Rais Magufuli: Nitahamia Dodoma mwaka huu, 2018

Rais Magufuli: Nitahamia Dodoma mwaka huu, 2018

Anatala kuhama na bahari aende nayo Dodoma
Kwani bahari ndio kigezo cha kuwa mji mkuu? mbona hatutaki kuelewa. nchi ngapi duniani mpaka nchi kubwa miji mikuu haiko katika fukwe za bahari na miji imeendelea sana tu. lazima tutofautishe mji wa kibiashara na na mji wa kisiasa. Dar utabaki biashara na sio lazima mji mkuu. Europe ndio kabisa miji mingi mikuu sio baharini hata baadhi ya Africa. ingekuwa hivyo basi Newyork ungekuwa mji mkuu au LA maana ndio kwenye biashara na watu wengi.
 
Rais Magufuli Kuhamia Dodoma Mwaka Huu

Rais John Magufuli amesema atahamia jijini Dododma kabla mwaka huu haujamalizika kama alivyoahidi serikali yake kuhamia huko.

Rais Magufuli amesema hayo wakati akizungumza katika hafla fupi ya kuwakabidhi hati za viwanja kwa mabalozi wa nchi mbalimbali na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Julai 30.

Amesema hadi sasa viongozi wengi wa serikali wameshahamia Dodoma akiwamo Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, mawaziri na viongozi mbalimbali wa kitaifa na kwamba Dar es Salaam amebaki yeye tu.

“Nimebaki mimi tu hapa. Nimepanga kabla mwaka huu haujamalizika nitahamia Dodoma, nilitaka nisihamie huko nikawaacha ndugu zangu wanaowakilisha nchi zao hapa Dar es Salaam, ndiyo mana nikahakikisha mnapata hati.

“Serikali imetoa maeneo mbalimbali jumla ya heka tano bure kwa ajili ya mabalozi, na ninyi ni mashahidi nimetoa hati hizi bila kudai chochote na mmepatiwa bila kusaini chochote, sijasema mhamie kesho, mtahamia wakati wowote mtakaotaka,” amesema Rais Magufuli.

Pamoja na mambo mengine, Rais Magufuli amesema, tayari viongozi wote na watumishi zaidi ya 6,000 wameshahamia hukoa ambapo pia amewatoa hofu mabalozi hao na wawakilishi wa kimataifa kuhusu usalama jijini humo.

“Tunaamini katika hatua tunazochukua mkihamia Dodoma itakuwa safi na kuhusu usalama tumehakikishiwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa.

“Dodoma ni mahali pazuri na ni rahisi kwenda nchi yoyote kwa kuanzia Dodoma. Tunaboresha huduma za usafiri ikiwamo miundombinu na afya kwa Dodoma na mikoa jirani ukiwamo Singida.

“Nimeagiza ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa msalato ili ndege zinazotua Dar es Salaam zitue Dodoma uanze kujengwa mara moja. Nataka niwahakikishie mabalozi Dodoma ni mahali pazuri nina uhakika patakuwa safi sana hasa baada ya ndege kutoka nchi zenu kutua hapa, tunataka kuitengeneza Tanzania mpya, yenye maendeleo na kushirikiana na sekta binafsi,” amesema.
Bado siku mbili mwaka uishe
 
Naona mmeamua kumkumbusha kwamba zimebaki siku 3 tu kabla ya mwaka kuisha. Isijekua kasahau kutokana na majukumu ya hapa na pale.
 
Ndio mjue mlichagua LIYUDA LIWAONGOZE magufuli ni muongo aliepitiliza ana ahadi hewa kuliko zinazotekelezeka.
.
Na kama mmemfuatilia huyu baba ni mtu wa MAJIVUNO anamajivuno wakati uwezo sifuri.
.
Nimebahatika kuisoma ilani ya CCM nimegundua asilimia 60 ya anavyovifanya havitoki kwenye ilani ila anaangalia upepo unaendaje ili aendelee kutupiga.
.
NA KWA JINSI DODOMA ILIVYO NA WAJINGA WENGI KULIKO WEREVU SIKU AKIHAMIA WATAPIGWA POROJO WABAKI WAMEKENA.
 
Kwani bahari ndio kigezo cha kuwa mji mkuu? mbona hatutaki kuelewa. nchi ngapi duniani mpaka nchi kubwa miji mikuu haiko katika fukwe za bahari na miji imeendelea sana tu. lazima tutofautishe mji wa kibiashara na na mji wa kisiasa. Dar utabaki biashara na sio lazima mji mkuu. Europe ndio kabisa miji mingi mikuu sio baharini hata baadhi ya Africa. ingekuwa hivyo basi Newyork ungekuwa mji mkuu au LA maana ndio kwenye biashara na watu wengi.
Umeelewa nilichokimaanisha au umejibu kwa kutumia mihemuko?
 
Umeelewa nilichokimaanisha au umejibu kwa kutumia mihemuko?
Hapana hajatumia mihemuko. Alikuwa anajaribu kuelezea anavyovijua na sio kinachoongelewa. Hivi kweli kakuona wewe hata hujui kuwa kuna nchi zingine ni land locked na hivyo bahari is out of suala? Hapana anajua ila alitaka kutufahamisha anachokijua
 
Itakua hivyo mkuu maana, si rahisi mtu aweze kuhamisha bahari...
 
Serikali ya CCM chini ya rais Pombe Magufuli ilitamba Sana na kupiga kelele kwamba kabla mwaka haujaisha rais atakua keshahamia makao makuu ya nchi mjini Dodoma kuungana na Makamu wake na waziri mkuu

Cha ajabu mwaka umebakiza dakika kadhaa uishe zile kelele na mbwembwe za rais kuhamia Dodoma kabla mwaka 2018 haujaisha sijui zimepotelea wapi

Wafia Chama na wajuvi wengine wa hii safari ya Dodoma mnijuze mmefikia wapi.
 
Alisema 2019

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haendi popote ng'o ni muongo kama waongo wengine,kwanza yeye ndie mpigadili wa kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom