Rais Magufuli hakubali hata kidogo kupewa "constructive criticism"

Rais Magufuli hakubali hata kidogo kupewa "constructive criticism"

NDUGU MWANZISHA THREAD NIMEGUDUNDUA WEWE SI MZALENDO KABISA. wewe na wenzio kadhaa mna constructive criticism zipi? zipi hebu nitajie? nyie mnafaham zaidi kuliko rais? nyie mna elimu na uzoefu mkubwa kuliko rais wa jamhuri hii? rais ndiye mzalendo namba moja na yeye yupo kwa ajili ya sisi wanyonge. hivyo anachosema kipo sahihi. wewe ni nani hata ubishe? wewe ni nani hata ukosoe? rais hakosei kila analofanya rais ni amin na kweli. wewe una uwezo gan wa kumkosoa? hayo mambo acheni. rais is always right. na anatuwakilisha sisi wananchi maskini. anatupigania na unaona ametuletea hata ndege kubwa hapa nchini. ninyi mlikua mnakosa sasa walalahoi tunaiona ndege ambayo tulizoe kuiona kwenye video tu. sasa tunaiona live ikipita hewani. kama rais angewasikiliza wakosoaji tusingepata ndege. acheni rais apige kazi. hapa ni kazi tu.
I WAS RIGHT
 
Huyu ni bully na anachofanya ni bullying na character assassionation ambazo ni baadhi ya tabia za madikiteta.
Character Assassination ni Modus Oparandi ya Madikiteta Katili Wote Duniani! - JamiiForums

Ukiishamjua kuwa hii ndio hulka yake, you have two options, au ukubali ndivyo alivyo, uishi naye kwa uangalifu, au umurpuke kwa ku fall out na ku shut up. Wengi wameamua ku shut up, hata humu jf, kuna watu huwasikii sikii kama enzi za JK.

Kwa situation tuliomo, the best way ni
If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him! - JamiiForums
P
Nimekuelewa [emoji120] [emoji40] [emoji87]
 
Kuna hadithi tulizisoma tukiwa wadogo nyingine nilidhani zilikuwa kwa ajili ya kutuchekesha tu. Ajabu baada ya kuwa mkubwa nikizikumbuka hizo hadithi nyingine hazikuwa vichekesho hata kidogo. Kwa mfano hii hadithi ya mfalme aliyesifiwa amevaa suti nzuri hata ukweli ulipokuwa kwamba alikuwa uchi. Nilipokuwa nasoma hadithi hii nikiwa mdogo niliwashangaa sana wasifiaji na hata mfalme mwenyewe.
Baada ya kukua sikushangaa tena.
 
Mystery kinachoitwa constructive critism ni constructive criticism kwelii au ni destructive critism.Realistically what most of you call constructive cricism is actually destructive criticism to meet your selfish ends.Criticism will only meet the requirements of being constructive it focuses solely on addressing or solving problems of the majority,if not it will be ignored. The fifth phase government is not here for the minority,but for the majority,hili ni lazima lieleweke.
 
Tuvumilie maumivu tu; huyu ndivyo alivyo na ninaamini inatokana na malezi aliyopata huko nyuma. Muda wake utafika ataondoka!
Hivi unadhani mtu wa aina hii ni rahisi kivile kuondoka madarakani??

Hapa TZ tukae mkao wa kula wa "kuipindua" Katiba, kuhusu terms anazoruhusiwa mtu kuwepo Ikulu
 
wala sijakufuru. rais wetu hakosei. he is always right. na ndio maana hatuwezi kumshtaki hata akimaliza muda wake madarakani.

Ina maana wewe unapingana vikali na vitabu vya dini vya Biblia kwa wakristo na Koran kwa waislamu vinavyoeleza kuwa ni Mungu pekee ambaye yuko 100% perfect??

Kwa kumuita Rais Magufuli kuwa hakosei, wewe ndiye unafanya KUFURU!
 
Vitabu vyote vya dini vinasema kuwa sisi binadamu wote tuna mapungufu yetu na tunapaswa tunapokosolewa tujitafakari na kukukubali ushauri/ ukosoaji huo

Katika vitabu hivyo hivyo vya dini vinaandika kuwa ni Mungu pekee ambaye yupo 100% perfect

Kwenye nchi yoyote yenye utawala bora, ukosoaji wa serikali "constructive criticism" kutoka kwa wananchi wake kwa serikali yao ni jambo la kawaida sana na linapokekewa kwa nia ya kujirekebisha pale inapokosea

Lakini inashangaza sana kwa mtawala wetu, Rais Magufuli, kuwa hapendi kabisa kukosolewa kwa matendo anayofanya na mara nyingi anawatumbua wale wote wanaomkosoa

Niseme wazi kuwa Rais wetu kwa kutopenda kabisa kupewa "constructive criticism" anafanya kufuru kwa Mungu, kwa kuwa vitabu vyote vya dini vinasema kuwa hakuna binadamu yoyote tokea dunia iumbwe amewahi kuwa 100% perfect

Nitatoa mifano michache kulithibitisha hili ninalolisema:-

Ni hivi Jana tu Rais Magufuli amemtumbua Profesa Mark Mwandosya, uenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mwalimu Nyerere na nafasi yake kuchukuliwa na Stephen Wassira

Ingawa taarifa ya Ikulu haikutaja sababu za kutumbuliwa kwake, lakini hisia za wachambuzi wengi wa kisiasa, wanasema ni kutokana na Profesa Mwandosya kuwa ni mkosoaji mkubwa wa Rais Magufuli kupitia ukurasa wake wa Twitter

Ikumbukwe kuwa ni siku chache zilizopita, Profesa Mwandosya aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa walifundishwa misingi ya utawala bora kuwa Rais anapokusema hadharani kuwa umekosea, unalazimika siku inayofuata upeleke barua yako ya kujiuzulu nafasi hiyo

Ingawa hakumtaja kwa jina, lakini wadadisi wa mambo wamesema ujumbe huo wa Twitter ulikuwa ukimlenga moja kwa moja Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, ambaye siku chache zilizopita, Rais Magufuli aliingilia kati sakata hilo na kumwambia, Mkuu huyo wa Mkoa anapaswa kulipa kodi ya makontena hayo ya shilingi zipatazo bilioni 1.2 ambazo Mkuu huyo wa Mkoa alikuwa anataka kukwepa kulipa

Nimekuwa nikijiuliza hivi Profesa Mwandosya ni nini kosa lake, kuelezea suala "obvious" kama hilo la Mkuu wa nchi kumkosoa hadharani Mkuu wake wa Mkoa wa Dar na mkuu huyo wa Mkoa kuonyesha "kumdindia" Mkuu huyo wa nchi kwa kukataa kujiuzulu??

Suala lingine ambalo lilileta kizaazaa siku za nyuma ni kutumbuliwa kwa Waziri wa Habari wa wakati ule Nape Nnauye, kwa "kosa" la kuunda Tume iliyochunguza tukio la kuvamiwa kwa Clouds media usiku na askari wenye silaha za moto amacho kitendo hicho kilifanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Kitu kilichofuata ni kila mtanzania anakijua, ni kwa Waziri huyo wa Habari kutumbuliwa

Nimekuwa pia nikijiuliza hivi kosa la Nape Nnauye lilikuwa nini katika sakata lile la uvamizi wa Clouds media kulikofanywa na askari wenye silaha za moto??

Pengine ni kuunda ile Tume yake ya uchunguzi ambayo hata hivyo yeye asingekuwa ni mwamuzi badala yake hivyo vyombo ambavyo yeye angevikabidhi ndivyo vingeamua hatma ya Mkuu wa Mkoa wa Dar

Kwa hiyo ni dhahiri kwa vitendo vinavyoendelea nchini ni kuwa Rais Magufuli hayuko tayari kukosolewa kwa ile tunayoiita "constructive criticism" kitendo ambacho anafanya kufuru kwa Mungu, kwa kuwa ni yeye pekee Mwenyezi Mungu ambaye amekuwa "exempted" kukosolewa, na sisi binadamu wote TUNASTAHILI kukosolewa ili tujirekebishe pale tulipokosea

Kwa Rais Magufuli kukataa kabisa kukosolewa ni kujitwalia nafasi ya Mungu ambapo kwa sisi binadamu tunaweza kuita kuwa anafanya KUFURU!

Mungu ibariki Tanzania
Mkuu raisi hataki ushauri,lakini raisi ni yeye sio wewe.Sasa hizo pilipili usiokula zakuwasha nini?
Ushaambiwa na Mkapa kuwa uraisi hauna ubia,maamuzi ni ya raisi yawe mazuri au mabaya.
Pambana na hali yako,ndio Tanzania mpya.
 
Hivi unadhani mtu wa aina hii ni rahisi kivile kuondoka madarakani??

Hapa TZ tukae mkao wa kula wa "kuipindua" Katiba, kuhusu terms anazoruhusiwa mtu kuwepo Ikulu
wala sijakufuru. rais wetu hakosei. he is always right. na ndio maana hatuwezi kumshtaki hata akimaliza muda wake madarakani.
Ninasema Kwa mujibu wa vitabu vyetu vya dini vya Biblia kwa wakristo na Koran kwa waoslamu hiyo ni KUFURU!
 
wala sijakufuru. rais wetu hakosei. he is always right. na ndio maana hatuwezi kumshtaki hata akimaliza muda wake madarakani.
GuDume Mzee Msekwa alikosea sana kwa kudhani na pengine kwa mapenzi makubwa aliyokuwa nayo kwa Mwl alidhani angeishi milele yeye na kizazi hicho !! Hivyo alipendekeza katiba mbovu inayotumika na watu leo wenye ubinafsi wa kiwango cha kutisha .
Na JK kwa unafki wa kulinda maslahi yake, alivuruga mchakato uliotakiwa kuwakomboa wananchi kwenye minyororo ya wanasiasa sampuli hii!! Na wabunge tulio nao ndio hao wanaopiga meza huku wakiimba NDIOOOO kwa kila pendekezo kutoka serikalini. Huku wakisahau wao ni wawakilishi wa wananchi.

Ndiyo inayoleta umungumtu wa mtu yeyote atakayekaa magogoni.
 
Vitabu vyote vya dini vinasema kuwa sisi binadamu wote tuna mapungufu yetu na tunapaswa tunapokosolewa tujitafakari na kukukubali ushauri/ ukosoaji huo

Katika vitabu hivyo hivyo vya dini vinaandika kuwa ni Mungu pekee ambaye yupo 100% perfect

Kwenye nchi yoyote yenye utawala bora, ukosoaji wa serikali "constructive criticism" kutoka kwa wananchi wake kwa serikali yao ni jambo la kawaida sana na linapokekewa kwa nia ya kujirekebisha pale inapokosea

Lakini inashangaza sana kwa mtawala wetu, Rais Magufuli, kuwa hapendi kabisa kukosolewa kwa matendo anayofanya na mara nyingi anawatumbua wale wote wanaomkosoa

Niseme wazi kuwa Rais wetu kwa kutopenda kabisa kupewa "constructive criticism" anafanya kufuru kwa Mungu, kwa kuwa vitabu vyote vya dini vinasema kuwa hakuna binadamu yoyote tokea dunia iumbwe amewahi kuwa 100% perfect

Nitatoa mifano michache kulithibitisha hili ninalolisema:-

Ni hivi Jana tu Rais Magufuli amemtumbua Profesa Mark Mwandosya, uenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mwalimu Nyerere na nafasi yake kuchukuliwa na Stephen Wassira

Ingawa taarifa ya Ikulu haikutaja sababu za kutumbuliwa kwake, lakini hisia za wachambuzi wengi wa kisiasa, wanasema ni kutokana na Profesa Mwandosya kuwa ni mkosoaji mkubwa wa Rais Magufuli kupitia ukurasa wake wa Twitter

Ikumbukwe kuwa ni siku chache zilizopita, Profesa Mwandosya aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa walifundishwa misingi ya utawala bora kuwa Rais anapokusema hadharani kuwa umekosea, unalazimika siku inayofuata upeleke barua yako ya kujiuzulu nafasi hiyo

Ingawa hakumtaja kwa jina, lakini wadadisi wa mambo wamesema ujumbe huo wa Twitter ulikuwa ukimlenga moja kwa moja Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, ambaye siku chache zilizopita, Rais Magufuli aliingilia kati sakata hilo na kumwambia, Mkuu huyo wa Mkoa anapaswa kulipa kodi ya makontena hayo ya shilingi zipatazo bilioni 1.2 ambazo Mkuu huyo wa Mkoa alikuwa anataka kukwepa kulipa

Nimekuwa nikijiuliza hivi Profesa Mwandosya ni nini kosa lake, kuelezea suala "obvious" kama hilo la Mkuu wa nchi kumkosoa hadharani Mkuu wake wa Mkoa wa Dar na mkuu huyo wa Mkoa kuonyesha "kumdindia" Mkuu huyo wa nchi kwa kukataa kujiuzulu??

Suala lingine ambalo lilileta kizaazaa siku za nyuma ni kutumbuliwa kwa Waziri wa Habari wa wakati ule Nape Nnauye, kwa "kosa" la kuunda Tume iliyochunguza tukio la kuvamiwa kwa Clouds media usiku na askari wenye silaha za moto amacho kitendo hicho kilifanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Kitu kilichofuata ni kila mtanzania anakijua, ni kwa Waziri huyo wa Habari kutumbuliwa

Nimekuwa pia nikijiuliza hivi kosa la Nape Nnauye lilikuwa nini katika sakata lile la uvamizi wa Clouds media kulikofanywa na askari wenye silaha za moto??

Pengine ni kuunda ile Tume yake ya uchunguzi ambayo hata hivyo yeye asingekuwa ni mwamuzi badala yake hivyo vyombo ambavyo yeye angevikabidhi ndivyo vingeamua hatma ya Mkuu wa Mkoa wa Dar

Kwa hiyo ni dhahiri kwa vitendo vinavyoendelea nchini ni kuwa Rais Magufuli hayuko tayari kukosolewa kwa ile tunayoiita "constructive criticism" kitendo ambacho anafanya kufuru kwa Mungu, kwa kuwa ni yeye pekee Mwenyezi Mungu ambaye amekuwa "exempted" kukosolewa, na sisi binadamu wote TUNASTAHILI kukosolewa ili tujirekebishe pale tulipokosea

Kwa Rais Magufuli kukataa kabisa kukosolewa ni kujitwalia nafasi ya Mungu ambapo kwa sisi binadamu tunaweza kuita kuwa anafanya KUFURU!

Mungu ibariki Tanzania
Student's participating in democratic activities through sharing his opinions in school club
 
Kwahiyo yote anayoyafanya ni ya kwake binafsi? lakinu hata kama ni maamuzi yake ni sawa tu make bwana wetu Yesu Kristu alituachia roho mtakatifu atuongoze katika nafsi zetu na kwa maana hiyo hata mtu awe vipi, katika nafsi yake yuko roho mtakatifu wa kumuongoza katika mema yote. Na kwasababu mh. anafanya peke yake lakini yaliyo mema, tunamshuru roho mtakatifu kwa kumuongoza na kuzidi kumlinda dhidi ya washauri wengine (wahovu)
 
Tatizo la watanzania kila mtu anajua kila kitu. Utakuta muuza nazi anaongelea kuendesha ndege.

Unakuta kondakta anamkosoa kocha wa Taifa Stars. Unakuta mama ntilie anamkosoa mwanasheria.

Hizi elimu zetu za kuokotaokota kwenye google zinatudanganya sana.

Constructive criticism inaanza na maisha binafsi ya mtu. Jikosoe wewe kwanza ndipo uwe na haki ya kumnyooshea mtu kidole.
 
Yani ukiangalia huko chamani au sera zake tangu apate kukabidhiwa kijiti cha kuwa Rais ni tofauti sana na ilani ya chama au mienendo ya Marais waliomtangulia

Yaani hana tena makundi na kama yapo ni yapo ila urafiki wao ni wa mashaka yaani ni marafiki lakini hawaaminiani tofauti na huko nyuma ya awamu zilizopita.

Mpaka sasa hakuna anaemuamini mwenzake hadi kufikia kila mtu anamuhisi mwenzie sio chamani sio maofisini hadi imechangia ongezeko la watu kuongea peke yao huko njiani.

Yaani mpaka sasa anachokifanya ni kama hajapitia chamani maana sera kabadilisha/kabadilika kama hakupitia chamani vile.
 
Hivi JPM ni Msukuma, Muhaya, Msubi, Mzinza au Mnyamlenge?!?!

Samahani lakini

I gonna be back¡!
 
Back
Top Bottom