Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,842
- 31,075
Vitabu vyote vya dini vinasema kuwa sisi binadamu wote tuna mapungufu yetu na tunapaswa tunapokosolewa tujitafakari na kukukubali ushauri/ ukosoaji huo
Katika vitabu hivyo hivyo vya dini vinaandika kuwa ni Mungu pekee ambaye yupo 100% perfect
Kwenye nchi yoyote yenye utawala bora, ukosoaji wa serikali "constructive criticism" kutoka kwa wananchi wake kwa serikali yao ni jambo la kawaida sana na linapokekewa kwa nia ya kujirekebisha pale inapokosea
Lakini inashangaza sana kwa mtawala wetu, Rais Magufuli, kuwa hapendi kabisa kukosolewa kwa matendo anayofanya na mara nyingi anawatumbua wale wote wanaomkosoa
Niseme wazi kuwa Rais wetu kwa kutopenda kabisa kupewa "constructive criticism" anafanya kufuru kwa Mungu, kwa kuwa vitabu vyote vya dini vinasema kuwa hakuna binadamu yoyote tokea dunia iumbwe amewahi kuwa 100% perfect
Nitatoa mifano michache kulithibitisha hili ninalolisema:-
Ni hivi Jana tu Rais Magufuli amemtumbua Profesa Mark Mwandosya, uenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mwalimu Nyerere na nafasi yake kuchukuliwa na Stephen Wassira
Ingawa taarifa ya Ikulu haikutaja sababu za kutumbuliwa kwake, lakini hisia za wachambuzi wengi wa kisiasa, wanasema ni kutokana na Profesa Mwandosya kuwa ni mkosoaji mkubwa wa Rais Magufuli kupitia ukurasa wake wa Twitter
Ikumbukwe kuwa ni siku chache zilizopita, Profesa Mwandosya aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa walifundishwa misingi ya utawala bora kuwa Rais anapokusema hadharani kuwa umekosea, unalazimika siku inayofuata upeleke barua yako ya kujiuzulu nafasi hiyo
Ingawa hakumtaja kwa jina, lakini wadadisi wa mambo wamesema ujumbe huo wa Twitter ulikuwa ukimlenga moja kwa moja Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, ambaye siku chache zilizopita, Rais Magufuli aliingilia kati sakata hilo na kumwambia, Mkuu huyo wa Mkoa anapaswa kulipa kodi ya makontena hayo ya shilingi zipatazo bilioni 1.2 ambazo Mkuu huyo wa Mkoa alikuwa anataka kukwepa kulipa
Nimekuwa nikijiuliza hivi Profesa Mwandosya ni nini kosa lake, kuelezea suala "obvious" kama hilo la Mkuu wa nchi kumkosoa hadharani Mkuu wake wa Mkoa wa Dar na mkuu huyo wa Mkoa kuonyesha "kumdindia" Mkuu huyo wa nchi kwa kukataa kujiuzulu??
Suala lingine ambalo lilileta kizaazaa siku za nyuma ni kutumbuliwa kwa Waziri wa Habari wa wakati ule Nape Nnauye, kwa "kosa" la kuunda Tume iliyochunguza tukio la kuvamiwa kwa Clouds media usiku na askari wenye silaha za moto amacho kitendo hicho kilifanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda
Kitu kilichofuata ni kila mtanzania anakijua, ni kwa Waziri huyo wa Habari kutumbuliwa
Nimekuwa pia nikijiuliza hivi kosa la Nape Nnauye lilikuwa nini katika sakata lile la uvamizi wa Clouds media kulikofanywa na askari wenye silaha za moto??
Pengine ni kuunda ile Tume yake ya uchunguzi ambayo hata hivyo yeye asingekuwa ni mwamuzi badala yake hivyo vyombo ambavyo yeye angevikabidhi ndivyo vingeamua hatma ya Mkuu wa Mkoa wa Dar
Kwa hiyo ni dhahiri kwa vitendo vinavyoendelea nchini ni kuwa Rais Magufuli hayuko tayari kukosolewa kwa ile tunayoiita "constructive criticism" kitendo ambacho anafanya kufuru kwa Mungu, kwa kuwa ni yeye pekee Mwenyezi Mungu ambaye amekuwa "exempted" kukosolewa, na sisi binadamu wote TUNASTAHILI kukosolewa ili tujirekebishe pale tulipokosea
Kwa Rais Magufuli kukataa kabisa kukosolewa ni kujitwalia nafasi ya Mungu ambapo kwa sisi binadamu tunaweza kuita kuwa anafanya KUFURU!
Mungu ibariki Tanzania