Rais Magufuli kutembelea Temeke zazua taharuki, barabara zaanza kutengenezwa usiku na mchana

Kumbe barabara ni kwaajili ya viongozi na siyo wananchi na viongozi wao
 
Hizo bara bara zipo nje ya TZ?
 
bora wangenipa mimi ile kazi...
Kuna baadhi ya washenzi wana vyeo humo lakini hawana protocol za kiutumishi kabisa + maadili. Bogus kabisa!
 
Nilipomuona tu DC wa Temeke Gondwe yuko busy Kujifanya anatembelea Watu, anasikiliza shida zao, anafoka mbele ya Media huku akiitatua Changamoto zao ila Uso wake ukiwa umejaa Unafiki mtupu nilihisi kuna Jambo linaloendelea huko Temeke.

Asichokijua tu DC Gondwe ni kwamba Bosi wake ana aina mbili ya Wanyetishaji wake wale wanaojulikana na wengi wa Jengo Tai Oysterbay Makao na wale wengine wa Kificho hivyo tayari Mzee ( Boss ) wake ana Taarifa za Kutosha za huko Temeke kuliko zile alizonazo Yeye ( DC Gondwe )

Huwa nachukia mno Uwajibikaji huu wa Kinafiki na wa Kusubiria au Kuvizia hadi Mkubwa afanye Ziara yake mahala husika ndipo Maendeleo nayo yanaanza Kufanywa ( Kufanyika )

Upuuzi mtupu...!!!
 
Hayo masaa yakishaisha ndio kila kitu kinakua sawa? Kwanza kahatarisha usalama wa nani hadi Hayo masaa 48 yatumike?
 
Watumishi wa umma wana haki zao, tofauti na mahausigeli mnaowatesa huko majumbani. Mnawatumikisha kingono na mishahara hamuwalipi kwa wakat et mnawatunzia.
 
Mjinga na mpumbavu nibwewe unayetetea wanya ujinga, kuna wajinga hawawajibiki hadi wasikie rais anakuja.
Elimu sasa hivi ni bure, rudi shule ukajifunze kuandika, ukiweza uje ujadiliane na wanaume hapa jukwaani.
 
Barabara za dmdp kwa temeke no kichefuchefu!! Very poor design, mfano barabara ya temeke mwisho sokota, Machinjioni chang'ombe na kwingineko kwa dmdp no shida!! Mhandisi mshauri aangaliwe kwa kutotumia utaalamu!! Karuhusu uwekaji wa chuma katikati ya barabara ilihali akijua hazina rust protection na zitagongwa na pia kuoza chini ya mwaka mmoja!! Huu no ushauri mbovu sana!! Aje ajifunze Shekilango road!! Same scope
 
Sababu ni simple: watanzania tumejenga tabia na utamaduni wa uzembe na ubabaishaji, vimetukaa sana kiasi kwamba tunaona hayo ndiyo maisha ya kawaida. Watu hawafanyi kazi bila kusukumwa, watu wako maofisini kupiga madili tu, siyo kufanya kazi. Hayo ndiyo maisha yetu na umekuwa ndiyo utamaduni wetu. Bila sisi wenyewe kubadilika, tutaendelea kumlaumu Magu, na mwishoe atatuacha hivyo hivyo tuendelee na ubabaishaji wetu. Too bad 😢
 
kwani barabara zinazojegwa za kuhudumia kuku?
Shida ni uelewa wako mdogo. Kwanini mnasubiri ujio wa Rais ndio muanze kutengeneza barabara? Mnajua Rais akija atawasambaratisha. Hiyo tabia ya kivivu ndio inaligharimu hili Taifa. Wachache sana wako proactive. Wengine ni kuhudhuria kazini hawajui hata wanafanya nini. Wanasubiri mkubwa aje ndio wanahangaika. tabia mbaya sana hiyo
 
 
Aje aone,kata mbagala, uwanja umenunuliwa kwa pesa nyingi, ijengwe sekondari ya kata, hadi leo kizungu mkuti, wataalam wanasema hapafai kujengwa shule eneo hilo,manispaa Temeke waliponunua hawakujua hilo.!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…