Rais Magufuli na mfumo Kristo

Status
Not open for further replies.

assadsyria3

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
6,903
4,051
Awali ya yote naomba nitangulie kusema na mapema kuwa yawezekana wakatokea watakao tofautiana nami na pengine hata kunishambulia. Hii ni kwasababu kila mmoja ana haki ya kuwa na mtazamo wake na hata ujasiri wa kufumbia macho dhulma pale inapofanywa kwasababu dhulma hiyo haimgusi yeye wala familia yake.

Wakati tunaelekea kupata uhuru mwishoni mwa miaka ya 1960, wengi tunakumbuka kulikuwa na mgawanyiko miongoni mwa wapigania uhuru. Mgawanyiko huu ulipelekea kuwa na vyama viwili, TANU na AMNUT. Japo AMNUT haikuwa na nguvu sana kiasi cha kuitikisa TANU, bado ukweli unabaki kuwa yalikuwepo makundi mawili tofauti.

Moja katika mtazamo wa AMNUT ilikuwa kwamba, ilikuwa ni mapema kwa Tanganyika kupewa uhuru, kwakuwa kwa hali ilivyokuwa kwa wakati ule, TANU kupewa uhuru ilikuwa kuwapa nafasi Wakristo wanufaike na kufaidika na uhuru peke yao huku Waislamu wapigania uhuru wakiishia kuwa raia wa daraja la tatu. Kwa maoni yao, ilikuwa ni bora kuchelewa kupata uhuru ili kupata muda wa kusawazisha tofauti zilizokuwepo, hasa za kielimu, baina ya wananchi wa dini kuu mbili, Uislamu na Ukristo.

Katika kujibu hoja hiyo, msimamo wa Mwalimu Nyerere ulikuwa kwamba, mkoloni yule yule aliyewakandamiza Waislamu wakabaki nyuma, hawezi kutatua tatizo hilo. Badala yake, ni jukumu la Viongozi katika Tanganyika huru kushughulikia tatizo hilo. Kisiasa, ni wazi hoja ya Mwalimu Nyerere ilikuwa na maana, na hivyo Waislamu wengi wakamuunga mkono. Kutokana na jinsi Mwalimu Nyerere alivocheza karata zake za kisiasa katika kupigania uhuru na hata baada ya kupatikana uhuru, ilimjengea imani kwa Waislamu na wananchi kwa ujumla.

Kutokana na Imani hiyo, na hasa Waislamu, ilikuwa ni vigumu kwa mtu kumnyooshea kidole kuwa hatendi haki. Na akithubutu, atashambuliwa na kutengwa. Ni kwa namna hii Sheikh Suleiman Takadir alipata misukosuko na hata kutengwa na Waislamu wenzake. Matokeo yake, malalamiko na madai ya ubaguzi na hujuma dhidi ya Waislamu wakati wa serikali ya Awamu ya Kwanza, imebakia kuwa historia chungu kwa Umma wa Kiislamu nchini Tanzania. Kama alivyojisemea Remmy Ongala, imekuwa ni kilio cha samaki, machozi yamekwenda na maji. Hakuna hata anayesikia na kujali kilio cha Waislamu katika walioshikilia ‘mpini.’

Wakati wa kamapeni, Mh. John Pombe Magufuli mara kadhaa alisisitiza kuwa hatowabagua watu kwa rangi zao, kwa makabila yao wala kwa dini zao. Hii ilileta faraja kuwa Mh. Magufuli ataleta usawa na haki katika serikali yake. Hata hivyo, Rais John Pombe Magufuli (JPM) nae ameingia kwa gia ileile. Amejitahidi kutengeneza mazingira ya kuaminiwa na ameaminika. Kila kona ni slogan za Rais Magufuli.

Kila mtu anamuunga mkono Mh. Rais Magufuli. Sasa katika mazingira haya na katika kuzingatia historia na uzoefu wa mambo wakati wa Mwalimu Nyerere, kuna haja ya kuwa makini. Katika mazingira haya yanayoendelea kujiumba, iwapo atatokea wa kulalamika kwamba kuna hujuma dhidi ya kundi fulani, iwe la kidini au kibaila, watu watamshangaa. Na ni hivi majuzi tu kakutana na Mufti Zuber wa BAKWATA naye akamsifia sana. Kipi tena cha kuthibitisha kuwa Rais ni mtenda haki, asiye bagua watu zaidi ya heshma aliyopewa Mufti kukaribishwa Ikulu?

Mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Magufuli alianza kwa hotuba kali sana wakati akilizindua Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hotuba ile ilileta hamasa ya hali ya juu sana na hata kuamsha ari ya uungwaji mkono kutoka kwa Watanzania wa ngazi ya kati na chini. Kilichofuatia ni kuanza na operation aliyoiita operation ya kutumbua majipu! Operation hii ilifanyika kwa kuanzia bandari na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Msisimko na shangwe za uungwaji mkono zilisikika kila kona ya Tanzania. Haikuchukua muda, akaanza kuonekana kama mtu aliyekuja kulikomboa taifa letu – Naam, mazingira yakawa wazi kufanya atakalo na hakuna mtu wa kulalama wala kudadisi. Kwanini? Kwasababu ameaminiwa kuwa yeye anafanya kwa maslahi ya taifa. Yeyote atakaye nyoosha kidole kudadisi au kuhoji, anaonekana mtu wa ajabu tena anataka kukwamisha harakati za kizalendo.

Ubaya wa mazingira kama haya ni kuwa huenda watu wakawa wazito kumsaidia Mheshimiwa Rais pale wanapohisi kwamba mambo hayaendi sawa. Wingu la ‘umaarufu’ na kuungwa mkono litawazuiya watu kuwa wakweli kwa Rais kwa kuhofia yasije yakawakuta yaliyomkuta Sheikh Suleiman Takadiri. Lakini kwa Mheshimiwa Rais naye, kwa kusikia nyimbo na ngonjera za ‘sifa’ tu na kuungwa mkono, anaweza asipate fursa ya kutizama pale penye dosari ndogo ndogo ambapo pangehitaji marekebisho.

Binafsi naamini kwamba, haitakuwa tunamsaidia Mheshimiwa Rais JPM iwapo hatutasema pale tunapoona kuwa mambo hayaendi sawa kama ilivyo dhamira njema ya Rais. Mheshimiwa Rais JPM ni binadamu na katika ari na hamasa ya kulitumikia taifa anaweza kujikwaa hapa na pale. Na hivyo ni wajibu wetu kumsaidia Rais wetu kipenzi. Na hapa mimi nitazungumzia yale ambayo nadhani hata katika mazungumzo yake na Mufti Zuberi hawakuyagusa.

Uteuzi wa Baraza la Mawaziri

Uteuzi wa Baraza la Mawaziri, kwangu mimi, umeacha maswali mengi kuliko majibu. Japo inashangaza Waislamu kupigwa ganzi na kushindwa kupaza sauti, pengine ni kutokana na mazingira ya “kizalendo” yaliyokwishajijenga. Ukiangalia Baraza la Mawaziri alilotangaza Mh. Magufuli, utaona kuwa Waislamu katika Baraza hilo (Japo kwa majina yao tu) ni 9 (8?) kati ya 34 sawa na 24%! tu. Hii ina maana Wakristo katika Baraza la Mawaziri ni 76%!

Tunajua hii ni ‘Awamu ya Hapa Kazi tu’, na kigezo cha mtu kuingia katika Timu ya Kumsaidia Rais, ni uchapa kazi. Swali ni je, hakuna Waislamu wachapa kazi wenye sifa za kuwa mawaziri wa kumudu kasi ya Mheshimiwa Rais JPM?
Tunajua pia kuwa ‘Imani’ ya mtu, haitafsiri utendaji kazi wake au uvivu wake au hata ufisadi wake na hivyo katika “Hapa Kazi Tu”, hoja ya Imani wakati wa uteuzi, yaweza kuwa haikuzingatiwa.

Lakini pengine tujiulize, itakuwa halali na sawa kisiasa, watu wa dini moja kufanya maamuzi na kuamua mustakabali wa nchi hii peke yao? Je, hii inasaidia vipi kujenga umoja na mshikamnao wa Watanzania na kuondoa ubaguzi? Je, hii ndiyo tafsiri stahiki (kivitendo) ya kauli na ahadi ya Mheshimiwa Rais Magufuli kwamba ataongoza kwa haki bila ya kubagua dini za watu?

Wapo mawaziri waliotolewa kutoka sehemu mbalimbali na hawajawahi kuwa viongozi wa kisiasa, haiingii akilini kwangu kuwa Waislamu hawapo!
Ikiwa inadhaniwa kuwa suala la imani sio muhimu katika uteuzi, hii ina maana inahalalisha watu wengi wa dini moja kufanya maamuzi ya nchi peke yao. Labda tusaidiane kwa pamoja, tunajua katika nchi hii zipo Dini Kuu mbili, Uislamu na Ukristo. Je, iwapo haya ya 20 kwa 80 yaliyo kwa Waislamu yatageuziwa kwa upande wa pili, wenzetu wataridhia tukitumia hoja ile ile ‘serikali haina dini na hatuangalii dini ya mtu?”

Aliwahi kulalamika Mzee Mtei ilipoteuliwa Tume ya Mzee Warioba juu ya Katiba akisema kuwa kulikuwa na Waislamu wengi na akasisitiza kuwa hoja kwamba nchi haina dini na haiongozwi kwa misingi ya dini, haistahiki kutolewa. Akasema, hatuwezi kupinga ukweli kwamba mtizamo na maamuzi ya watu yanaathiriwa na Imani za dini zao. Lakini tutakumbuka pia kwamba wakati wa Mzee Ally Hassan Mwinyi ilitokea katika Baraza lake la Mawaziri, yakaongezeka majina ya Waislamu kinyume na ilivyokuwa ada.

Japo idadi yenyewe wala haikufikia robo ya Mawaziri wote, lakini zikapigwa sana kelele na kudaiwa kuwa Mwinyi anataka kuisilimisha Tanzania. Hayo yaliwahi kutokea pia kwa Rais Mstaafu JK alipoteuwa idadi fulani ya Mabalozi ikaonekana kuwa kulikuwa na majina mengi ya Waislamu. Nakumbuka marehemu Profesa Seithy Chachage aliwahi kutupiwa swali kwamba haoni kuwepo kwa majina mengi ya Kiislamu ni dalili kuwa Kikwete anapendelea Waislamu? Jibu la Profesa Chachage lilikuwa kwamba inabidi kwanza ufanyike utafiti tujue serikalini katika nafasi zote muhimu, kuna Waislamu wangapi na Wakristo wangapi, ndio tuseme.

Kama huu ndio ukweli kama alivyoubainisha Mzee Mtei, na kama hii ndiyo hali unapogeuza mambo kwa upande wa pili, kwa nini idhaniwe kuwa Waislamu wao wataridhia kuona Baraza la Mawaziri na ‘Timu’ ya Watendaji Wakuu Serikalini katika Uwiano huu wa 20 kwa 80?

Kama Mh. Rais anaamini kuwa kuna Waislamu walimpigia kura na hata kumpigania hata akashinda, siamini kuwa walikuwepo tu Waislamu wa kupiga kura, lakini wa kushika nafasi za Mawaziri na Makatibu Wakuu, tabu kuwapata.
Katika mambo ambayo Waislamu wamebaki na butwaa, ni uteuzi wa Mh. Ndalichako kuwa Waziri wa Elimu.

Mtu ambae alisababisha mpaka maandamano dhidi yake kutokana na tuhuma za hujuma iliyokuwa ikidaiwa kufanywa dhidi ya Waislamu akiwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa. Mh. Ndalichako alidiriki kubadilisha matokeo ya mtihani yaliyokuwa tayari yametangazwa baada ya kupigiwa kelele! Wakati akiwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania. Leo ndio kapewa nafasi ya kuwa Waziri wa Elimu!

Uteuzi wa Makatibu Wakuu

Uteuzi wa Makatibu Wakuu haukuwa na nafuu kwa Waislamu hata kidogo. Kwani kati ya Makatibu Wakuu na Manaibu wao walioteuliwa wapatao 50, kati yao Waislamu japo kwa majina ni 10 (11?) tu sawa na 20%, huku waliosalia sawa na 80% ni Wakristo. Hawa ndio watendaji wa serikali. Hawa ndio wanaopanga na kuratibu mipango ya maendeleo ya nchi. Bado hoja ni zile zile, inawezekana ikawa ni kweli kuwa hakuna Waislamu wachapakazi na wenye sifa za kuwa Makatibu Wakuu wanaoweza kumudu kasi ya Mheshimiwa Rais JPM? Kama ilivyokuwa kwa Mawaziri, wapo pia Makatibu Wakuu walioteuliwa wakitokea katika taasisi za elimu ya juu na taasisi nyingine.

Je, huko hakuna Waislamu wenye sifa na uwezo wa kushika nyadhifa hizo? Inawezekana wakawa wapo, lakini Mh. Rais hakuona haja ya kuzingatia uwiano wa dini mbalimbali katika uteuzi. Lakini mtu anaweza kuhoji, kama ingekuwa si kuzingatia imani, basi ingetokea bahati mbaya Waislamu nao wakawa wengi katika orodha ya Makatibu Wakuu kama ilivyokuwa kwa Wakristo katika Baraza la Mawaziri. Lakini bahati mbaya imekuwa ya kuwaangukia Waislamu kwa nyanja zote! Sijui Sayansi ya Bahati Nasibu-sio jambo la kupanga (Science of Coincidence), inasemaje hapa.

Ikumbukwe kuwa Mh. Rais aliahidi wakati wa kampeni kuwa, katika utawala wake hatowabagua watu kwa rangi zao, makabila yao wala dini zao. Kauli sahihi kabisa. Lakini labda tujiulize, kipi cha kuthibitisha ahadi hii? Kama nilivyotangulia kusema, yawezekana katika kuongozwa na ahadi hiyo ya kutokubagua, Mheshimiwa Rais hakutizama kabisa suala la dini katika uteuzi wake. Lakini labda pengine tuligeuze jambo hili liwe kwa upande mwingine. Asilimia 10 ya Mawaziri Wakristo, 90 Waislamu, asilimia 80 ya Makatibu Wakuu, Waislamu, waliosalia dini nyingine!

Huu ni mwanzo wa safari ndefu mbele yetu. Tunamuomba Mh. Magufuli atembee juu ya maneno yake, atende haki. Hoja za kisiasa kwamba katika uteuzi hatujali dini bali sifa, haitatusaidia sana na wala haifanyi kazi. Labda atokee mtu aje na utafiti wa kisayansi kuthibitisha mambo mawili.

Moja, kwamba kadiri alivyochambua, hao asilimia 20 tu, ndio Waislamu pekee aliopata katika seti ya Waislamu nchini wenye sifa za kuwa Mawaziri na Makatibu Wakuu. Lakini pia katika utafiti huo, atuonyeshe sifa zilizozingatiwa katika hao waliowateua ili kuweza kuona kwamba kweli katika ‘seti’ ya Waislamu wenye sifa, hakuna mwenye sifa hizo
.

Chanzo: Anuur newspaper

mytake
Tazama list ya wakuu wa mikoa, tazama list ya wakuu wa wilaya.
 
Ndugu, umeandika mambo mengi kwa kutumia mihemko tu.

Udini ni mind - set ya mtu.

Je! Kiongozi akiwa mkristo au muislamu, inakuzuia nini wewe kupata mkate wako wa kila siku?!

Imefikia wakati sasa naomba tuachane na upuuzi huu!

Fanya kazi halali ili upate kipato halali.

#ACHA KUTEGEMEA MBELEKO ZA DINI AU KABILA#
 
Unataka maji, umeme, barabara au unataka mchungaji/sheikh? Hao viongozi wameteuliwa kuongoza ibada? Na kwanini tunaingelea dini mbili tu (wakristu na waislam) na kuacha Watanzania wa dini nyingine mfano, bohora, dini za asili n.k.?

Na mwisho, Wahindi hawalalamiki kabisa licha ya baraza zima la mawaziri kutokuwa na mhindi hata mmoja. Na hata kutumbuliwa wahindi wanatafuta namna ya kupambana na maisha. Hivi sisi Watanzania weusi tuna kasoro gani? Tumelelewa vibaya? Kwanini umaskini, udini tunaulilia sisi wakati wahindi waliozaliwa hapa hapa wanapiga hatua licha ya kuwa wachache kwenye nafasi ya uongozi?
 
Awali ya yote naomba nitangulie kusema na mapema kuwa yawezekana wakatokea watakao tofautiana nami na pengine hata kunishambulia. Hii ni kwasababu kila mmoja ana haki ya kuwa na mtazamo wake na hata ujasiri wa kufumbia macho dhulma pale inapofanywa kwasababu dhulma hiyo haimgusi yeye wala familia yake.
Wakati tunaelekea kupata uhuru mwishoni mwa miaka ya 1960, wengi tunakumbuka kulikuwa na mgawanyiko miongoni mwa wapigania uhuru. Mgawanyiko huu ulipelekea kuwa na vyama viwili, TANU na AMNUT. Japo AMNUT haikuwa na nguvu sana kiasi cha kuitikisa TANU, bado ukweli unabaki kuwa yalikuwepo makundi mawili tofauti. Moja katika mtazamo wa AMNUT ilikuwa kwamba, ilikuwa ni mapema kwa Tanganyika kupewa uhuru, kwakuwa kwa hali ilivyokuwa kwa wakati ule, TANU kupewa uhuru ilikuwa kuwapa nafasi Wakristo wanufaike na kufaidika na uhuru peke yao huku Waislamu wapigania uhuru wakiishia kuwa raia wa daraja la tatu. Kwa maoni yao, ilikuwa ni bora kuchelewa kupata uhuru ili kupata muda wa kusawazisha tofauti zilizokuwepo, hasa za kielimu, baina ya wananchi wa dini kuu mbili, Uislamu na Ukristo.
Katika kujibu hoja hiyo, msimamo wa Mwalimu Nyerere ulikuwa kwamba, mkoloni yule yule aliyewakandamiza Waislamu wakabaki nyuma, hawezi kutatua tatizo hilo. Badala yake, ni jukumu la Viongozi katika Tanganyika huru kushughulikia tatizo hilo. Kisiasa, ni wazi hoja ya Mwalimu Nyerere ilikuwa na maana, na hivyo Waislamu wengi wakamuunga mkono. Kutokana na jinsi Mwalimu Nyerere alivocheza karata zake za kisiasa katika kupigania uhuru na hata baada ya kupatikana uhuru, ilimjengea imani kwa Waislamu na wananchi kwa ujumla.
Kutokana na Imani hiyo, na hasa Waislamu, ilikuwa ni vigumu kwa mtu kumnyooshea kidole kuwa hatendi haki. Na akithubutu, atashambuliwa na kutengwa. Ni kwa namna hii Sheikh Suleiman Takadir alipata misukosuko na hata kutengwa na Waislamu wenzake. Matokeo yake, malalamiko na madai ya ubaguzi na hujuma dhidi ya Waislamu wakati wa serikali ya Awamu ya Kwanza, imebakia kuwa historia chungu kwa Umma wa Kiislamu nchini Tanzania. Kama alivyojisemea Remmy Ongala, imekuwa ni kilio cha samaki, machozi yamekwenda na maji. Hakuna hata anayesikia na kujali kilio cha Waislamu katika walioshikilia ‘mpini.’
Wakati wa kamapeni, Mh. John Pombe Magufuli mara kadhaa alisisitiza kuwa hatowabagua watu kwa rangi zao, kwa makabila yao wala kwa dini zao. Hii ilileta faraja kuwa Mh. Magufuli ataleta usawa na haki katika serikali yake. Hata hivyo, Rais John Pombe Magufuli (JPM) nae ameingia kwa gia ileile. Amejitahidi kutengeneza mazingira ya kuaminiwa na ameaminika. Kila kona ni slogan za Rais Magufuli. Kila mtu anamuunga mkono Mh. Rais Magufuli. Sasa katika mazingira haya na katika kuzingatia historia na uzoefu wa mambo wakati wa Mwalimu Nyerere, kuna haja ya kuwa makini. Katika mazingira haya yanayoendelea kujiumba, iwapo atatokea wa kulalamika kwamba kuna hujuma dhidi ya kundi fulani, iwe la kidini au kibaila, watu watamshangaa. Na ni hivi majuzi tu kakutana na Mufti Zuber wa BAKWATA naye akamsifia sana. Kipi tena cha kuthibitisha kuwa Rais ni mtenda haki, asiye bagua watu zaidi ya heshma aliyopewa Mufti kukaribishwa Ikulu?
Mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Magufuli alianza kwa hotuba kali sana wakati akilizindua Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hotuba ile ilileta hamasa ya hali ya juu sana na hata kuamsha ari ya uungwaji mkono kutoka kwa Watanzania wa ngazi ya kati na chini. Kilichofuatia ni kuanza na operation aliyoiita operation ya kutumbua majipu! Operation hii ilifanyika kwa kuanzia bandari na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Msisimko na shangwe za uungwaji mkono zilisikika kila kona ya Tanzania. Haikuchukua muda, akaanza kuonekana kama mtu aliyekuja kulikomboa taifa letu – Naam, mazingira yakawa wazi kufanya atakalo na hakuna mtu wa kulalama wala kudadisi. Kwanini? Kwasababu ameaminiwa kuwa yeye anafanya kwa maslahi ya taifa. Yeyote atakaye nyoosha kidole kudadisi au kuhoji, anaonekana mtu wa ajabu tena anataka kukwamisha harakati za kizalendo.
Ubaya wa mazingira kama haya ni kuwa huenda watu wakawa wazito kumsaidia Mheshimiwa Rais pale wanapohisi kwamba mambo hayaendi sawa. Wingu la ‘umaarufu’ na kuungwa mkono litawazuiya watu kuwa wakweli kwa Rais kwa kuhofia yasije yakawakuta yaliyomkuta Sheikh Suleiman Takadiri. Lakini kwa Mheshimiwa Rais naye, kwa kusikia nyimbo na ngonjera za ‘sifa’ tu na kuungwa mkono, anaweza asipate fursa ya kutizama pale penye dosari ndogo ndogo ambapo pangehitaji marekebisho.
Binafsi naamini kwamba, haitakuwa tunamsaidia Mheshimiwa Rais JPM iwapo hatutasema pale tunapoona kuwa mambo hayaendi sawa kama ilivyo dhamira njema ya Rais. Mheshimiwa Rais JPM ni binadamu na katika ari na hamasa ya kulitumikia taifa anaweza kujikwaa hapa na pale. Na hivyo ni wajibu wetu kumsaidia Rais wetu kipenzi. Na hapa mimi nitazungumzia yale ambayo nadhani hata katika mazungumzo yake na Mufti Zuberi hawakuyagusa.
Uteuzi wa Baraza la Mawaziri
Uteuzi wa Baraza la Mawaziri, kwangu mimi, umeacha maswali mengi kuliko majibu. Japo inashangaza Waislamu kupigwa ganzi na kushindwa kupaza sauti, pengine ni kutokana na mazingira ya “kizalendo” yaliyokwishajijenga. Ukiangalia Baraza la Mawaziri alilotangaza Mh. Magufuli, utaona kuwa Waislamu katika Baraza hilo (Japo kwa majina yao tu) ni 9 (8?) kati ya 34 sawa na 24%! tu. Hii ina maana Wakristo katika Baraza la Mawaziri ni 76%!
Tunajua hii ni ‘Awamu ya Hapa Kazi tu’, na kigezo cha mtu kuingia katika Timu ya Kumsaidia Rais, ni uchapa kazi. Swali ni je, hakuna Waislamu wachapa kazi wenye sifa za kuwa mawaziri wa kumudu kasi ya Mheshimiwa Rais JPM?
Tunajua pia kuwa ‘Imani’ ya mtu, haitafsiri utendaji kazi wake au uvivu wake au hata ufisadi wake na hivyo katika “Hapa Kazi Tu”, hoja ya Imani wakati wa uteuzi, yaweza kuwa haikuzingatiwa. Lakini pengine tujiulize, itakuwa halali na sawa kisiasa, watu wa dini moja kufanya maamuzi na kuamua mustakabali wa nchi hii peke yao? Je, hii inasaidia vipi kujenga umoja na mshikamnao wa Watanzania na kuondoa ubaguzi? Je, hii ndiyo tafsiri stahiki (kivitendo) ya kauli na ahadi ya Mheshimiwa Rais Magufuli kwamba ataongoza kwa haki bila ya kubagua dini za watu?
Wapo mawaziri waliotolewa kutoka sehemu mbalimbali na hawajawahi kuwa viongozi wa kisiasa, haiingii akilini kwangu kuwa Waislamu hawapo!
Ikiwa inadhaniwa kuwa suala la imani sio muhimu katika uteuzi, hii ina maana inahalalisha watu wengi wa dini moja kufanya maamuzi ya nchi peke yao. Labda tusaidiane kwa pamoja, tunajua katika nchi hii zipo Dini Kuu mbili, Uislamu na Ukristo. Je, iwapo haya ya 20 kwa 80 yaliyo kwa Waislamu yatageuziwa kwa upande wa pili, wenzetu wataridhia tukitumia hoja ile ile ‘serikali haina dini na hatuangalii dini ya mtu?”
Aliwahi kulalamika Mzee Mtei ilipoteuliwa Tume ya Mzee Warioba juu ya Katiba akisema kuwa kulikuwa na Waislamu wengi na akasisitiza kuwa hoja kwamba nchi haina dini na haiongozwi kwa misingi ya dini, haistahiki kutolewa. Akasema, hatuwezi kupinga ukweli kwamba mtizamo na maamuzi ya watu yanaathiriwa na Imani za dini zao. Lakini tutakumbuka pia kwamba wakati wa Mzee Ally Hassan Mwinyi ilitokea katika Baraza lake la Mawaziri, yakaongezeka majina ya Waislamu kinyume na ilivyokuwa ada. Japo idadi yenyewe wala haikufikia robo ya Mawaziri wote, lakini zikapigwa sana kelele na kudaiwa kuwa Mwinyi anataka kuisilimisha Tanzania. Hayo yaliwahi kutokea pia kwa Rais Mstaafu JK alipoteuwa idadi fulani ya Mabalozi ikaonekana kuwa kulikuwa na majina mengi ya Waislamu. Nakumbuka marehemu Profesa Seithy Chachage aliwahi kutupiwa swali kwamba haoni kuwepo kwa majina mengi ya Kiislamu ni dalili kuwa Kikwete anapendelea Waislamu? Jibu la Profesa Chachage lilikuwa kwamba inabidi kwanza ufanyike utafiti tujue serikalini katika nafasi zote muhimu, kuna Waislamu wangapi na Wakristo wangapi, ndio tuseme.
Kama huu ndio ukweli kama alivyoubainisha Mzee Mtei, na kama hii ndiyo hali unapogeuza mambo kwa upande wa pili, kwa nini idhaniwe kuwa Waislamu wao wataridhia kuona Baraza la Mawaziri na ‘Timu’ ya Watendaji Wakuu Serikalini katika Uwiano huu wa 20 kwa 80?
Kama Mh. Rais anaamini kuwa kuna Waislamu walimpigia kura na hata kumpigania hata akashinda, siamini kuwa walikuwepo tu Waislamu wa kupiga kura, lakini wa kushika nafasi za Mawaziri na Makatibu Wakuu, tabu kuwapata.
Katika mambo ambayo Waislamu wamebaki na butwaa, ni uteuzi wa Mh. Ndalichako kuwa Waziri wa Elimu. Mtu ambae alisababisha mpaka maandamano dhidi yake kutokana na tuhuma za hujuma iliyokuwa ikidaiwa kufanywa dhidi ya Waislamu akiwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa. Mh. Ndalichako alidiriki kubadilisha matokeo ya mtihani yaliyokuwa tayari yametangazwa baada ya kupigiwa kelele! Wakati akiwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania. Leo ndio kapewa nafasi ya kuwa Waziri wa Elimu!
Uteuzi wa Makatibu Wakuu
Uteuzi wa Makatibu Wakuu haukuwa na nafuu kwa Waislamu hata kidogo. Kwani kati ya Makatibu Wakuu na Manaibu wao walioteuliwa wapatao 50, kati yao Waislamu japo kwa majina ni 10 (11?) tu sawa na 20%, huku waliosalia sawa na 80% ni Wakristo. Hawa ndio watendaji wa serikali. Hawa ndio wanaopanga na kuratibu mipango ya maendeleo ya nchi. Bado hoja ni zile zile, inawezekana ikawa ni kweli kuwa hakuna Waislamu wachapakazi na wenye sifa za kuwa Makatibu Wakuu wanaoweza kumudu kasi ya Mheshimiwa Rais JPM? Kama ilivyokuwa kwa Mawaziri, wapo pia Makatibu Wakuu walioteuliwa wakitokea katika taasisi za elimu ya juu na taasisi nyingine. Je, huko hakuna Waislamu wenye sifa na uwezo wa kushika nyadhifa hizo? Inawezekana wakawa wapo, lakini Mh. Rais hakuona haja ya kuzingatia uwiano wa dini mbalimbali katika uteuzi. Lakini mtu anaweza kuhoji, kama ingekuwa si kuzingatia imani, basi ingetokea bahati mbaya Waislamu nao wakawa wengi katika orodha ya Makatibu Wakuu kama ilivyokuwa kwa Wakristo katika Baraza la Mawaziri. Lakini bahati mbaya imekuwa ya kuwaangukia Waislamu kwa nyanja zote! Sijui Sayansi ya Bahati Nasibu-sio jambo la kupanga (Science of Coincidence), inasemaje hapa.
Ikumbukwe kuwa Mh. Rais aliahidi wakati wa kampeni kuwa, katika utawala wake hatowabagua watu kwa rangi zao, makabila yao wala dini zao. Kauli sahihi kabisa. Lakini labda tujiulize, kipi cha kuthibitisha ahadi hii? Kama nilivyotangulia kusema, yawezekana katika kuongozwa na ahadi hiyo ya kutokubagua, Mheshimiwa Rais hakutizama kabisa suala la dini katika uteuzi wake. Lakini labda pengine tuligeuze jambo hili liwe kwa upande mwingine. Asilimia 10 ya Mawaziri Wakristo, 90 Waislamu, asilimia 80 ya Makatibu Wakuu, Waislamu, waliosalia dini nyingine!
Huu ni mwanzo wa safari ndefu mbele yetu. Tunamuomba Mh. Magufuli atembee juu ya maneno yake, atende haki. Hoja za kisiasa kwamba katika uteuzi hatujali dini bali sifa, haitatusaidia sana na wala haifanyi kazi. Labda atokee mtu aje na utafiti wa kisayansi kuthibitisha mambo mawili. Moja, kwamba kadiri alivyochambua, hao asilimia 20 tu, ndio Waislamu pekee aliopata katika seti ya Waislamu nchini wenye sifa za kuwa Mawaziri na Makatibu Wakuu. Lakini pia katika utafiti huo, atuonyeshe sifa zilizozingatiwa katika hao waliowateua ili kuweza kuona kwamba kweli katika ‘seti’ ya Waislamu wenye sifa, hakuna mwenye sifa hizo.

tazama list ya wakuu wa mikoa, tazama list ya wakuu wa wilaya.
Kwanza kwani dini ni nini kwenye uongozi? Sasa sisi ambao hatuamini mungu tusemeje? Acha habari hizo bhana
 
Ukweli mchungu huu
 
Du! Mpaka natetemeka maana naogopa sana kujihusisha na mambo ya dini kwasababu najua madhira yake
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom