Sikudhani kuwa
msemaji ukweli waweza kuwa na akili za kiwango cha chini kiasi hicho. Wewe unadhani ajapo mgeni Tanzania huwa ni mgeni wa mkulu binafsi au nchi? Bill Gates kaja Tanzania sio kwa sababu Magu ni Rais bali kafuatilia miradi ya foundation yake na ilianza siku nyingi kabla hata huyo mtu wako hajawa na ndoto ya kuwa siku moja watu watakosea na kumpa heshima hiyo.
Hao wengine ni program za kazi zinazowaleta bila kujali ni nani yupo hapo, hata Amin alikuwa anapokea wageni ofisini kwake waliokuwa wanaenda kwa program za kikazi.
Maelezo yako labda ungesema safari kama ile ya Raila kule kwake na kulala siku tatu ndiyo hayo maswali ungeuliza. Pale katembelewa yeye binafsi na sio nchi, Leo hii hata yeye angekuwa yuko Likizo huko kwao bado Bill Gates angeonana na Mama Samia.
Acha kupotosha watu kwa ushabiki maandazi