abagabo
Senior Member
- Jun 4, 2014
- 155
- 168
Wana jamvi, muda huu nipo ndani ya manispaa ya Bukoba. Kuna matangazo yanapitishwa kwenye mitaa ya mji huu yakihusisha ujio WA Magufuli mjini hapa kesho, na kuhutubia Jumatatu kuanzia saa tano hadi saa saba.
=======
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli anatarajia kuwasili Bukoba Kesho Januari mosi mwaka 2017 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili akitokea mkoani Geita.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo DISEMBA 31 MWAKA 2016 na mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jeneral Mstaafu Salum Kijuu imebainisha kuwa Rais Magufuli atatembelea maeneo mbalimbali yaliyoathiriwa na tetemeko la ardhi na baada ya hapo atahutubia mkutano wa hadhara utakaofanyika mjini Bukoba.
Hii itakuwa ni ziara yake ya kwanza kuifanya mkoani Kagera tangu achaguliwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.