Rais Magufuli: Nitahamia Dodoma mwaka huu, 2018

Rais Magufuli: Nitahamia Dodoma mwaka huu, 2018

Mh rais, napenda kukumbusha tu kwamba uliahidi kuhamia Dodoma rasmi kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Napenda kukukumbusha kwamba bado tunaikumbuka ahadi yako na tunategemea kukuona ukihamia Dodoma mwaka huu kama ulivyoahidi.

Hata hivyo huku mwaka ukielekea ukingoni hatuoni dalili wala amsha amsha ya maandalizi ya wewe kuhamia Dodoma. Ifahamike kwamba hili ni jambo kubwa sana na la kihistoria. Hivyo tungetegemea katika muda huu mfupi uliobakia tuone maandalizi kabambe. Mfano, hali ya Ikulu ya Dodoma na utayari wake wa kukupokea na mambo mengine kede wa kede.

Kinyume chake kuna ukimya usiokuwa wa kawaida. Sio mkuu wa mkoa wa Dodoma wala mamlaka nyingine zinazohusika zinazohusika wanaonekana kuwa excited na ujio wako Dodoma ndani ya miezi hii miwili.

Pamoja na hayo, ni muhimu sana mh rais uhamie Dodoma haraka kama ulivyoahidi ili kuweza kuokoa kiasi kikubwa cha fedha kinachopotea sasa kwa viongozi wengi kulazimika kurudi Dar kila mara ili kukuunga mkono katika shugjuki unazofanya huku Dar. Mara nyingi makamu wa rais yupo Dar, waziri mkuu yupo Dar( leo yupo anakagua ujenzi wa madaraja ya tazara na ubungo), wakuuu wa majeshi, na viongozi wengi waandimizi serikalini wanalazimika kuwa na route za Dar- Dom kila mara. Yote haya yanatumia pesa nyingi za watanzania bula sababu.

Tafadhali mh kama tumeamua kuhamia Dodoma basi tufanye kweli tukae Dodoma. Ksma bado Dar kutamu nanatamani kuwepo muda wote basi iwe wazi kwamba serikali itakuwa na makao makuu Dar na Dodoma simultaneously. Hapa tutawaelewa.

Tafadhali oneeni huruma kodi zetu, wananchi tunaumia.
 
Mawazo yangu, sababu za Dom kuwa makao makuu eti IPO kati,urahisi kufika,hazina mashiko kwa dunia ya sasa ya Technologia. Bahari pekee,kipupwe,historia kinainapa Dar,heshima kubwa.Upepo wa dhiki wa Dodoma,haikuwa haki kuwasukumiza watendaji wetu wa serikali! Sina uhakika balozi ngapi wataweka makazi ya kudumu mbali ya ofisi ndogo!Bajeti hiyo tungeweza maliza kabisa zahanati,hospitali za wilaya na madarasa nchi nzima!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahamie tu huku town ya mzizima kusiwepo mifoleni mchundo!!
 
Hata mwinyi alihamia lakin alikaa mwaka mmoja akamiss maji ya bahari na pweza akarudi
 
Hili
Mawazo yangu, sababu za Dom kuwa makao makuu eti IPO kati,urahisi kufika,hazina mashiko kwa dunia ya sasa ya Technologia. Bahari pekee,kipupwe,historia kinainapa Dar,heshima kubwa.Upepo wa dhiki wa Dodoma,haikuwa haki kuwasukumiza watendaji wetu wa serikali! Sina uhakika balozi ngapi wataweka makazi ya kudumu mbali ya ofisi ndogo!Bajeti hiyo tungeweza maliza kabisa zahanati,hospitali za wilaya na madarasa nchi nzima! Hil

Sent using Jamii Forums mobile app
Hili la kuhamia Dom sijawahi kulielewa lengo na mantiki yake. Sioni hawa watu wakiishi Dom. N kudanganyana tu.
 
Rais Magufuli Kuhamia Dodoma Mwaka Huu






Rais John Magufuli amesema atahamia jijini Dododma kabla mwaka huu haujamalizika kama alivyoahidi serikali yake kuhamia huko.

Rais Magufuli amesema hayo wakati akizungumza katika hafla fupi ya kuwakabidhi hati za viwanja kwa mabalozi wa nchi mbalimbali na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Julai 30.

Amesema hadi sasa viongozi wengi wa serikali wameshahamia Dodoma akiwamo Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, mawaziri na viongozi mbalimbali wa kitaifa na kwamba Dar es Salaam amebaki yeye tu.

“Nimebaki mimi tu hapa. Nimepanga kabla mwaka huu haujamalizika nitahamia Dodoma, nilitaka nisihamie huko nikawaacha ndugu zangu wanaowakilisha nchi zao hapa Dar es Salaam, ndiyo mana nikahakikisha mnapata hati.

“Serikali imetoa maeneo mbalimbali jumla ya heka tano bure kwa ajili ya mabalozi, na ninyi ni mashahidi nimetoa hati hizi bila kudai chochote na mmepatiwa bila kusaini chochote, sijasema mhamie kesho, mtahamia wakati wowote mtakaotaka,” amesema Rais Magufuli.

Pamoja na mambo mengine, Rais Magufuli amesema, tayari viongozi wote na watumishi zaidi ya 6,000 wameshahamia hukoa ambapo pia amewatoa hofu mabalozi hao na wawakilishi wa kimataifa kuhusu usalama jijini humo.

“Tunaamini katika hatua tunazochukua mkihamia Dodoma itakuwa safi na kuhusu usalama tumehakikishiwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa.

“Dodoma ni mahali pazuri na ni rahisi kwenda nchi yoyote kwa kuanzia Dodoma. Tunaboresha huduma za usafiri ikiwamo miundombinu na afya kwa Dodoma na mikoa jirani ukiwamo Singida.

“Nimeagiza ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa msalato ili ndege zinazotua Dar es Salaam zitue Dodoma uanze kujengwa mara moja. Nataka niwahakikishie mabalozi Dodoma ni mahali pazuri nina uhakika patakuwa safi sana hasa baada ya ndege kutoka nchi zenu kutua hapa, tunataka kuitengeneza Tanzania mpya, yenye maendeleo na kushirikiana na sekta binafsi,” amesema.
MEMBE FOR PRESDENTIAL 2020
 
Mheshimiwa rais, nakukumbusha tu kwamba una siku nne tu zimebaki utimize ahadi yako ya kuhamia Dodoma. Tafadhali , usimsahau kipenzi chako Bashite. Nakushauri pia ukihamia Dodoma uhamie kwelikweli, sio kila leo kiguu na njia kurudi Dar. Sisi wananchi unaopenda kutuita wanyonge hatupo tayari kubeba gharama hizo. Labda mtumie mishahara yenu mkitaka kueudi Dar kujivinjari. Ni hayo tu Mh na Mrukufu sana Rais.
 
Mimi bado nasibiri kuona ikulu ya Dar ikifanywa jumba la makumbusho maana Rais aliahidi kabla ya kuisha mwaka huu atakuwa amehamia Dodoma na ile ikulu ya Dar kuipiga kufuli.

Zimebaki siku 3 tu tuufunge mwaka wa 2018.
 
31 December ndiyo inakaribia hiyo.
ahadi nyepesi kabisa kama hii isipotekelezwa, je vipi zile kubwa za viwanda, nk?
 
Back
Top Bottom