Rais Magufuli: Rais Kenyatta alinipigia simu, tulizungumzia mgogoro uliopo mipakani

MOTOCHINI

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
27,580
30,025
Rais John pombe Magufuli leo amesema Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta alimpigia simu na kumpa pole

Pia Rais Magufuli amesema kuwa wamezungumzia mgogoro ulipo mipakani mwa nchi hizi mbili na kuamua mawaziri wa pande zote mbili wanaohusika na Uchukuzi kukutana.

---

Kenyatta alinipigia simu nikiwa Chato. Leo pia kanipigia tumezungumza pia. Tumezungumza kama migogoro kule mipakani. Kenya ni marafiki zetu. Tumekubaliana mawaziri wetu wa uchukuzi na wakuu wa Mikoa watakutana mpakani na Kenya wazungumze hili walimalize.

Hii korona isiwe chanzo cha migogoro. Haiwezekani kila dereva anayekwenda huko awe na korona. Nawaomba viongozi wa mikoa inayopakana na Kenya wasitatue matatizo yao kwa jazba. Wazingatie uchumi wa nchi zetu.

Ninafahamu mtu ukichokozwa kidogo ukanyamaza, na wewe unachokoza kidogo. Nataka Wakenya na Watanzania wafanye biashara vizuri”

Naomba, na kwakuwa tumezungumza vizuri na Mheshimiwa Kenyatta, sisi tumeyamaliza.

Haiwezekani mtu anasafiri anaenda nchi jirani anaambiwa akae mpaka sijui siku ngapi wakati amepakia bidhaa

Korona haikuwanzia Afrika. Na imewakoromea wote hata wale wenye uwezo.
 
Njaa mwana malewa, nadhani kile chakula cha Ethiopia na Uganda cha kuziba "NGAP" ya chakula cha Tanzania hakikuwepo kama kilivyotarajiwa!

Imebidi Mtu mzima aseme poo! Hana jinsi imembidi Uhuru achutame kujisitiri baada ya kuambiwa yupo uchi kwa maana Wahenga walisema "mtu mzima akivuliwa nguo....huchutama"

#Akilizahandshake#

CC: Zigi Rizla Kafrican Depay Yosef Festo Teargass Tony254 pingli-nywee komora096 Edward Wanjala
kikihboy nomasana, sam999, NairobiWalker, hbuyosh, msemakweli, simplemind, Kimweri, Bulldog, MK254, Kafrican, Ngongo, Ab_Titchaz, mtanganyika mpya, JokaKuu, Ngongo, Askari Kanzu, Dhuks, Yule-Msee, waltham, Mzee, mombasite gabriel, Juakali1980, Boda254, mwaswast, MwendaOmo, Iconoclastes, oneflash, Kambalanick, 1 Africa, saadeque, burukenge, nyangau mkenya, Teen-Upperhill Nairobi, kadoda11
 
Kenyata wakati anatangaza kufunga mipaka alikuwa sober sana
Rais John pombe Magufuli leo amesema Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta alimpigia simu na kumpa pole

Pia Rais Magufuli amesema kuwa wamezungumzia mgogoro ulipo mipakani mwa nchi hizi mbili na kuamua mawaziri wa pande zote mbili wanaohusika na Uchukuzi kukutana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona wamechemsha,mapema hivyo?
Kwani walipoamua kufunga mpaka wao walimpigia nani simu?
Wasitichezee tupo bize na uchaguzi,wasubiri hadi uchaguzi upite ndipo tuwafikirie ombi lao
 
Rais John pombe Magufuli leo amesema Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta alimpigia simu na kumpa pole

Pia Rais Magufuli amesema kuwa wamezungumzia mgogoro ulipo mipakani mwa nchi hizi mbili na kuamua mawaziri wa pande zote mbili wanaohusika na Uchukuzi kukutana.
Wewe bado upo lumumba tu? Rudi kwenu ukatengeneze kayoga

In God we Trust
 
Back
Top Bottom