Rais Magufuli kutua Bukoba kesho Jumapili, kuhutubia wananchi Jumatatu

Kesho tarehe 01/01/2017 rais magufuli atawasili mjini bukoba kwa ziara ya kikazi na kuwapa pole wahanga wa tetemeko la ardhi atahutubia wananchi tarehe 02/01/2017 SAA tano asubuhi .

Karibu bukoba tupate na rambi rambi zetu.

Hotuba za Magufuli zinachosha, I swear hakuna jipya mtakalolisikia, ni yaleyale aliyoyasema Dodoma, Kigamboni, Mwanza, Singida.
Kind of a borer
 
Hapo ndipo utajua ni jinsi tulivyo wanafiki. Watawageuzia kibao waliolaumu kutofika Bukoba mpaka leo ....!!!

Tangu tetemeko litokee Bukoba ni muda gani umepita ?..

Kipi kilimzuia kwenda kwa Wananchi wake waliokubwa na janga baya kabisa kama Raisi wa Nchi ?

Kiongozi anatakiwa kuwa mfano kwa sababu ametangulizwa mbele na waliompa mamlaka ,siamini ktk kiongozi anae tekeleza wajibu wake kwa kusukumwa/kulazimishwa kwa namna yeyote ile..

Ndugu zanguni wa Bukoba hakikisheni mnaonyesha mfano,msikubali kuchunguliwa kama Watoto wadogo.
 
Kuna watu walijaza wananchi taarifa za upotoshaji juu ya suala la dangote ila alipojitokeza rais akaeleza ukweli wale watu niliwaoba ni malofa na wpmbavu.
Hata kwenye hili la kagera hopefully ukweli utawekwa wazi na kuna watu lazima watanuna tena.

Ukweli upi zaidi ya huu tulio uona kwa vitendo vya dhahiri ,mwaka mmoja unaenda kutoa pole ya nini sasa kama huo sio unafik tu !!!..
 
Ni bora tu wana Kagera wasijitokeze. Miezi minne baadaye tena baada ya shinikizo kubwa hapa jamii forums. Na pesa zao bilioni 16 walizochangiwa kishazikwapua.
Wanafiki mtaaibika mwaka huu. Kazi kushinda na mafisadi tu
 
cc tumeenda ufaransa kwa mapumziko ya kuupokea mwaka mpya, atawakuta tu waamiaji
 
Sasa waTz tulivyo na mambo ya siasa yalivyo jamaa akifika atapondea sana watu waliokuwa wanasema haendi alafu umati utampigia makofi sana na kumshangilia mnooo! Watasahau kabisa kama jamaa aliwachunia walipokuwa wanamuhitaji hasa na sasa wamenyoosha maisha yao ndio anaenda.

Na kama ilivyo ada wataimba nyimbo lukuki za kumtukuza, asante sana ulaghai wa siasa na uzuzu wa wa-bongo
Si mlisema haendi na mkaanza kulaumu sana? Sasa anaenda sijui mtajificha wapi enyi bavicha wanafiki
 
Wahaya kaeni majumbani kwenu.
Mgeni wetu tutamkaribisha na wala hamna sababu ya kutuelekeza cha kufanya.na hapa naomba apokee ujumbe huu:
Rais ni Magufuli,karibu kwetu Mgeni,
Wenye wivu wafeli,Mapokezi yawe medani,
Tule ndizi na ugali, samaki na akamwani,
Karibu sana Mgeni,Ujisikie nyumbani

Nasaha tunasubiri,majanga kutuepusha
mabadiliko si siri ,Kagera yametukumba
Tumebaki kufikiri,janga njaa lanyemelea
Karibu sana Mgeni,Ujisikie nyumbani

Mito imekauka,maji sasa ni shida
mnyauko usiseme,Ndizi ni historia
tetemeko limepita,wahanga tunahangaika
Karibu sana Mgeni Ujisikie nyumbani
 
Ni bora tu wana Kagera wasijitokeze. Miezi minne baadaye tena baada ya shinikizo kubwa hapa jamii forums. Na pesa zao bilioni 16 walizochangiwa kishazikwapua.
Yaani wakati mwingine unajiaibisha sana kwa hiyo mlikuwa mnaandika humu ili akienda mseme ni kwa sababu ya nyie chagadema
 
Umati wa watu utakaojitokeza kesho utapeleka kilio kwa mafisadi.

Wananchi wako tayari kubadili katiba na kumruhusu magufuli awe rais wa milele ili kuyaangamiza kabisa mafisadi wa ufipa.
 
Back
Top Bottom