Rais Magufuli na wageni mashuhuri duniani

Rais Magufuli na wageni mashuhuri duniani

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
13,185
Reaction score
24,055
Kwa hali ilivyo nchini inakuwaje unapata hawa wageni ambao wengine wana madaraka kimataifa huku wengine wakiwa ni matajiri wakubwa duniani.

Sisi ‘’tunataka/tunapenda’’ Tanzania iwe ‘’the skunk of the world’’ halafu wewe unatujibu kwa kupokea kwa siku moja hapo Ikulu ugeni wa watu watatu ambao ni mover and shaker hapa duniani;

1) Katibu Mkuu wa Nchi za Jumuiya ya Madola, Rt Hon Patricia Scotland QC.

2) Naibu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Inmi Patterson

3) Tajiri namba moja duniani, Bill Gates.

Hivi hawa wageni wako hawajui kuwa Tanzania hakuna ‘’Freedom of Speech’’?

Hivi hawa wageni hawajui kama wewe ni ‘’Dikteta Uchwara’’?

Hivi hawa wageni hawajui kuwa ACACIA imezuiwa kusafirisha ‘’mchanga wake’’ wenye makanikia nje ya nchi na kwa misingi hiyo ''amevunja sheria'' za biashara kitaifa na kimataifa? Kwa nini wanakuja kuwekeza pesa zao kwenye utawala ambao hauheshimi Katiba na Sheria?

Ina maana sisi ''tunaopiga kelele'' hawatusikii au wanasikia na kutuona wajinga?

Kwa nini mnatufanyia ‘’vituko’’ vya aina hii?

Rais Magufuli acha Usanii wa kisiasa!

Hata wananchi wa Tanga walipovamia gari yako ili usimame ''tulisema'' ni usanii!

VIDEO: Katibu Mkuu wa Nchi za Jumuiya ya Madola, Rt Hon Patricia Scotland QC alipokutana na Rais Magufuli Ikulu Dar es Salaam.

VIDEO: Naibu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Inmi Patterson alipokutana na Rais Magufuli Ikulu Dar es Salaam.

VIDEO: Bill Gates alipokutana na Rais Magufuli Ikulu Dar es Salaam.
 
Moja ya sababu ya Tanzania kuwa masikini ni pamoja na "laana" ya kuwa na "uchafu" badala ya "mtoto" . Mauchafu yanaliangamiza hili Taifa. Ni mpaka pale "mauchafu" yatakapotoweka na kuhakikisha hakuna tena kuletwa "uchafu" ndipo tutakuwa salama. Polee
 
Mmh..... Sijui kama huu uzi utadumu......

Kwa kuwa Mkulu hayuko tayari kukosolewa, bali anatakaga siku zote aimbiwe "mapambio" ya kusifiwa tu......

[HASHTAG]#hatunyamazi[/HASHTAG]
 
Sikudhani kuwa msemaji ukweli waweza kuwa na akili za kiwango cha chini kiasi hicho. Wewe unadhani ajapo mgeni Tanzania huwa ni mgeni wa mkulu binafsi au nchi? Bill Gates kaja Tanzania sio kwa sababu Magu ni Rais bali kafuatilia miradi ya foundation yake na ilianza siku nyingi kabla hata huyo mtu wako hajawa na ndoto ya kuwa siku moja watu watakosea na kumpa heshima hiyo.

Hao wengine ni program za kazi zinazowaleta bila kujali ni nani yupo hapo, hata Amin alikuwa anapokea wageni ofisini kwake waliokuwa wanaenda kwa program za kikazi.

Maelezo yako labda ungesema safari kama ile ya Raila kule kwake na kulala siku tatu ndiyo hayo maswali ungeuliza. Pale katembelewa yeye binafsi na sio nchi, Leo hii hata yeye angekuwa yuko Likizo huko kwao bado Bill Gates angeonana na Mama Samia.
Acha kupotosha watu kwa ushabiki maandazi
 
kuja hao wageni wakubwa duniani ni pigo kwetu sisi ba-vichaa , tulitamani watususe tupate cha kuongea na kupost

Sent using Jamii Forums mobile app
Lakini Mkuu hebu tupe feedback za zile trillion 418 zetu za acacia ambazo zingetuwezesha kila mtanzania kuweza kumiliki Noah yake....

Mbona kimya kimezidi kupita kiasi, je majadiliano yamekamilika au "wanaume" weshaenda kwao Canada kimya kimya?
 
Kwa hali ilivyo nchini inakuwaje unapata hawa wageni ambao wengine wana madaraka kimataifa huku wengine wakiwa ni matajiri wakubwa duniani.

Sisi ‘’tunataka/tunapenda’’ Tanzania iwe ‘’the skunk of the world’’ halafu wewe unatujibu kwa kupokea kwa siku moja hapo Ikulu ugeni wa;

1) Katibu Mkuu wa Nchi za Jumuiya ya Madola, Rt Hon Patricia Scotland QC.

2) Naibu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Inmi Patterson

3) Tajiri namba moja duniani, Bill Gates.

Hivi hawa wageni wako hawajui kuwa Tanzania hakuna ‘’Freedom of Speech’’?

Hivi hawa wageni hawajui kama wewe ni ‘’Dikteta Uchwara’’?

Hivi hawa wageni hawajui kuwa ACACIA imezuiwa kusafirisha ‘’mchanga wake’’ wenye makanikia nje ya nchi na kwa misingi hiyo umevunja sheria za biashara kitaifa na kimataifa? Kwa nini wanakuja kuwekeza pesa zao kwenye utawala ambao hauheshimi Katiba na Sheria?

Ina maana sisi ''tunaopiga kelele'' hawatusikii au wanasikia na kutuona wajinga?

Kwa nini mnatufanyia ‘’vituko’’ vya aina hii?

Rais Magufuli acha Usanii wa kisiasa!

VIDEO: Katibu Mkuu wa Nchi za Jumuiya ya Madola, Rt Hon Patricia Scotland QC alipokutana na Rais Magufuli Ikulu Dar es Salaam.

VIDEO: Naibu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Inmi Patterson alipokutana na Rais Magufuli Ikulu Dar es Salaam.

VIDEO: Bill Gates alipokutana na Rais Magufuli Ikulu Dar es Salaam.

Duuuh,eti hayo unaona maajabu,no wonder anawaita baadhi yenu ni wapumbav!
 
Wanaosema hayo yote ni wapinzani uchwara wa nchi hii.
Itabidi kuwe ma oparesheni ya kuzirudisha akili za wanachadema mahali pake, maana waliozichukua wameziacha bila kuziendeleza.
Ila mkuu amesema wanalumumba wenzake ni wapumbav!!
 
Sikudhani kuwa msemaji ukweli waweza kuwa na akili za kiwango cha chini kiasi hicho. Wewe unadhani ajapo mgeni Tanzania huwa ni mgeni wa mkulu binafsi au nchi? Bill Gates kaja Tanzania sio kwa sababu Magu ni Rais bali kafuatilia miradi ya foundation yake na ilianza siku nyingi kabla hata huyo mtu wako hajawa na ndoto ya kuwa siku moja watu watakosea na kumpa heshima hiyo.
Hao wengine ni program za kazi zinazowaleta bila kujali ni nani yupo hapo, hata Amin alikuwa anapokea wageni ofisini kwake waliokuwa wanaenda kwa program za kikazi. Maelezo yako labda ungesema safari kama ile ya Raila kule kwake na kulala siku tatu ndiyo hayo maswali ungeuliza. Pale katembelewa yeye binafsi na sio nchi, Leo hii hata yeye angekuwa yuko Likizo huko kwao bado Bill Gates angeonana na Mama Samia.
Acha kupotosha watu kwa ushabiki maandazi
Amejitoa ufahamu,yaani ameona hilo ni jambo kubwa na la ajabu!!
 
Back
Top Bottom