ajabu ajabu, na zinaeleweka!.

Gambo anajisikia sana na kujiona kama ni mungu mtu, na hata akiongea, kuna wakati anaongea huku anabetua mdomo!, mtu mwenye cheo cha Mkuu wa Mkoa hawezi kuacha kumtaja mbunge wa eneo husika hata kama humpendi vipi!.

Mhe. rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli huyu RC wako wa Arusha, Mrisho Gambo ni janga!, japo anaweza kuwa ni swahiba wako sana, lakini kiukweli hakufai kabisa!, huwezi kum ignore mchaguliwa wa wananchi mbele wa wapiga kura wake!. Ila pia huyu Mbunge wa Arusha, Mhe. Godbless Lema nae ni majanga!, kichwani hajatulia kabisa, zile fujo alizoanzisha pale, kisa ni kwa kutokutajwa tuu, ni kukosa uvumilivu, subra na ustahimilivu.

Arusha ni ngome yake, wananchi wa Arusha wanaojua, hilo donge la mteule wa rais kutokumtaja kwa makusudi hakukupaswa kumuingilia kati, Lema would lose nothing kwa kuwa calm na ku keep cool mpaka Mkuu wa Mkoa amalize kuongea, you never know, kama Lema angetulia kimya, mwisho wa siku Mkuu wa Mkoa angemtaja tuu wakati wa Shukrani, Lema alifanya papara kuingilia kati.

Wateule wote wa serikali wanapaswa kufahamu kuwa serikali yoyote iliyopo madarakani inapata legitimacy from the people, hivyo viongozi hao ni lazima waheshimu wishes of the people hata kama hukubaliani na chaguo la wananchi kuipiga chini CCM na kuichagua Chadema au upinzani katika eneo husika, hata kama Mrisho Gambo humpendi vipi Mhe. Godbless Lema, kwenye official public events ambazo Mbunge has a role, ni lazima amtaje Mhe. Lema apende asipende kwa sababu Lema ndie chaguo la wananchi wa eneo hilo na ndiye mwakilishi wao halali, RC ni mteule wa rais, yuko hapo at president's please, anaweza kungolewa wakati wowote, wakati Lema ana a five-year renewable contract!.

Mbunge ndiye mwakilishi halali wa wananchi wale na RC ni mteuliwa tuu, hivyo lazima aheshimu the wishes of the people.

Viongozi wa upinzani nao, lazima wajifunze kuheshimu na kutii mamlaka za nchi, Mkuu wa Mkoa ndio mamlaka kuu mkoani hapo, wakati mamlaka inaongea, hakuna mtu mwwingine yoyote mwenye right ya kuingilia na kuikatiza mamlaka. Jana pale kiukweli kabisa Gambo amemuheshimu sana Lema kwa kumvumilia, ningekuwa ni mimi jana pale Lema angekwenda tena kun..a debe! .
RC ni kama rais, haiwezekani rais anaongea halafu wewe unaamka kumkatiza!.

Managing Diversity katika political arena ni muhimu sana haswa kwenye maeneo yaliyoshikwa na upinzani, watendaji wa serikali lazima watenganishe nafasi zao za kiutendaji kwa umma na ukada wao wa chama cha Mapinduzi, kazi yao ni kuwatumikia wananchi wote hata kama wananchi hao waliikataa CCM, wakifanya shughuli yoyote lazima watambue uwepo wa wawakilishi halali wa wananchi hata kama hawawapendi ndilo chaguo la watu.

Managing Diversity ni somo la namna ya kuutawala u tofauti wetu katika kufikia lengo moja la kuleta maendeleo. Utofauti huo unaweza kuwa wa kijinsia, kabila, dini, rangi, kisiasa, kiuchumi, kijamii watu wote tuko tofauti lakini bado sisi wote ni wamoja.

Hawa viongozi wa awamu ya tano wanahitaji semina elekezi kuwafunda mipaka yao, wakiendelea kuachwa hivi hivi, hawa viongozi wapendwa watazidi kujiinua na kujiona na wao ni vi mungu watu kwenye maeneo yao, na utafikia kiwango, watajiinua hata kumpita mungu wao!.
Paskali
 
Wanabodi,
Kwa kilichotokea leo Arusha, Watendaji wa serikali wanahitaji kupigwa msasa wa somo linaloitwa "Managing Diversity " ila wapinzani nao waache bangi zao! .

Kiukweli kabisa nina mashaka na IQ ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, ila bangi za Mbunge wa Arusha, Mhe. Godbless Lema zinaeleweka.

Gambo anajisikia ni mungu mtu, mtu mwenye akili timamu, hawezi kuacha kumtaja mbunge wa eneo husika hata kama humpendi vipi, Magufuli huyu Gambo hakufai! ; ila Lema nae zile ni bangi, kwa kutokutajwa tuu, you would lose nothing kwa kuwa calm! .
Pasco
mh Raisi huyo Gambo ni tatizo kwa heshima nataazima muondoe kabla ya kukutia aibu ya mwaka.Na amewaangusha vijana ,tulilia madaraka tukapewa huu ndo utendaji wetu?
 
Sijaona tatizo la Lema alichokitaka ni recognition tu na he deserve it. Tatizo Gambo anaona kama akimtambuwa lema atakuwa amejishusha sana.huu ni upumbavu wa kiwango cha degree. Magufuli usitegemee watendaji aina ya Gambo wanaweza kukusaidia katika kuleta maendeleo . Ni wazi hata wafadhili wametushangaa sana kwenye eneo la tukio busara imeshindwa kutumika. Mrisho Gambo ameniboa sana leo. Watu wametoa fedha zao mnakuja kujibizana hadharani.nadhani Rais utachukua hatua kwa hili lililotokea leo . Muhamishe huu Mkoa kama unampenda sana huyu Gambo. Watu tunataka maendeleo na si malumbano.
 
Ndo ujue bangi ni nzuri mana zimemsaidia Lema kujitahidi kadri ya uwezo wake mpaka Mradi huo umekamirika, kuliko Rais kuchagua madeiwaka wanamuaibisha leo mbele ya wahisani..nitaendelea kusema kuwa kuna watu Uongozi hauwapendi ila wao uongozi wanaupenda
 
Hiyo tabia ya Gambo ameitoa kwa aliyemteua, au umesahau ya Kinondoni Biafra na mwezi uliopita pale Magomeni Quarters?
Pale Biafra Meya wa Kinondoni alitengwa na mtakatifu akamkejeli tu, pale Magomeni meya huyo huyo tena akatengwa kiitifaki jukwaani.
Hivyo basi kilio chako Pasco ni sawa tu na kesi ya nyani kumepelekea ngedere.
 
Acheni kupepesa macho alichokifanya Guuumbo ni kukosa busara kwani angepungukiwa nn kumtaja Lema ila sishangai maana yawezakuwa alikuwa akitekeleza maagizo ya wakuu wake,ila namshauri kabla ya kufanyia kazi maelekezo anayopewa ayapime Kwanzaa mengine yanachafua picha ya taifa.
 
Amejenga yeye au ametafuta ardhi? Siasa zitawaua!! Unaweza kuta hana kitu yule. Kama alikuwa na umuhimu kama anaotaka angealikwa yeye. Kwani hawakujua?
Watu wengine mnaongea kama mmekunywa chimpumu. Hivi mkuu wa mkoa kiitifaki akimtaja Lema katika uzinduaji huo kuna ubaya? achilia mbali kwamba yeye ndo kaitafuta ardhi na wafadhili watakaoijenga hospitali hii.
 
Inauma sana, nimejaribu kijivisha viatu vya lema nkajua leo ningerusha ngumi!
Lema kaongea kwa uchungu kama amehangaika usiku na mchana kwa ajili ya mradi ule....
 
Gambo na yule aliyemteua hawana tofauti sana. Alichokifanya Gambo pale Arusha ni sawa sawa na kile alichokifanya "mtukufu" kwenye msiba wa Masaburi. Ni kuvuruga tu.

Ukiwa Kiongozi nyimwa vyote lakini usinyimwe Busara.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom