Rais Magufuli, kwanini haujaenda Japan?

Rais Magufuli, kwanini haujaenda Japan?

Ndio maana kuna wawakilishi ndugu yangu... Kilakona aende yeye ataweza? Mbona rais wa korea Kazkazini hajawahi kufika Africa na mambo yake yanaendelea kam kawaida!!!?? Muache Jembe JPM apige kazi
Hapana kuna mikutano mingine Rais ni muhimu aende. Kwenda kuongea na wengine napo ni kupiga kazi. Unaweza negotiate miradi ya maendeleo kwenye sector mbali mbali.
 
Akitoka tu,mabaharia wanapindua meli.
Halafu wanaofanyaga mapinduzi ni junior officers unakuta hata captain tu mwenye nyota tatu anaongoza mpango mzima
Kwa Tanzania haiwezekani kwa sasa. Labda huko mbeleni ikitokea hali ya kusababisha hayo.
 
Ngoja nimtetee katika hili. Isingewezekana aende kwa kuwa anashughulikia ndege iachiwe. Halafu akienda huko mkutano utafanyika kwa Kiswahili?
Wanasheria ndo wanashughulikia. Na solution ni kulipa deni. Kiingereza mbona anaelewa? Labda kuongea ndo tatizo ila pamoja na hayo anaeleweka.
 
Sasa, unahakika mambo yote huko magogoni na Lumumba yapo sawa??!!, kaziba mianya yote ya wapigaji deals, je wanampenda??, Kazuia kusafirishwa kwa makinikia kiasi kwamba huko kwa mabeberu viwanda vya kuchakata makinikia vimedorora, je mabeberu wanapenda??, tena akienda huko kwao (mkutanoni) si ndiyo itakuwa rahisi kumpata na kumdhuru kwa lolote nk,.!!!

Hayo ni maoni yangu tu, naweza nisiwe sahihi.😁
Hilo laweza kutokea endapo atataka kujiongezea muda 2025.
 
Cha muhimu ujumbe anapata na nina uhakika yeye au Jafo wamenisoma. Information is POWER.

Ndiyo Auntie wamekusoma, tunataka na sisi Rais wetu japo apate world exposure na wenzake huko majuu, "mgaagaa na upwa hali wali mkavu"--- wahenga walisema.
 
Kule Japan kuna mkutano unaohusu Maendeleo ya Africa. Najua Rais Magufuli ni muumini wa maendeleo.
Japan ni mdau mkubwa wa maendeleo hapa nchini kwetu.
Rais Magufuli najua umemtuma Waziri mkuu,ila kumbuka tulikuchagua wewe na siyo waziri mkuu.
Unajua mkutano kuhudhuriwa na Rais kuna uzito wako.
Pia unakutana na ideas mpya. Sasa wewe umejifungia tu Ikulu huku marais wenzako wa Africa wanajadili maendeleo.
Tena hapa ungetumia uchu ulionao kwa maendeleo kuongea na waziri mkuu wa Japan.
Angalia Rais wa Rwanda Juzi alikuwa France kwenye G7.Leo yupo Japan.
Rais wa South Africa pia ilikuwepo kwenye SADC,akawepo kwenye G7 leo yupo Japan.
Kama mpenda maendeleo ulitakiwa usikose huu mkutano.
View attachment 1192348View attachment 1192349View attachment 1192350
Hao pia ni mabeberu kama walivyo mabeberu wengine,

Inakuwaje mkutano unaohusu maendeleo ya Africa ufanyike Japan!?
Amin amin nawaambia,,,, "waafrika wasipoamka na kujipigania,,, hakuna ngozi nyeupe yoyote itakayokuja kuwapigania"

Amen.
 
Nimeona leo umeandika kitu cha tofauti. Nikaona labda it might be the food you had for dinner today.
Yaani wewe bwana. Nimeona niandike kwa maendeleo ya nchi yetu. Nchi hii ni yetu sote.
 
Ndiyo Auntie wamekusoma, tunataka na sisi Rais wetu japo apate world exposure na wenzake huko majuu, "mgaagaa na upwa hali wali mkavu"--- wahenga walisema.
Kabisa. Hata Jk alisema bora Mbwa anaetembea anaweza ambulia hata mfupa,kuliko mbwa aliejifungia ndani.
 
Hao pia ni mabeberu kama walivyo mabeberu wengine,

Inakuwaje mkutano unaohusu maendeleo ya Africa ufanyike Japan!?
Amin amin nawaambia,,,, "waafrika wasipoamka na kujipigania,,, hakuna ngozi nyeupe yoyote itakayokuja kuwapigania"

Amen.

Wewe huku Afrika unayo maendeleo gani??, hata kutengeneza sindano imekushinda!!, Chanjo ya Ebola imetoka huko huko kwao!!, Ugonjwa waetu wao wamehangaika kutafuta chanjo na tiba kwa ajili yetu!!, halafu leo unasimama kuwabeza!!🤔🤔
 
Hao pia ni mabeberu kama walivyo mabeberu wengine,

Inakuwaje mkutano unaohusu maendeleo ya Africa ufanyike Japan!?
Amin amin nawaambia,,,, "waafrika wasipoamka na kujipigania,,, hakuna ngozi nyeupe yoyote itakayokuja kuwapigania"

Amen.
Mabeberu gani na wewe? Japan ni mmoja wa wadau wa maendeleo Africa. Miradi mingapi hapa Africa imejengwa kwa hisani ya Japan?.Hivi kwanza Beberu ndo nani ? Kwa hiyo sisi ni majike wanatupanda sio? Huoni hili jina linawakuza zaidi ? Haijalishi mkutano unafanyika wapi,cha muhimu ni kinachojadiliwa kwa maendeleo ya nchi yetu.
Tusijifanye tunajua sana,lazima tujifunze kwa walio juu yetu kimaendeleo.
 
Kwame Nkurumah alipinduliwa kwa sababu alitaka kubadili katiba ili awe Rais wa maisha. Hapo ndo alikosea.
Sasa Magufuli hajataka kubadili katiba.
Kupinduliwa siyo rahisi,lazima kuwe na sababu.
Hizi habari umezitoa wapi? Alipinduliwa kwa kusaidiwa na CIA nenda ka research tena dada na wala si suala la katiba
 
Hizi habari umezitoa wapi? Alipinduliwa kwa kusaidiwa na CIA nenda ka research tena dada na wala si suala la katiba
Nilisoma mahali. Nkwame alitaka kuwa Rais wa maisha ndo maana akapinduliwa.
 
🤣🤣🤣🤣🤣 Haaaaaaaa, nimecheka leo, kuliko siku zote humu jf.
Hahhahhah. Halafu wamekazana kuwaita mabeberu mabeberu. Kwanza hawaoni wanajidhalilisha wenyewe ? Kwanza aloanzisha hili jina ana inferiority complex ya ajabu kabisa. Yaani Mpaka kuwaita hivyo alijiona yeye ni Jike hivyo Anastahili kupandwa na Beberu.
 
That's very true, Auntie.🙏🏻🙏🏻
 
Hizi habari umezitoa wapi? Alipinduliwa kwa kusaidiwa na CIA nenda ka research tena dada na wala si suala la katiba
Unajua alijidhibitisha kama Rais wa maisha. Alifunga watu waliompinga,inshort alikuwa dictator. Ndo maana hata ilikuwa rahisi kumwangusha maana watu waghana viongozi wenzake walikuwa hawampendi sababu ya udictator wake.
 
Nilisoma mahali. Nkwame alitaka kuwa Rais wa maisha ndo maana akapinduliwa.
Hapo uliposoma ulipotoshwa. Aliyempindua alikua mwanajeshi aliyekwisha fukuzwa sababu alihisiwa kuplot mapinduzi mwaka 1965. Akawa akifanya kazi kwenye bank. Lakini ali organize mapinduzi kwa kusaidiana na wanajeshi wengine na msaada wa CIA wakati Kwake akiwa Vietnam safarini kuelekea China nyuma kukafanyika mapinduzi. Walipofanikiwa kuipindua wakamweka Lt General aliyeondoshwa kazini kuwa rais mpaka mwaka 1969 alipolazimishwa kujiuzulu kwa scandal
 
Hapana sijapotoshwa. Nimesoma sehemu nyingi tu. Nkurumah alikuwa dictator alijidhibitisha kama Rais wa Maisha. Alifunga waliompinga. Ndo maana ikawa Rais kwake kupinduliwa.
 
Back
Top Bottom