Rais Magufuli, kwanini haujaenda Japan?

Rais Magufuli, kwanini haujaenda Japan?

Ni dharau sana kwa mkuu mmoja wa nchi huko nje kuwaita marais wote wa Afrika kwake ili kujadili nao maendeleo ya Afrika. It is, in the background, to make himself equal to all of them combined.

Wa zamani mtamkumbuka Rais Jomo Kenyata. Alikuwa hapandi ndege. Safari zake sana sana kwenda Mombasa au sehemu za nchi jirani, kwa barabara. Point hapa ni kwamba hakuwa anasafiri nje na bado kajenga sana uchumi wa Kenya.

Maendeleo ya Afrika yataletwa na Waafrika wenyewe. Viongozi wa nchi za nje wanawaalika marais wa Afrika kwao ili kulinda mirija ya nchi zao ndani ya Afrika. Maneno mbadala ni camouflage tu.

Naunga mkono Jiwe kutokwenda. Hata kumtuma Waziri Mkuu ni makosa. Balozi wetu Japan angetosha sana.

Tukatae kudharauliwa. Ukitaka kushiriki maendeleo yetu basi karibu kwetu tuzungumze.

Well done on this one, Jiwe!
 
Mimi hapa nina sababu kamili tena zinazofahamika ila Nitafuteni baadaye nawahi hapa kiwanjani nione kama babu keshalipwa nirudi na hiyo ndege.
Ok nimerudi,sikuweza kurudi na ndege kwani babu bado amegoma kuiachia na amesema mkichelewa Jumatano ataipeleka kwao Israel.Jibu la swali lako sasa ni kwamba hakwenda kwa sababu miaka yote wakuu wa SADEKI hawaendagi kwenjye hii mikutano.Wewe unataka aende akafanye nini?
 
Kikao kina umuhimu sana. Ukizingatia yeye anapenda maendeleo.

1.kwa nini maendeleo ya afrika wajadili Japan?'japan ni afrika?

2.tangu nchi za afrika zipate uhuru vikao kama hivi ni vya kawaida for decades; je una statistics za mafanikio ya hivi vikao? with proof
 
Ni dharau sana kwa mkuu mmoja wa nchi huko nje kuwaita marais wote wa Afrika kwake ili kujadili nao maendeleo ya Afrika. It is, in the background, to make himself equal to all of them combined.

Wa zamani mtamkumbuka Rais Jomo Kenyata. Alikuwa hapandi ndege. Safari zake sana sana kwenda Mombasa au sehemu za nchi jirani, kwa barabara. Point hapa ni kwamba hakuwa anasafiri nje na bado kajenga sana uchumi wa Kenya.

Maendeleo ya Afrika yataletwa na Waafrika wenyewe. Viongozi wa nchi za nje wanawaalika marais wa Afrika kwao ili kulinda mirija ya nchi zao ndani ya Afrika. Maneno mbadala ni camouflage tu.

Naunga mkono Jiwe kutokwenda. Hata kumtuma Waziri Mkuu ni makosa. Balozi wetu Japan angetosha sana.

Tukatae kudharauliwa. Ukitaka kushiriki maendeleo yetu basi karibu kwetu tuzungumze.

Well done on this one, Jiwe!
Sio kweli kwamba Jomo Kenyatta alikuwa hasafiri nje,Alikuwa anasafiri sana nje na ndiyo maana uchumi wa Kenya ulipanda juu tena kwa kuwa na viwanda vingi na vya kisasa.Ukitaka kutoka hapo ulipo,kutana na waliokuzidi kimaendeleo na sio kuwakimbia.
 
Sasa, unahakika mambo yote huko magogoni na Lumumba yapo sawa??!!, kaziba mianya yote ya wapigaji deals, je wanampenda??, Kazuia kusafirishwa kwa makinikia kiasi kwamba huko kwa mabeberu viwanda vya kuchakata makinikia vimedorora, je mabeberu wanapenda??, tena akienda huko kwao (mkutanoni) si ndiyo itakuwa rahisi kumpata na kumdhuru kwa lolote nk,.!!!

Hayo ni maoni yangu tu, naweza nisiwe sahihi.😁
Kama ni hatari kwake tumshauri asisafiri popote kwa sababu wao huko nje wako kila mahali.Lakini si hata wakitaka watamfuata tu hapahapa?
 
Kama ni hatari kwake tumshauri asisafiri popote kwa sababu wao huko nje wako kila mahali.Lakini si hata wakitaka watamfuata tu hapahapa?


Hapa Bongo sio rahisi, mcheza kwao hutuzwa.🇹🇿🇹🇿😁
 
Ndio maana kuna wawakilishi ndugu yangu... Kilakona aende yeye ataweza? Mbona rais wa korea Kazkazini hajawahi kufika Africa na mambo yake yanaendelea kam kawaida!!!?? Muache Jembe JPM apige kazi

Kuna safari za kutuma wawakilishi lakini sio mikutano mikubwa kama hii.Mikutano hii huwezi fananisha na safari za Rwanda,Uganda,Kenya nk.Hapa kuna kitu cha ziada.
 
Haiwezekani maendeleo ya Africa yakajadiliwe Japan.

Tuna miradi mingi sana, lazima tutumie fedha zetu kwaajili ya hiyo miradi,safari hazina maana.

Nasema uongo jamani?
​
Ndiyo
 
Labda mashariti ya wazee wa Gamboshi.
 
Hapana sijapotoshwa. Nimesoma sehemu nyingi tu. Nkurumah alikuwa dictator alijidhibitisha kama Rais wa Maisha. Alifunga waliompinga. Ndo maana ikawa Rais kwake kupinduliwa.
Mwambia agoogle hapo chap Kwame Nkurumah.ataona unayoyasema.
 
1.kwa nini maendeleo ya afrika wajadili Japan?'japan ni afrika?

2.tangu nchi za afrika zipate uhuru vikao kama hivi ni vya kawaida for decades; je una statistics za mafanikio ya hivi vikao? with proof
Japan ni mdau mkubwa wa maendeleo. Yes maendeleo ya waafrica yataletwa na waafrica wenyewe. Ila ni kwa kushirikiana na walioendelea tayari. Jamani huangalii hata miradi yetu yote pesa kuna mkono wa wahisani,technology pia tunawahitaji asilimia 100 kwa ajili ya kubuild capacity yetu.
 
Maendeleo yako Africa na yataletwa na Waafrica wenyewe. Ni upuuzi kutwa kucha kutanga tanga nyumba za jirani kuomba omba chakula cha wanao
Yes upo sawa,ila umesahau kwa msaada wa wahisani. Pesa na technology.
 
Sio kweli kwamba Jomo Kenyatta alikuwa hasafiri nje,Alikuwa anasafiri sana nje na ndiyo maana uchumi wa Kenya ulipanda juu tena kwa kuwa na viwanda vingi na vya kisasa.Ukitaka kutoka hapo ulipo,kutana na waliokuzidi kimaendeleo na sio kuwakimbia.

Kwa miaka 14 ambapo Jomo Kenyatta alikuwa Rais wa Kenya, alipanda ndege mara moja tu. Hii ilikuwa 1969 alipokwenda Ethiopia kuonana na Mfalme Haile Selasie.

Usiite watu waongo bila kuchunguza vizuri.
 
Kabudi ni mkoministi yeye kaamua kumshauri mtukufu waongoze Nchi kienyeji kinyume cha Sheria na katiba, sasa wanaongoza kwa mujibu za zidumu fikra zao binafsi siyo Sheria za Nchi
Yani mi nawaangaliagaaa muda wote wanawalalamilkia mabeberu tu alafu hawaonyeshi way foward miaka ya kulalamika ilikua 1990 huko lakini kila siku wanazungumza ukombozi utazani tuko kwenye harakati za kutafuta uhuru. Mi nishabiki wa magufuli ila hawa wakina kabudi wanaboa bora angekua anamsikiliza dr mpango yule jamaa yuko modern kidogo
 
Hata mimi nashangaa sana sijui kwanini presdaa anaweka kapuni hizi safari muhimu kwa maendeleo

Labda pengine kuna intelligent info zinazofanya asiende

Otherwise hii ni tatizo kabisa sasa si jokes tena
 
Ana mambo mengi ya kuweka sana hapa nchini na ukumbuke mwakani kuna uchaguzi mkuu hivyo lazima aweke mambo sawa kama waliomweka kwenye hiyo nafasi hawajamfanya hamna
 
Kule Japan kuna mkutano unaohusu Maendeleo ya Africa. Najua Rais Magufuli ni muumini wa maendeleo.

Japan ni mdau mkubwa wa maendeleo hapa nchini kwetu.

Rais Magufuli najua umemtuma Waziri Mkuu, ila kumbuka tulikuchagua wewe na siyo Waziri Mkuu.

Unajua mkutano kuhudhuriwa na Rais kuna uzito wake?

Pia unakutana na ideas mpya. Sasa wewe umejifungia tu Ikulu huku marais wenzako wa Africa wanajadili maendeleo.

Tena hapa ungetumia uchu ulionao kwa maendeleo kuongea na waziri mkuu wa Japan.
Angalia Rais wa Rwanda juzi alikuwa France kwenye G7. Leo yupo Japan.

Rais wa South Africa pia ilikuwepo kwenye SADC, akawepo kwenye G7 leo yupo Japan.

Kama mpenda maendeleo ulitakiwa usikose huu mkutano.

View attachment 1192348View attachment 1192349View attachment 1192350
Akienda huko watamkamata kama ilivyokamatwa ile airbus na Yule mkulima. Na Mimi naomba akamatweee kwanini hataki kulipa madeni??
 
Kwame Nkurumah alipinduliwa kwa sababu alitaka kubadili katiba ili awe Rais wa maisha. Hapo ndo alikosea.
Sasa Magufuli hajataka kubadili katiba.
Kupinduliwa siyo rahisi,lazima kuwe na sababu.
Kwa hiyo akibadili katiba na yeye anakuwa kwenye risk ya kupinduliwa ?
 
Back
Top Bottom