Rais Magufuli Jumapili asali kanisani St. Peter

Rais Magufuli Jumapili asali kanisani St. Peter

Sijaelewa ukisema kanisani kwake..ni kwa vipi kulimiliki au namna gani.kabla alikua anasali kanisa la nani ?
 
Mwalimu Nyerere, aliitambua na kuiheshimu Ikulu kama ofisi. Makazi yake yalikuwa nyumbani kwake Msasani-nyumba aliyojenga kwa mkopo, akaishiwa fedha, na kuamua kuirejesha serikalini. Shughuli za kiserikali, kama dhifa, kuapisha viongozi, kuwapokea viongozi wakuu wa nchi, alizifanyia Ikulu. Msasani pia alikuwa na ki-ofisi kidogo, lakini ambacho yeyote aliyeitwa huko alianza "kuugua" hata kabla ya kujua ameitwa kwa shauri gani.
Kila asubuhi Mwalimu alifika St. Peter kwa ajili ya kusali. Hiyo ilikuwa ratiba yake kwa maisha yake yote. Kwa sababu hiyo, St. Peter pakajulikana na "Kanisa la Nyerere".
Kwa kweli mzee wetu huyu alipaheshimu sana Ikulu ndo maana akasema ni mahali patakatifu. Sina uhakika kama atakuja kutokea mtu mwingine atakayeparudishia hadhi yake! Hili nilikuwa nalisikia sana kwamba kabla hajaanza siku lazima aingie kanisani kusali, ndo nikawa nawaza kwa sauti kwamba aliwezaje kutoka Magogoni mpaka Oyster Bay kusali? Kumbe mzee alikuwa anaishi uraiani? Sasa hawa wa sasa hivi saa ngapi utaliita jamaa lije linajinyeanyea? Maana kama ni ma-deal ya wizi na wewe umeshiriki sasa yatakuogopa saa ngapi? Nasikia enzi za mwl. ukiitwa ofisini lazima utamani ardhi ipasuke hata kama umeitwa kwa jambo la heri tu!!
 
jamani, JP sio laigwani, ni mtumishi wa umma kama walivyo walimu manesi na askari, ya mke wake na wanae yanatuhusu nini? sasa kila mtu akija na mkewe ofisini haiwezi kuwa ofisi tena. mkewe JP ana ajira yake na majukumu ya kifamilia kama munataka kupiga nae picha nendeni kazini kwake mtamkuta.
Haki ya Mungu wewe ni kapumbav tena kataahira! Hapo alipoenda leo ni ofisini/kazini hapo? Una maanisha mama huyo bado ni mwalimu mpaka sasa hivi tunavyoongea? Hivi wewe unajua maana ya first lady? Mburura mkubwa wewe, huyo mama ajira yake ya ualimu ilikoma siku Mh. Magufuli alipoapishwa, unaposema ya mke na watoto hayatuhusu unazidi ukujidhihirisha jinsi ulivyo kagonjwa ka akili. Hao watu wanatunzwa kwa kodi yetu ni haki yetu kufgahamu, kama Mh. Rais hana ndoa atuambie ili tupunguze gharama!!! Tusije kuwa tunalipa watu kumbe ndoa ilishavunjika siku nyingi!!
 
Kwa mtu mwenye ufaham wa psychology nd body language atakubaliana nami kwamba JPM ni mtu flan very humble and down to earth. U can tell a lot by just observing him. Mengine ni weakness za ki binadam. All the best to him. #Amen.
 
Eti njiwa unasemaje kuhusu hii misa takatifu ya magufuli
 
Last edited by a moderator:
Eti njiwa unasemaje kuhusu hii misa takatifu ya magufuli


hahaha sasa mi nitamzuia mtu kwenda kwenye nyumba yake ya ibada ...?? JPM ni mkristo wacha aende kanisani au wataka tuandamane kwanini raisi anakwenda kanisani..????! utakuwa ni upumbavu ! nyerere alikuwa akienda kanisani ... mwinyii alikuwa akienda msikitini,,, mkapa kanisani Fr. JK msikitini... mwache akaombe mungu wake anayemjua yeye... as long as anajua watanzania nini tunahitaji na analifahamu hilo...

mwaka huu kazi tu!

 
jamani, JP sio laigwani, ni mtumishi wa umma kama walivyo walimu manesi na askari, ya mke wake na wanae yanatuhusu nini? sasa kila mtu akija na mkewe ofisini haiwezi kuwa ofisi tena. mkewe JP ana ajira yake na majukumu ya kifamilia kama munataka kupiga nae picha nendeni kazini kwake mtamkuta.
Tia bidii ila kaa ukijua jipu halifichiki
 
Natumai hii ya kusalimia kwaya itakua ya leo tu, siku nyingine ataenda straight kwenye kiti chake kama Nyerere au Ben
 
sababu ya kwenda peke yake badala ya familia nzima ama na mkewe nadhani ni kuondoa attention kwa baadhi ya waumini na kuwaondoa kwenye mood ya kusali na kubaki kuwashangaa, pili kanisa katoliki kutegemeana na makanisa wanayo misa zaidi ya tatu hivyo sio lazima kama rais anaenda misa ya kwanza basi na mke aende katika misa hiyo, kila mmoja na chaguo lake mwingine anaweza kwenda misa ya pili au ya tatu au hata ya kwanza.
 
So what?
What do you mean?
Baada ya zama za Kaswida, tunguli na Machagudoa kupita sasa Ni zamu ya kwaya, bia na kitimoto?
 
Back
Top Bottom