Rais Magufuli kutembelea China

Rais Magufuli kutembelea China

Swali la Civics,

Taja Rais wa KWANZA Duniani ambaye hakuwahi kusafiri / kufanya ziara nje ya Nchi kipindi chote Cha miaka kumi cha Uongozi wake___________________
 
rais wa china ataongea kichina sijui mandarin na wetu kiswahili..genius move
 
Mnafikiria kununua tu huko nje na siyo kuuza! Hiyo shilingi inapandaje sasa we taahira?
Sasa wewe mbumbumbu Tanzania inatengeneza vipuri gani vya mashine? Taja kiwanda hata kimoja ili tununue Tanzania badala ya kuagiza toka huko nje
 
Sasa wewe mbumbumbu Tanzania inatengeneza vipuri gani vya mashine? Taja kiwanda hata kimoja ili tununue Tanzania badala ya kuagiza toka huko nje
Kwamba nchi zote duniani zinabadilishana vipuri vya mashine tu we mwendawazimu? Siyo bure mmerogwa nyie
 
Kwamba nchi zote duniani zinabadilishana vipuri vya mashine tu we mwendawazimu? Siyo bure mmerogwa nyie
Nazungumzia Tanzania siwezi kua mwendawazimu kuzungumzia nchi zote duniani wakati ninaishi Tanzania aisee ungejibu swali la kiwanda cha vipuri vya printer, caterpiller, ndege, magari ili vinunuliwe hapa hapa itakua jambo jema sana
 
Nazungumzia Tanzania siwezi kua mwendawazimu kuzungumzia nchi zote duniani wakati ninaishi Tanzania aisee ungejibu swali la kiwanda cha vipuri vya printer, caterpiller, ndege, magari ili vinunuliwe hapa hapa itakua jambo jema sana
Siwezi kujibu upumbavu! Huo peleka mkajadili kwenye vikao vyenu vya ndani
 
Hahahaha chige jamaa yetu anaenda Uchina bwana. Angemsikiliza Jakaya mapema na kutokuleta unazi usio na mantuki leo hii asingefika hapa. Ooh bandari Bagamoyo blah blah, oooh SGR iende Kigali. Sasa wachina wameshajua ana shida, watamminya huko.
 
Nimekuwa nasubiri ziara ya Rais Magufuli China kwa muda mrefu,to me this is a dream come true.Natamani akitoka huko apitie Tehran and may be Moscow as a slap in the face to Western countries especially Washington.
Fuata link ifuatayo for more imformation.


=======


Rais Dk. John Magufuli kwa mara ya kwanza anatarajiwa kuvuka mipaka ya Bara la Afrika, kwa kuitembelea China kwa ziara ya kiserikali, Gazeti la JAMHURI limebaini.

China imekuwa mdau muhimu wa maendeleo wa Tanzania, kupitia mkakati mahususi wa Tanzania ya viwanda, wawekezaji kadhaa kutoka nchi hiyo ya barani Asia wameitikia wito kwa kuanzisha viwanda kadhaa hapa nchini.

Vyanzo vyetu vinasema ziara hiyo ya Rais Magufuli imekuja wakati mwafaka, ambapo China na Tanzania zinahitajiana zaidi kimkakati. Tanzania inaihitaji China katika mkakati wake wa kujenga viwanda na kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa kati kufikia mwaka 2025.

“Unajua China ni rafiki wa kweli…kuna hatua ambazo amezichukua Rais Magufuli za kuwadhibiti wanyonyaji wa rasilimali zetu zimewakera wadau wa maendeleo kutoka Bara la Ulaya.

“Ziara yake nje ya mipaka ya nchi kuanzia China, inapeleka ujumbe mzito sana, hiyo inanikumbuka miaka zaidi ya 40 iliyopita ambapo Mwalimu Julius Nyerere alikwenda China kukutana na Mwenyekiti Mao.

“Kitendo cha Rais Magufuli kuanzia huko kinaleta hisia kali zaidi, maana ni dhahiri kwamba wote tunahitajiana, China inahitaji kuwekeza viwanda vyake Afrika na Tanzania imekaa kwenye nyonga ya Afrika ambako China inaweza kunufaika zaidi,” kinasema chanzo chetu.

Baadhi ya Watanzania waishio China wameliambia Gazeti la JAMHURI kwamba kitendo cha Rais Magufuli kufanya ziara nchini China kitaleta imani ya wafanyabiashara wa China, hivyo Tanzania itakuwa kwenye nafasi ya kunufaika zaidi.

Akizungumza na JAMHURI, mmoja wa Watanzania wanaoishi jijini Beijing, Salum Khamis Hussein, amesema nchi kama Tanzania ambayo inahitaji kukua kiviwanda pamoja na utekelezaji wa miradi mikubwa, inahitaji kuwa karibu zaidi na China.

“Tanzania inahitaji kuwa karibu zaidi na China, maana mambo mengi yanayofanywa na Rais Magufuli tunaona dhahiri namna yanavyoyakera mataifa ya Magharibi, mshirika wa kweli wa maendeleo ya Afrika kwa sasa ni China, japo tunatakiwa kujua namna ya kushirikiana naye.

“Zipo propaganda nyingi kuhusu China, hasa kwenye miradi, tumesikia kuhusu Zambia kwamba China sasa inaendesha migodi, Kenya nako tunaambiwa China wanataka kuendesha Bandari ya Mombasa, lakini ukweli ni kwamba tunawahitaji na wao wanatuhitaji, hivyo tunahitajiana,” anasema Salum.

JAMHURI limezungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, ambaye hakutaka kuzungumzia ziara hiyo isipokuwa kusisitiza kwamba huu ni mwaka wa uwekezaji.

Waziri Kabudi alisisitiza kuhusu kauli ya Rais Magufuli katika hafla ya kufungua mwaka wa mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini (Sherry Party), kwamba, mwaka 2019 ni mwaka wa uwekezaji. Hotuba hiyo ya Rais Magufuli imechapishwa katika kurasa za katikati za gazeti hili.

Kwa kuzingatia kauli hiyo ya “mwaka 2019 ni mwaka wa uwekezaji” JAMHURI linafahamu kuwa China imekuwa katika mipango ya kuwekeza viwanda 200 hapa nchini.

“Hilo (safari ya China) siwezi kulizungumzia. Ninachoweza kusema ni kwamba, kama alivyosema Mheshimiwa Rais katika ‘Sherry Party’ huu ni mwaka wa uwekezaji. Jambo jingine ninaloweza kusema ni kuwa uhusiano na ushirikiano wetu na nchi mbalimbali ni mzuri,” amesema Waziri Kabudi ambaye ameteuliwa kuongoza wizara hiyo hivi karibuni akitokea Wizara ya Katiba na Sheria.

JAMHURI limemtafuta Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, ambaye hakuwa tayari kuzungumzia ziara hiyo ya Rais Magufuli nchini China, akisisitiza kuwa suala hilo halijafika ‘mezani’ kwake, kwa hiyo si busara kulizungumzia.

Katika hali isiyo ya kawaida, hata watendaji wengine kadhaa wa serikali wamekuwa wazito kuzungumzia ziara hiyo, na miongoni mwao, wameshindwa hata kuzungumzia fursa za uwekezaji zilizopo kati ya China na Tanzania.

Safari hiyo ya Rais Magufuli nchini China itakuwa ya kwanza nje ya Bara la Afrika tangu aingie madarakani Novemba 5, 2015.

Rais Magufuli ataelekea China katika wakati ambao ujazo wa biashara kati ya taifa hilo na Tanzania unatajwa kufikia dola za Marekani bilioni 4.6, takriban Sh trilioni 10.3, kwa hiyo ziara yake inatajwa kuinufaisha Tanzania kupitia sera ya mambo ya nje ya diplomasia ya uchumi.

Rais Magufuli binafsi amewahi kusikika akiisifu China kwamba imekuwa ikitoa mikopo ambayo si tu ni yenye riba nafuu, bali pia isiyo na masharti ya ‘ajabu’.

Hali ilivyo

Oktoba mwaka jana China ilisherehekea miaka 69 tangu kuundwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, siku ambayo huadhimishwa Oktoba Mosi, kila mwaka na katika shughuli hiyo, Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki, aliwaeleza waandishi wa habari mambo ambayo Tanzania inajivunia kutokana na uhusiano wake na China kwa zaidi ya miongo minne, akisema miongoni mwa mambo hayo ni yale ya kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Kwa mujibu wa balozi huyo, kihistoria China iliiunga mkono Tanzania katika harakati za ukombozi wa mataifa ya kusini mwa Afrika na Tanzania kuongoza harakati za kuiwezesha Jamhuri ya Watu wa China kutambulika katika Umoja wa Mataifa na kuwa mwanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama.

Alisema Tanzania ni miongoni mwa mataifa yaliyonufaika na misaada ya China tangu miaka ya 1960, na miongoni mwa manufaa hayo ni Reli ya Uhuru (Tazara) iliyojengwa kwa mkopo usio na riba kutoka China, ukiwa ni mradi mkubwa wa kwanza kufanywa na China nje ya mipaka yake.

Alieleza kuwa Tanzania pia imekuwa ikinufaika na misaada ya China katika sekta ya elimu na afya na kwamba, kwa miaka 50 sasa China imekuwa ikituma madaktari wake kufanya kazi nchini huku maelfu ya Watanzania wakipata fursa ya mafunzo nchini China.

Balozi huyo anaamini kuwa Tanzania inaweza kunufaika zaidi na China katika maeneo mengine kadhaa yakiwamo ya utalii, kilimo na uwekezaji katika viwanda.

Takwimu zinabainisha kuwa miradi mipya isiyopungua 196 imesajiliwa nchini katika sekta za viwanda, makazi, kilimo na uvuvi, na ujazo wa kibiashara kati ya China na Tanzania ukitajwa kufika dola za Marekani bilioni 4.3 kwa mwaka.

Katika moja ya mikutano ya jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika, China ilikwisha kutangaza kutenga dola za Marekani bilioni tano kununua bidhaa kutoka Afrika, hatua ambayo inatajwa kuwa ni fursa nzuri kwa Tanzania.

Rais Xi Jinping Dar



Machi, 2013, Rais wa China, Xi Jinping, alifanya ziara nchini Tanzania kwa mwaliko wa mwenyeji wake, Jakaya Kikwete, na mataifa haya mawili kutia saini mikataba 17 ya ushirikiano.

Mataifa haya mawili uhusiano wake umedumu kwa miaka takriban 57 sasa, tangu iliyokuwa Tanganyika na baadaye Tanzania.

Rais Xi kwa wakati huo alifika Dar es Salaam akitokea Moscow, Urusi ambako ndiko alikoanza safari yake ya kwanza katika nchi za nje tangu kuapishwa kwake rasmi kuwa Rais wa China.

Katika mikataba hiyo 17 aliyotia saini Rais Xi, masilahi mbalimbali yaliguswa, yakiwamo ya kiuchumi na utamaduni. Miongoni mwa hayo ni ujenzi wa bandari mpya Bagamoyo pamoja na mtandao wa reli wa kuunganisha na reli nyingine za Tanzania.

Akizungumza Ikulu jijini Dar es Salaam kwa wakati huo, kiongozi huyo wa China alisema ziara yake ni ishara ya uhusiano mwema kati ya nchi mbili hizi, uhusiano ambao umeendelea tangu ulipoanza wakati wa Rais Julius Nyerere na Mao Zedong.

Wachambuzi wa mambo wanaeleza kuwa China inaitazama Afrika kama mbia muhimu katika maendeleo ya kiuchumi, ikilenga kuwekeza katika madini, nishati na miundombinu, lakini pia Afrika ni soko muhimu la bidhaa za China.

Taarifa za mwaka 2013 wakati wa ziara hiyo zilibainisha kuwa China ni taifa la pili katika uwekezaji nchini Tanzania likitanguliwa na Uingereza.



Magufuli na safari za nje

Mwezi Januari mwaka 2017, Rais Magufuli ambaye imekuwa nadra kwake kusafiri nje ya nchi, kwa mara ya kwanza alisafiri nje ya Afrika Mashariki, kwenda Addis Ababa nchini Ethiopia ambako alihudhuria mkutano wa 28 wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU).

Hiyo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kuhudhuria mkutano huo tangu aingie madarakani kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano, Novemba 2015.

Akiwa Addis Ababa, Rais Magufuli alikutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika waliohudhuria mkutano huo, ambao vilevile ulihudhuriwa na Antonio Guterres, akiwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN).

Ni mkutano huo ambao pia ulitumiwa kumchagua mwenyekiti mpya wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU), iliyokuwa ikiwaniwa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Amina Mohammed, mwanadiplomasia Abdoulaye Bathily kutoka Senegal, Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad, Moussa Faki Mahamat, mwanasiasa mkongwe kutoka Botswana, Pelonomi Venson-Moitoi na aliyekuwa wakati mmoja mshauri wa rais wa Equatorial Guinea, Mba Mokuy.



Fursa zaidi China

Gazeti la JAMHURI linafahamu kuhusu kuwapo kwa ongezeko kubwa la wafanyabiashara kutoka Tanzania kwenda China kufanya biashara mbalimbali kama nguo, vipuri vya magari na pikipiki pamoja na vifaa vya kielektroniki.

Biashara ya nguo imekuwa ikichukua nafasi kubwa, na soko la nguo za China nchini limekuwa likikua siku hadi siku, ingawa Rais Magufuli amekuwa na msimamo wa kuhakikisha pamba ya nchini inatumika kutengeneza nguo hapa Tanzania na si kuisafirisha nje ya nchi, kisha Tanzania kuagiza nguo kutoka nje.

Mji wa Guangzhou ni moja ya miji ambayo wafanyabiashara wa nguo wa Tanzania hufika kwa ajili ya kununua na kuleta bidhaa hizo nchini.

Miji mingine ambayo wafanyabiashara wa Tanzania hufika kwa ajili ya ununuzi wa bidhaa za kuuza nchini ni pamoja na Shenzhen.
Kinachomponza Raisi wenu ni kiburi kisicho na msingi wowote ule kabla ya utaalamu. Propaganda dhidi ya Uchina yeye naye alizifanya sana baada ya kuingia Ikulu.

Akaanza kushambulia ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo bila hata kuwa na sababu za msingi. Wenzake wanakusanyika kule Afrika Kusini mwenye mkutano wa BRICS yeye kiburi tu, SINO-AFRICAN FORUM yeye kiburi tu. Sasa mambo yanaanza kuwaka moto huku nyumbani kwake ndiyo akili zinaanza kumuingia. Hivi angekuwa ni mtu wa kusikiliza unadhani angefika hapa alipofika leo ? Ujehuri bila maarifa ni anguko.

Pia lazima muelewe kwamba hata akienda Uchina bado atahitaji kujenga mahusiano mazuri na mataifa ya Magharibi kwasababu hata Uchina naye anajua bila Magharibi hawezi kuendelea. Hii nchi bwana
 
ITAPENDEZA SANA AKIKWEA PIPA HILI
1552471202113.png
 
Kinachomponza Raisi wenu ni kiburi kisicho na msingi wowote ule kabla ya utaalamu. Propaganda dhidi ya Uchina yeye naye alizifanya sana baada ya kuingia Ikulu.

Akaanza kushambulia ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo bila hata kuwa na sababu za msingi. Wenzake wanakusanyika kule Afrika Kusini mwenye mkutano wa BRICS yeye kiburi tu, SINO-AFRICAN FORUM yeye kiburi tu. Sasa mambo yanaanza kuwaka moto huku nyumbani kwake ndiyo akili zinaanza kumuingia. Hivi angekuwa ni mtu wa kusikiliza unadhani angefika hapa alipofika leo ? Ujehuri bila maarifa ni anguko.

Pia lazima muelewe kwamba hata akienda Uchina bado atahitaji kujenga mahusiano mazuri na mataifa ya Magharibi kwasababu hata Uchina naye anajua bila Magharibi hawezi kuendelea. Hii nchi bwana
Ni kweli kwamba tumefanya makosa fulani fulani katika nyanya za kidiplomasia lakini pia we have made some breakthroughs.Makosa mengine yameletwa na kukosa uzoefu,hata hivyo nafurahi kukiri kwamba tumejifunza pakubwa na bado tunaendelea kujifunza.Ziara hii ya China ni out of realization that we cannot go it alone,ni lazima tujenge mahusiano na mataifa mengine,lakini yale tu ambayo yatakuwa development partners wazuri.Sio siri kwamba mataifa ya magharibi sio development partners wazuri na yanaporomoka kiuchumi,not by chance,but by design.Kwao win win situation is a taboo,and this is unacceptable.

Mkuu,the World Economic Powehouse is "being moved" East and this trend is irreversible.So it makes sense sisi kuji-align na mataifa ya mashariki.Kwa hiyo Magufuli kuji-identify na Beijing is quite correct.I hope trend hii ya kujenga mahusiano na mataifa mengine rafiki zitaendelea.Hatupati faida yeyote by living in isolation,infact we loose.
 
Kumbukeni mchina anacheza rough, how sure are you kuwa hiyo nyonga itabakia salama?
Sioni ubaya wa Mchina,kwa kuwa yeye hana strings attached kwenye mikopo yake tofauti na akina Robin Hood.Jambo la msingi kwake ni kurudisha mikopo yake,na hiyo ndiyo dawa ya mkopo.Mkopo sio Grant mkuu.
 
Katikati ya kutekana na kupigana risasi???... morality and fairness ni ndoto.
Sisi nia yetu kama taifa ni kwenda Kaskazini,halafu wewe unafanya kila juhudi na kutumia kila mbinu kuturudisha kusini,what do you expect.Tukuchekee?
 
Sisi nia yetu kama taifa ni kwenda Kaskazini,halafu wewe unafanya kila juhudi na kutumia kila mbinu kuturudisha kusini,what do you expect.Tukuchekee?
Kama gharama ya safari ya "taifa"kuelekea kaskazini ni ku-eliminate wana wa nchi wanao tofautiana nanyi , safari haitakuwa na mafanikio!
 
Kama gharama ya safari ya "taifa"kuelekea kaskazini ni ku-eliminate wana wa nchi wanao tofautiana nanyi , safari haitakuwa na mafanikio!
Kutofautiana ni kawaida,ila busara na hekima lazima vitumike.Matusi na kejeli havitufikishi popote.
 
Mleta uzi umejitahidi kuremba remba,lakini wapi! Ukweli uko wazi maji yako shingoni. Eti akitoka China apitie Tehran na Moscow, hivi huwa hata mnajisomea kweli au ni kuunga tu mkono hizo juhudi.Iran na Russia wamewekewa vikwazo vya kiuchumi. Iran imeumizwa sana na vikwazo, Russia wana afadhali kidogo lakini mambo ni magumu. Sasa huyo rais wenu apite huko kufanya nini labda? Basi apite na Caracas, Venezuela akaongeza ujuzi wa kuvuruga uchumi na maisha ya watu.
 
Back
Top Bottom