Basi usipende kukurupukia hoja zinazozidi uwezo na weledi wakoSiwezi kujibu upumbavu! Huo peleka mkajadili kwenye vikao vyenu vya ndani
Wewe labda ni mtoto mdogo. Baada ya vita na Uganda April, 1979, Nyerere alituambia tufunge mkanda miezi 18 lkn haikuwa hivyo hadi leo miaka 40.Uchumi wa Zimbabwe siyo kama wa Tanzania, wao ni wa mashamba makubwa na kununua vyakula kwenye supermarket. Sisi wetu unaendeshwa na wakulima/wafanyabiashara wadogo wadogo, tunanunua vyakula magengeni kwa hiyo siyo rahisi mtu kubonyeza kutufe akiwa huko na kuuzima uchumi wetu.
Wewe labda ni mtoto mdogo. Baada ya vita na Uganda April, 1979, Nyerere alituambia tufunge mkanda miezi 18 lkn haikuwa hivyo hadi leo miaka 40.
Kabla ya hivyo vita uchumi wetu ulikuwa juu ya ule wa Kenya na hata sarafu yetu pia ilikuwa juu ya ile ya Kenya. Kumbuka wazungu walimshauri Nyerere akishamfurumisha Amin kwenye ardhi yetu aachane naye lkn Nyerere alikaidi na hadi leo , we're still paying the price.
Kwa akili yako, usifikiri tunaweza kusimama mbele ya vikwazo vya wazungu. Hapo mnajifurahisha tu na story za vijiweni.
Mugabe hakuwa na mvuto ndio maana walimsusia.Huyo ameona ajinyoshe tu huko, China hamna lolote kabisa kwa maana halisi ya uwekezaji.
Mugabe alipotiliwa ngumu na wazungu naye alihamia huko akifikiri wangeweza kumsaidia lkn yaliyofuata ni kilio na simanzi. Zimbabwe ilipigwa nuks ya milele.
Hivyo mkiona na Magufuli naye eti anaenda huko, kisa wazungu wamemchunia kwa utawala mbovu, basi mjue ndio mwanzo wa kuuwa uchumi wa Tanzania. Time will bear me a witness.
Mbona unamdhalilisha Msanii Mkubwa.China kitaleta imani ya wafanyabiashara wa China, hivyo Tanzania itakuwa kwenye nafasi ya kunufaika zaidi
Tanzania imekaa kwenye nyonga ya Afrika ambako China inaweza kunufaika zaidi,”
Naukumbuka huu wimbo wa yule mvuta bangi wa Temeke wa Mgambo wanavyoruka na kukanyagana!!!!!! .
Nchi za kiswahili dawa yake ni kutosikiliza miluzi ya pembeni katika uongozi ili mradi unafanya kwa maslahi ya nchiYaani kuna watu washachukia hii safari. ..
Na sio ajabu ndio hao hao walikuwa wakimbeza jamaa kwanini hasafiri nje.
Sisi ni wa kipekee!
Sent using Jamii Forums mobile app
Hichi ndicho tunajidanganya kusema kwamba Magufuli anafanya makubwa wakati kiukweli amevurunda. Mwalimu Nyerere mbona hakuwa na uzoefu wowote ule lakini miaka yake kumi ya mwanzo alifanya vizuri sana kwenye diplomasia kuanzia ngazi ya kanda hadi dunia.Ni kweli kwamba tumefanya makosa fulani fulani katika nyanya za kidiplomasia lakini pia we have made some breakthroughs.Makosa mengine yameletwa na kukosa uzoefu,hata hivyo nafurahi kukiri kwamba tumejifunza pakubwa na bado tunaendelea kujifunza.Ziara hii ya China ni out of realization that we cannot go it alone,ni lazima tujenge mahusiano na mataifa mengine,lakini yale tu ambayo yatakuwa development partners wazuri.Sio siri kwamba mataifa ya magharibi sio development partners wazuri na yanaporomoka kiuchumi,not by chance,but by design.Kwao win win situation is a taboo,and this is unacceptable.
Mkuu,the World Economic Powehouse is "being moved" East and this trend is irreversible.So it makes sense sisi kuji-align na mataifa ya mashariki.Kwa hiyo Magufuli kuji-identify na Beijing is quite correct.I hope trend hii ya kujenga mahusiano na mataifa mengine rafiki zitaendelea.Hatupati faida yeyote by living in isolation,infact we loose.
Hichi ndicho tunajidanganya kusema kwamba Magufuli anafanya makubwa wakati kiukweli amevurunda. Mwalimu Nyerere mbona hakuwa na uzoefu wowote ule lakini miaka yake kumi ya mwanzo alifanya vizuri sana kwenye diplomasia kuanzia ngazi ya kanda hadi dunia.
Upuuzi ni kuamini kwamba mahusiano na mataifa ya mbali ni muhimu kuliko mahusiano na majirani. Raisi angeanza kwanza kujenga hapa nyumbani hasahasa na Wakenya, Wakongo, Waganda, Wamozambique na Wazambia hata kama ni washindani wetu kibiashara. Hawa majirani hawaepukiki hata kam hatutawapenda. Kutaka kuleta ushindani kana kwamba tuko kwenye Mercantile Europe ni utoto.
Suala jingine ambalo mnajifanganya ni kudhani kwamba Uchumi wa dunia ikihamia Mashariki basi Magharibi ndiyo kutaanguka. Nachelea kusema kwamba tunajidanganya sana na pengine mtazamo wetu wa dunia siyo mpana. Msingi mkubwa wa Uchumi wa nchi za magharibi ni mtaji "Capital". Ubepari wa Karne ya 21 unashuhudia hatua ya tofauti kabisa ambayo mitaji inakuwa mikononi mwa makampuni na taasisi za kibiashara na siyo Serikali.
Sasa hapa duniani, hakuna sehemu yenye makampuni na taasisi za kibiashara zenye nguvu kama nchi za Magharibi. Uchumi wa Uchina na nchi nyingi za Asia tokea mwaka 1979 umeendeshwa sana na makampuni binafsi ya Magharibi. Kama ilivyo Silicon Valley kule Marekani, basi Shanghai nako kuko hivyo hivyo, kumejaa makampuni ya teknolojia ya Marekani na Ulaya. Mpaka leo hii, dunia bado inategemea sana teknolojia kutoka makampuni ya Magharibi.
Kikubwa zaidi ni kwamba taasisi za nchi za Magharibi mbali na ujinga mwingi wa wazungu, huwa zinaaminika sana kwasababu zinaendeshwa kwa sheria tena na mataifa mengi. Taasisi kubwa za Asia kama The Shanghai Cooperation na Asia Infrastructure Development Bank zinaendeshwa na serikali ya Uchina ambayo kwenye rekodi ya dunia ni taifa ambalo halina hulka ya kuheshimu utawala wa sheria. Unahisi watu wataziamini kirahisi tu ???
Sema Uchina ninachowapendea ni kwamba angalau wanakuwa na heshima na hawapeleki pua zao kwenye siasa za nchi za watu na mikopo yao ina unafuu wa hali ya juu kuliko. Wazungu huwa wanaangalia sura, nchi za Afrika wanazifanyia umafia sana tena wanaleta dharau kubwa. Lakini mbali na haya yote kwa dunia hii ya sasa tutakuwa ni wajinga kama tutasema tunaegemea tu Asia kwasababu Magharibi kunaanguka.
Tujitathmini upya, Uchina wanaweza kuwa wa kwanza lakini hili halimaanishi kwamba Magharibi ndiyo kutapoteana kabisaa. Uchumi wa dunia umefungamana sana kipindi hiki kuliko wakati wowote ule, hivyo hata kama Uchina na Marekani wanashindana sana, kuna sehemu nyingi sana wanaongea lugha moja.
chige, JokaKuu, Consigliere
Umafia uko hadi Uchina, sema wao wanatumia njia nyingine kuufanya. Nakuhakikishia hakuna taifa duniani linalofanya biashara kwa hasara au kutoa sadaka. Sehemu kubwa ya matatizo ya Afrika kwa kipindi hiki siyo wazungu bali ni Waafrika wenyewe, miaka 10 baadae Mungu akitujalia uzima baada ya kuegemea Mashariki tutakuja kuligundua hili."Sema Uchina ninachowapendea ni kwamba angalau wanakuwa na heshima na hawapeleki pua zao kwenye siasa za nchi za watu na mikopo yao ina unafuu wa hali ya juu kuliko. Wazungu huwa wanaangalia sura, nchi za Afrika wanazifanyia umafia sana tena wanaleta dharau kubwa." Well said,and
this is why we are moving East!Tunataka heshima,na umafia wao hatuutaki.
True Mimi niliishi Zim for 4 years ni wapenda supermarket sana haoUchumi wa Zimbabwe siyo kama wa Tanzania, wao ni wa mashamba makubwa na kununua vyakula kwenye supermarket. Sisi wetu unaendeshwa na wakulima/wafanyabiashara wadogo wadogo, tunanunua vyakula magengeni kwa hiyo siyo rahisi mtu kubonyeza kutufe akiwa huko na kuuzima uchumi wetu.
Wewe unaaangalia haya mambo kwa juu juu sana ndiyo maana unakuja na maelezo kama haya, umejiuliza kuhusu IMF na WB kukataa kumkopesha nyerere. Umejiuliza kwanini walikataa kumkopesha fedha kujenga bwawa la umeme mto la rufiji? kumbuka kipindi hicho hakukuwa na China yenye misuli kama sasa.Wewe labda ni mtoto mdogo. Baada ya vita na Uganda April, 1979, Nyerere alituambia tufunge mkanda miezi 18 lkn haikuwa hivyo hadi leo miaka 40.
Sababu za uchumi kuwa mbaya ni mjumuisho wa mambo mengi miaka ya kati ya sabini. kulikuwa na ukame ulioikumba afrika ya mashariki, pia kulikuwa na uhaba wa mafuta (oil embargo), kuanguka kwa jumuiya ya EAC na hatimaye vita ya Kagera, ukichanganya na fitna za mabeberu, mambo yalikuwa si mambo wakati ule.Kabla ya hivyo vita uchumi wetu ulikuwa juu ya ule wa Kenya na hata sarafu yetu pia ilikuwa juu ya ile ya Kenya. Kumbuka wazungu walimshauri Nyerere akishamfurumisha Amin kwenye ardhi yetu aachane naye lkn Nyerere alikaidi na hadi leo , we're still paying the price.
Mambo yamebadilika sana siku hizi, hivi ulitengemea Tanzania kuweza kufanya upasuaji wa moyo? Ulitengemea kuwa na treni ya umeme? Wasomi wameongezeka, teknolojia na biashara pia zimekuwa na uchumi kwa nchi za kiafrika na Asia umekuwa sana, hivyo siyo lazima kutegemea tena kila kitu kutoka Ulaya. Nyerere hakuwa na jinsi lakini sasa kuna mbadala.Kwa akili yako, usifikiri tunaweza kusimama mbele ya vikwazo vya wazungu. Hapo mnajifurahisha tu na story za vijiweni.
,vita vya ukombozi kutumia pesa na nguvu zetu kwenda kuwakomboa majirani zetu wangeachwa wapambane na hali zao,
Wakoloni wangewaachia wachagga nchi tungekuwa mbali sana kuzidi Kenya.Ule mpango wa kumuachia Chief Marleare sijui kwann walibadili mawazo wakamwachia ticha.
Sawa Lumumba,this means ni busara tuka emulate miracle ya China kuliko ya nchi za magharika,a miracle which is now backfiring,jambo ambalo linaonyesha wazi kwamba all is not well.Lumumba tuache kuimba parrot songs ambazo nchi za magharibi wametufundisha na ambazo hazina ukweli wowote just because they are afraid that the cake will be taken away from them.Hakuna ubaya wowote wa Wachina,tuchukue mikopo yao,ila tulipe.Dawa ya mkopo wahenga walisema ni kulipa.Umafia uko hadi Uchina, sema wao wanatumia njia nyingine kuufanya. Nakuhakikishia hakuna taifa duniani linalofanya biashara kwa hasara au kutoa sadaka. Sehemu kubwa ya matatizo ya Afrika kwa kipindi hiki siyo wazungu bali ni Waafrika wenyewe, miaka 10 baadae Mungu akitujalia uzima baada ya kuegemea Mashariki tutakuja kuligundua hili.
Matatizo ya Tanzania na Afrika kwa ujumla hayawezi kusuluhishwa na nchi za Magharibi au Mashariki. Katika hili nasema lazima tujitathmini sanaa. Uchina mwenyewe aliligundua hili mapema akaachana na michezo ya kulalia Eastern Bloc pekee.