Rais Magufuli ruhusu ajira sasa

OPERATION ENTEBBE

Senior Member
Feb 13, 2017
120
74
Rais Magufuli ruhusu ajira kwa vijana

Tu naingia mwaka wa pili sasa, Rais yuko kimya kuhusu AJIRA, as if hakuahidi, wizara husika nayo haina kazi ipo ipo tu na wimbo wa uhakiki mwaka wa pili hhuu

Mbaya zaidi Magufuli amekuwa ndio kila kitu, Wizara zinahitaji vijana wajiriwe lakini wanamtizama Magufuli

Magufuli toa ajira sasa kwa vijana, Tafadhali mlioko mawazirani huko mushaurini aajiri vijana wana angamia na wanaanza kukimbia nchi sasa
 
Anza kufanya hata kazi za kujipatiaa ujuzi bila malipo au biashara, muda ukifika wa kuitwa utaitwa kama. Kama hautaitwa utakuwa na mengi umejijengea, unaweza kukuta kama mtu hauna kazi sasa hivi ukaanza hata kilimo, ukija kuitwa kazini utawakimbia wewe.

Mengi yapo ya kufanya kuliko kukaa miaka 2 unasubiri kazi ambayo unaweza hata usipate nafasi.

Hata mashirika ya binafsi etc yapo

Muangalie nje ya boksi, maisha ni yenu. Kuliko kukaa kusubiri kama unasubiri basi fanya kitu, kila kitu kinajenga ujuzi hata kuuza kitu kidogo.
 
Mkuu samahani hivi ccm wanakulipa?
Mana umekuwa kipofu kabisa hata mambo ambayo yako wazi kabisa unatetea, sio sawa kabisa
Hali ilivyo sasa hata hizo nafasi za kujitolea hakuna na kama zipo unaweza kuta huwezi hata mudu gharama za usafiri
Panastahili pongezi pongeza na panapostahili kukosolewa Fanya hivyo,mapenzi yasikutie upofu kwa hili serikali imechemshaa
 
Kila kitu kimemshinda, nimesitishiwa ajira yangu mwaka sasa, hakuna chochote anachokifanya, hata watendaji wanaogopa kutoa mwongozo wa nn kifanyike kwa ajira mpya
 
Kujiajiri ni wito! Hasa kwa mtoto wa kiume..
kujiajiri mtaji unatoa wapi kama ni fresh from school? afu ukute nyumbani wamekusomesha ili nawe uje uwasaidie.

wakati tunaambiwa tujiajiri basi mtupatiage na mitaji.
 
Back
Top Bottom