Rais Magufuli hali ya maisha ni ngumu sana, tuonee huruma

Nuaunga mkono hoja ,watu wengi wanalalamika hali ya sasa ngumu hata kabla ya korona
 
Tumia akili kujibu hoja. Tofautisha watalaamu na wakandarasi wazawa.
Works both ways makandarasi ni watu sio mbuzi,na sifa za makandarasi mmoja wapo ni expertise. Tanzania inao makandarasi wengi tu,na wenye sifa kwa kazi lakini hawathaminiwi na watu kama wewe.
Huwezi hata kidogo ukaufikia uchumi wa kati bila kuwashirikisha wananchi.
 
May 22, 2020
Mbarali, Mbeya
Tanzania

Wakulima wa mpunga walia

Shuhudia kinachowakuta wakulima wavunaji wa mpunga bonde la Usangu juhudi zao za kufanya kazi kwa bidii zinaishia patupu kutokana na sera mbovu zisizounganisha miundo-mbinu na maeneo ya kilimo




Source: MbeyaYetuOnlineTV
 
May 16, 2020
MWAMBAO MWA ZIWA NYASA, BARABARA CHANGAMOTO KUANZIA LITUHI HADI CHIWINDI

Changamoto mtandao wa barabara ya mwambao mwa ziwa Nyasa kuanzia Lituhi,Liuli hadi Chiwindi mpakani mwa Tanzania na nchi ya Msumbiji. Wananchi wa Kijiji cha Mtupale kata ya Chiwanda wilaya ya Nyasa mpakani mwa Tanzania na Msumbiji wahaidiwa lami

source : Songea TV
 
Sema Hali yako mkuu Sio Wana nch wakat mm kwa mwezi naingiza million mbili na serekal hii hii kwann niseme maisha magum au unafikir Nan utampa uongozi alafu akawa anakupa pesa acha Mambo ya siasa kushinda jamiforums nenda kafanye kaz
Hakuna ubishi kweli unafanya kazi nzuri, kujenga miundo mbinu, zahanati, vituo vya afya na hospitali. Hakuna ubishi umeinyoosha nchi iliyokuwa imepinda...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna ubishi kweli unafanya kazi nzuri, kujenga miundo mbinu, zahanati, vituo vya afya na hospitali. Hakuna ubishi umeinyoosha nchi iliyokuwa imepinda...
Fanya kweli kwenye sanduku la kura kuondoa ugumu huu bila hivyo mtaendelea kumwomba magu na hali itakuwa mbaya zaidi awamu ya mwisho.
 
Idugunde,

Serikali ya CCM ilivyoharibu uchumi wa nchi, usiombe hisani toka kwa CCM bali fanya kweli kupitia sanduku la kura kwa kuchagua chama tofauti na CCM

December 2019
Zitto akiongea na wananchi Akichambua hali ya uchumi kuelekea uchaguzi 2020


Sanduku LA kura kwa tume IPI?
 
Sanduku LA kura kwa tume IPI?

Pamoja na hali hii ya kweli ya kisiasa nchini lakini ni bora kuendelea kupiga kura ya kuikataa CCM kuliko kuweka tumaini la kupata hisani toka kwa CCM .

Kura kupitia sanduku la kura siku zote hupeleka ujumbe kwa watawala hata kama wakiiba, wakibadilisha matokeo lakini watapata ujumbe.
 
Lockdown ya aina hiyo uliyoielezea hapa ni imagination yenu ya mtaa wa lumumba. Haijawahi kuelezewa au kufanywa na nchi yeyote duniani.

Hiyo ndiyo lockdown mzeee. Hivi unajua kwenye lockdown hata magari binafsi barabarani hayaruhusiwi?
 
Hbr zenu mabibi na mabwana!?, niende moja kwa moja kwenye hoja ya msingi.

Nimekuwa nikijiuliza kwa nini awamu hii maisha yanaonekana ni magumu zaidi na wakati huo lawama zinaenda kwa viongoz, viongoz nao watoa lawama kwa wananchi/vijana.

Mfano mzuri bwana spika anasema vijana ni wavivu hawataki kufanya kazi, kazi yao ni kucheza pooltable,. Dah.!
Viongozi wengine mpaka rais wamekuwa wakisema, nchi hii ina fursa nyingi hivyo vijana wachangamkie fursa hizo badala ya kusubir ajira rasmi.

Vijana nao wanalalamika mishe haziendi, kilimo hakilipi, biashara hazifanyiki, ajira hakuna lawama zote kwa serikali.

Weka wazo lako hapa chini, hatua zipi zinapaswa kuchukuliwa kwa upande wa sisi kama raia lakin pia serikali inapaswa kufanya nini ili kunusuru hali hii tete.!??

Mawazo yangu machache ni haya hapa;

Kwanza kabisa mfumo wetu wa elimu unapaswa kufumuliwa, elimu itolewe ile ya kumuwezesha muhitimu kujiajir mara baada ya kuhitimu masomo yake ya sekondar au chuo.
N.b Masomo ya kilimo, biashara, uchumi, ujasiriamali n.k yatolewe kuanzia sekondari mpaka vyuoni na iwe ni lazima mwanafunzi asome.

Pili, kilimo kipewe hadhi na thamani kubwa.
Thamani ya kilimo ni uhakika wa soko zuri lenye tija au manufaa kwa mkulima wa hilo zao.
Serikali inawajibu wa kutafuta soko nje ya nchi pia kuanzisha viwanda vitakavyo demand zao linalo patikana eneo husika.

Tatu, Namuunga mkono Mbunge msukuma aliposema, ni ajabu kumpa mkopo mtu asome halafu mwisho wa siku anahitimu anapewa karatasi/cheti. Badala yake mbunge ameshauri mikopo itolewe hata baada ya kuhitimu ili vijana wakaanzishe miradi itakayo msaidia yeye pamoja na kulipa deni hslb.


Pamoja na jitihada nzuri za Rais wetu Magufuli lakini bado ni kama vile kuna button haijawa pressed.

Serikali ya Magu inafeli wapi, na nini kifanyike.???
 
Watumishi wakiwezesha mengine unakuja yenyewe hasa walimu
Maana wao wapo hadi vijijini
Imagine ukiongeza mshahara wa mwalimu utakuwa umpeleke tsh ngapi kijijini?
 
Hakuna ubishi kweli unafanya kazi nzuri, kujenga miundo mbinu, zahanati, vituo vya afya na hospitali. Hakuna ubishi umeinyoosha nchi iliyokuwa imepinda...
kwahiyo kumbe mnavyomsifia mnajikaza tu ? unafiki ni kitu kibaya sana !
 
Hakuna ubishi kweli unafanya kazi nzuri, kujenga miundo mbinu, zahanati, vituo vya afya na hospitali. Hakuna ubishi umeinyoosha nchi iliyokuwa imepinda...
Wewe kumbe unamsifia huku unapata shida sana aisee wewe kenge badilika
 
Hakuna ubishi kweli unafanya kazi nzuri, kujenga miundo mbinu, zahanati, vituo vya afya na hospitali. Hakuna ubishi umeinyoosha nchi iliyokuwa imepinda.

Ila hali yetu wananchi ni mbaya sana. Tunaamka asubuhi hatujui kama tutakula au vipi. Tukifungua biashara zinakufa, kila tunachojaribu hakiendi.

Hivyo wewe kama mkuu angalia namna ambavyo utalegeza ili mzunguko wa pesa uongezeke mitaani. Sio kwamba hatutaki kazi bali mzunguko wa pesa ni hakuna kabisa.
Naunga mkono hoja
IMG_20210208_205837_744.jpg
 
Back
Top Bottom