Rais Magufuli ni Mkweli Daima!. Jee Tumuunge Mkono Rais Wetu Katika Kila Ukweli Wake, Hata Kama Uko Kinyume cha Katiba, Sera na Ilani?.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,507
113,629
Wanabodi,

Leo nimepata tena fursa ya kuendelea na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa, mada ya leo ikiwa ni swali kuhusu, kunapotokea mkanganyiko kati ya ukweli wa rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, na ukweli halisi, au ikitokea ukweli wa rais Magufuli ukitofautiana na ukweli wa katiba, sheria, taratibu, kanuni, sera na Ilani ya uchaguzi ya CCM, jee ni ukweli upi ufuatwe katika utawala wa nchi yetu kati ya ukweli wa rais wetu, au ukweli wa katiba, sheria, taratibu, kanuni, sera na Ilani ya uchaguzi ya CCM

Moja ya sifa kuu na za pekee za rais Magufuli ni kuwa kuwa mkweli daima, sometimes, anakuwa mkweli too much mpaka anapitiliza, katika kuusema ukweli, rais Magufuli atausema ukweli wake no matter what, hata kama ukweli huo wake, sio ukweli halisi, au unapigana na katiba, sheria, taratibu, kanuni, sera na hata ilani ya uchaguzi ya CCM, as long as ni ukweli wake, rais Magufuli atausema tuu ukweli huo, bila kujali the consequences ya ukweli huo, na kuwaachia kigugumizi wasaidizi wake namna ya kuuweka sawa ukweli huo kama unakwenda kinyume cha sera na ilani, ila unapokwenda kinyume cha katiba, uzoefu wangu umeonyesha, huwa wananyamaza tuu!.

Hili ni bandiko la hojaji kuhusu Watanzania kumuunga mkono rais wetu katika kufuata ukweli huu wa rais wetu, kwa vile Rais Magufuli ni Mkweli Daima!. Jee Tumuunge Mkono Rais Wetu Katika Kila Ukweli wake, Hata Kama Ukweli Huo unakwenda Kinyume cha Katiba, sheria, taratibu, kanuni, Sera na Ilani ya uchaguzi ya CCM?. Katika kumuunga mkono rais wetu katika ukweli wake, jee sasa nchi yetu iendeshwe kwa ukweli wa rais wetu, au tuendelee kuiendesha nchi yetu kwa mujibu wa Katiba, sheria, taratibu, kanuni, Sera na Ilani ya uchaguzi ya CCM?.
Hitimisho.
Inapotokea rais akatoa msimamo wake binafsi ambao ndio ukweli wake, na ukaenda kinyume na ukweli halisi, au kinyume cha katiba, sheria, taratibu, kanuni, sera na Ilani ya uchaguzi ya CCM, jee Watendaji wa serikali yetu tukufu, watatekekeza nini kati ya ukweli wa rais , au ukweli halisi, na kwenye ukweli wa rais unaokwenda kinyume cha katiba, sheria, taratibu, kanuni, sera na Ilani ya uchaguzi ya CCM, watendaji wa serikali, watekeleze ukweli upi?.

My Take
Hili la mtu kusema chochote, popote, as long as ni ukweli, mimi naliunga mkono, maana kila mmoja wetu, akiwa ni mkweli wa aina hii na kusema chochote, popote, its healthy, maana you never know, katika hii ongea ongea, kuna siku hata waliohusika na matukio kama ya kina Lissu, watakuja kuropoka, na ukweli utajulikana!.

Wasalaam.
Jumatano Njema.
Paskali
 
We jamaaa mwanzoni ulikuwa mwandishi haswaa lakini now days sijui umepatwa na nini??
 
Comments Reserved ''Mkubwa hajambi''
 
Katika maisha yangu sijawahi kumwamini mwanasiasa
 
Hivi huyu mtu inamaana anatakiwa kuungwa mkono yeye tu amekua nani haswa? Saa zingine mawazo tofauti ni bora zaidi maana tangu waanze kuumunga mkono sijaona tija yoyote ile haswa ukizingatia huyu mtu ni mvunjaji wa sheria namba moja katiba namba mbili, utu namba tatu roho mbaya namba 4 daah
 
Kwa kutaka tutoa elimu nzuri, nazani ilipaswa kuanza na sera ya uzazi hapo kwanza.

Pili, Mimi nafikiri magufuli katoa kauli hili kwa mtaji wa kisiasa ndani ya ccm, kwasababu mkuu moja takwimu inaeleza kuwa watanzania Tupo million 50.

Kwenye idadi hivyo inasemeka wakatoliki wapo mbioni kuzidiwa na waslimu Kwasababu wakatoliki ndio wanaofata uzazi wa mpango.

Pia nilazima tuwe wakweli tu kuwa waslimu bado hawana elimu sana so kwenye hili ccm wameona kuwa tatizo Kwasababu taifa litamuliwa na upinzani wa kweli.

Natamka Hivi Kwasababu waslimu ni wakweli katika maamuzi.

mr mkiki
 
Kuna siku atakuelewa kama vile umecheza biko
 
Paskali ila moyoni unajua ukweli ni upi.. bunge limekuweza kweli na unawapatia kisawa sawa.. anza kusifia kila kitu hadi kikomba anachonywea chai.. tupo nyuma yako

Sometimes huwaga nawazaga huyu mzee angepoteaga kama Ben Saanane

Tatizo mnapenda kusifiana tuuuu na kuungana tuuuu. Ila ntamusifia siku Tanzania ikiwa donor country, siku na sisi tugawe misaada, tupeleke mitumba ulaya, tuwe matajiri naingoja hiyo siku walah

Ila hizi porojo nyingine za Paschal Njaa ni useless na upumbavu
 
Ukweli wa Magufuli unàwatesa sana wanasiasa makanjanja kama Lisu na Zitto
unamwita zitto kanjanja? hujui hata sheria ya takwimu mmeibadilisha kwa ajili yake? unamwita lisu kanjanja? kwann mlitaka kumuua kanjanja? wewe upo shallow kichwani huwezi jua hawa watu wanajadili nini. nakushauri uweke nyimbo za komba uanze kunengua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…