Rais Magufuli, somo la managing diversity kwa Serikali yako linahitajika

No hiyo inaitwa the biggest charity, begins at home, japo ni mtu mwenye upendeleo wa ajabu ambaye anayeweza kuwapa sumu watoto wa jirani wafe ili mwanae ndie abakie lakini kwenye hili la cheo cha Jaji Wambali sio kwa sababu ya kesi ya Kafulila, Jaji Wambali ni very deserving kwa post hiyo.

Paskali

Hahahahhahaha Shemeji baada ya ule uamuzi hata mpwa wako anajua ulikuwa wa kijinga ah basi Shemeji,tumezoea kwa wasukuma huwezi kumbishia Baba Mwenye nyumba
 
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amemtaka Rais Magufuli kuleta maridhiano ya kitaifa na kwamba yeye na chama chake wamenyoosha mkono wa mapatano

Ifuatayo ni Hotuba Fupi ya Kiongozi Mkuu wa Upinzani nchini Tanzania Freeman Aikael Mbowe mbele ya Watanzania katika kuadhimisha miaka 58 ya Uhuru:

Mheshimiwa Rais,
Waheshimiwa viongozi wote mlioko mahali hapa,
Waheshimiwa watanzania wenzangu!

Nimekuja kushiriki sherehe za miaka 58 ya Uhuru kama uthibitisho wa ulazima wa kuwepo maridhiano, kuwepo upendo, na kuwepo mshikamano katika Taifa letu.

Nawapongeza sana watanzania kwa siku hii ya leo na ninamuomba Mwenyezi Mungu siku ya leo ikafungue milango tuweze kuishi kama Taifa linalopendana, tuvumiliane, tukosoane, turuhusu demokrasia. Tukajenge Taifa lenye upendo na mshikamano.

Na Mheshimiwa Rais una nafasi ya kipekee kuweka historia ya maridhiano katika Taifa kwani kuna wengine wanalalamika, wengine wanaumia. Basi Mheshimiwa Rais tumia nafasi hiyo ukaliweke Taifa katika hali ya utengamano.

Nakushukuri sana. Asante sana.
_____________
Hotuba fupi ya Mwenyekiti wa CHADEMA na KUB, Mh *Freeman Mbowe* katika sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika, zilizofanyika Jijini Mwanza leo 9 Disemba 2019
View attachment 1286525
Hiki Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alichokiomba kwa rais Magufuli, ndio kitu hiki hiki akina sisi tulichoshauri hapa.

Kwa vile sasa amekishauri KUB, kitazingatiwa zaidi.

P.
 
Managing Diversity ni somo la namna ya kuutawala u tofauti wetu katika kufikia lengo moja la kuleta maendeleo. Utofauti huo unaweza kuwa wa kijinsia, kabila, dini, rangi, kisiasa, kiuchumi, kijamii watu wote tuko tofauti lakini bado sisi wote ni wamoja.
Sidhani kama hili somo limeshawaingia hao uliowataja Paschal
 
UTEUZI WA RC ARUSHA NA DC ARUSHA WATENGULIA

Rais Magufuli, leo ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Idd Kimanta

Pia ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro na nafasi yake imechukuliwa na Kenan Kihongosi wa UVCCM Iringa

Aidha, ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dkt. Maulid Madeni na kumteua Dkt. John Pima kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri

#JFLeo #Magufuli
View attachment 1483586

Soma pia:

1) Arusha: RC Gambo aibua sintofahamu Soko la Samunge, abeza taarifa ya DC na Mkurugenzi

2) Nini tatizo la RC Mrisho Gambo na wasaidizi wake?

3) Ugomvi baina ya RC Gambo na Mkurugenzi wa Jiji Arusha lashika kasi

4) RC Gambo aumbuka vijana wa CCM Arusha wamshambulia mitandaoni, aamua “ku left “

5) Ntibenda: Kama kuondolewa kwangu kama RC Arusha kuna mkono wa mtu; Mungu atalipa
Duh...!.
Kuna kitu niliwahi kushauri kumhusu Mrisho Gambo.
Rais Magufuli, somo la managing diversity kwa Serikali yako linahitajika
P
 
Duh...!.
Kuna kitu niliwahi kushauri kumhusu Mrisho Gambo.
Rais Magufuli, somo la managing diversity kwa Serikali yako linahitajika
P
Rais Magufuli ni mtu muungwana sana. Kuna watu huwa anawavumilia na kuwapa nafasi ya "kuzingatia moyoni" ili warejee kwenye msitari; ila baada ya muda wakishindwa huwa wanaondolewa.

Gambo kwa umri bado ni kijana sana. Alianguka kama DC wakati wa JK, baadae akakumbukwa. Ilimpasa kuwa na staha na unyenyekevu hasa anapo-deal na subordinates wake (DC na DED) mbele ya public na pia anaposhughulika na masuala ya kijamii ambapo mbunge wa Arusha anahusika.

Anyway, labda anaweza kujifunza kwa mara nyingine.

Somo hili la ku-manage diversity kuna baadhi ya ma-DC na Ma-RC vijana wanajukumu la kujifunza pia ili yaliyomkuta Gambo yasiwakute.

Kila la kheri wateuliwa, na poleni mliotumbuliwa. Cheo hubaki dhamana ya mwenye mamlaka ya uteuzi.
 
Wanabodi,

Kwa kilichotokea leo Arusha, Watendaji wa serikali wanahitaji kupigwa msasa wa somo linaloitwa "Managing Diversity " ila wapinzani nao waache mambo yao! .

Kiukweli kabisa nina mashaka na IQ ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, ila tabia za Mbunge wa Arusha, Mhe. Godbless Lema zinaeleweka.

Gambo anajisikia sana na kujiona kama ni mungu mtu, na hata akiongea, kuna wakati anaongea huku anabetua mdomo!, mtu mwenye cheo cha Mkuu wa Mkoa hawezi kuacha kumtaja mbunge wa eneo husika hata kama humpendi vipi!.

Mhe. rais Dr. JohnPombe Joseph Magufuli huyu RC wako wa Arusha, Mrisho Gambo ni janga!, japo anaweza kuwa ni swahiba wako sana, lakini kiukweli hakufai kabisa!, huwe kum ignore mchaguliwa wa wananchi mbele wa wapiga kura wake!. Ila pia huyu Mbunge wa Arusha, Mhe. Godbless Lema nae ni majanga!, kichwani hajatulia kabisa, zile ni fujo alizoanzisha pale, kisa ni kwa kutokutajwa tuu, ni kukosa uvumilivu, subra na ustahimilivu, Arusha ni ngome yake, wananchi wa Arusha wanaojua, hilo donge la mteule wa rais kutokumtaja kwa makusudi hakukupaswa kumuingilia kati, Lema would lose nothing kwa kuwa calm na ku keep cool mpaka Mkuu wa Mkoa amalize kuongea, you never know, kama Lema angetulia kimya, mwisho wa siku Mkuu wa Mkoa angemtaja tuu wakati wa Shukrani, Lema alifanya papara kuingilia kati.

Wateule wote wa serikali wanapaswa kufahamu kuwa serikali yoyote iliyopo madarakani inapata legitimacy from the people, hivyo viongozi hao ni lazima waheshimu wishes of the people hata kama hukubaliani na chaguo la wananchi kuipiga chini CCM na kuichagua Chadema, hata kama Mrisho Gambo humpendi vipi Godbless Lema, kwenye official public events ambazo Mbunge has a role, ni lazima amtaje Lema apende asipende kwa sababu Lema ndie mwakilishi wao.

Mbunge ndiye mwakilishi halali wa wananchi wale na RC ni mteuliwa tuu, hivyo lazima aheshimu the wishes of the people.

Viongozi wa upinzani nao, lazima wajifunze kuheshimu na kutii mamlaka za nchi, Mkuu wa Mkoa ndio mamlaka kuu mkoani hapo, wakati mamlaka inaongea, hakuna mtu mwwingine yoyote mwenye right ya kuingilia na kuikatiza mamlaka. Jana pale kiukweli kabisa Gambo amemuheshimu sana Lema kwa kumvumilia, ningekuwa ni mimi jana pale Lema angekwenda tena kun..a debe! .
RC ni kama rais, haiwezekani rais anaongea halafu wewe unaamka kumkatiza!.

Managing Diversity katika political arena ni muhimu sana haswa kwenye maeneo yaliyoshikwa na upinzani, watendaji wa serikali lazima watenganishe nafasi zao za kiutendaji kwa umma na ukada wao wa chama cha Mapinduzi, kazi yao ni kuwatumikia wananchi wote hata kama wananchi hao waliikataa CCM, wakifanya shughuli yoyote lazima watambue uwepo wa wawakilishi halali wa wananchi hata kama hawawapendi ndilo chaguo la watu.

Managing Diversity ni somo la namna ya kuutawala u tofauti wetu katika kufikia lengo moja la kuleta maendeleo. Utofauti huo unaweza kuwa wa kijinsia, kabila, dini, rangi, kisiasa, kiuchumi, kijamii watu wote tuko tofauti lakini bado sisi wote ni wamoja.

Hawa viongozi wa awamu ya tano wanahitaji semina elekezi kuwafunda mipaka yao, wakiendelea kuachwa hivi hivi, hawa viongozi wapendwa watazidi kujiinua na kujiona na wao ni vi mungu watu kwenye maeneo yao, na utafikia kiwango, watajiinua hata kumpita mungu wao!.
Paskali
Haha yametimia
 
Tulishauri sana kwa Warioba kuwa nafasi hizi zifutwe au zipate legitimate ya kura za wananchi kwani bila hivyo mkoa au wilaya inakuwa empire ya mtu kwenda anavyotaka kusahau umoja wa kitaifa na maslahi ya watu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom