Rais Magufuli hahusiki kwa lolote mnalomsema baya

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,188
11,221
Aminini ama msiamini Mh Rais hayupo huko mnamtafakarisha. Mkuu wetu yupo bize na maswala ya maendeleo. Kiukweli kabisa kutokana na nidham ya kila taasisi basi kila mtu anawajibika sehem yake tofauti na pale zamani taasisi za umma zilijifanyia mambo hovyohovyo this tm kila mtu anafanya kazi kwa mujibu wa sheria hakuna huruma.

Nini tofauti ya serikali hii na ile iliopita. Serikali iliopita ilikuwa mtu akiadhibiwa na taasisi nyingine alikuwa na uwezo kulalamika ikulu na akapata kaupendekeo au huruma ya juu. This time mkuu tulie nae anataka watu wawajibike kwa yale wanayatenda pasipo kuangalia makunyanzi.
Kiufupi mbele ya serikali hii makosa ni dhambi kubwa na hakuna msamaha. Angalie wale waliokamatwa na dawa za kulevya serikali imeacha washughulikiwe no huruma why wote mwaelewa.

Unajuwa kweli kabisa kunasiku tutajiona wapumbavu maana tunashindwa mtumia huyu rais vizuri. Nataka kuwambia tukiachana na siasa huyu rais is the best of all time. .
 
Mnyeti, Bashite, Kigwangala ( ametangaza hadharani kuua, na leo kuna kada wa CCM anamkumbusha kuwa alikosea hilo agizo angelitolea kwenye vikao vya siri)
 
Wewe nawe acha uongo, mwanzoni mlisema wanaolalamika ni mafisadi na wapiga dili. Sasa imeingia awamu ya viongozi wa dini kulalamika, alianza Kakobe kwa kumwambia atubu, wamefuata baraza la maaskofu na ujumbe wa kwaresma kwamba hali iliyopo nchini hivi sasa inaogopesha, watu wanapotea, wengine wanaokotwa kwenye viroba kando ya fukwe, risasi zinaua mwanafinzi, wasiojulikana wanaua viongozi kwa mapanga, biashara zinakufa, watu wanapoteza ajira, wakati huo huo serikali haijiri, ubaguzi wa kikanda, ubaguzi wa kutopeleka maendeleo sehemu ambazo chama tawala hakikushinda na mengine yanyofanana na hayo. Hakika huyu sio best wa wakati wote kama unavyotaka kutuaminisha.
 
Mkuu pamoja na yoote hapo juu kumhusu rais moja kwa moja, hili la kuongoza taifa lenye wasio julikana ni tatizo kubwa sana.
 
Serikali ya CCM kupitia Waziri Kigwangala imetoa tamko na kusisitiza raiya wa kigeni wauliwe mara moja iwezekanavyo.
 
Wewe nawe acha uongo, mwanzoni mlisema wanaolalamika ni mafisadi na wapiga dili. Sasa imeingia awamu ya viongozi wa dini kulalamika, alianza Kakobe kwa kumwambia atubu, wamefuata baraza la maaskofu na ujumbe wa kwaresma kwamba hali iliyopo nchini hivi sasa inaogopesha, watu wanapotea, wengine wanaokotwa kwenye viroba kando ya fukwe, risasi zinaua mwanafinzi, wasiojulikana wanaua viongozi kwa mapanga, biashara zinakufa, watu wanapoteza ajira, wakati huo huo serikali haijiri, ubaguzi wa kikanda, ubaguzi wa kutopeleka maendeleo sehemu ambazo chama tawala hakikushinda na mengine yanyofanana na hayo. Hakika huyu sio best wa wakati wote kama unavyotaka kutuaminisha.
Wala siyo best Wa muda mfupi pia, ni worst Wa muda wote.
 
Ni vizuri viongozi tunaowachagua na wawakilishi wao wawe viongozi na wawaachie watendaji kazi zao.
Wasitoe maelekezo yanayovunja sheria.
Ni lazima pawe na kiongozi ambaye ni kimbilio la wale wanaoonewa na matamko ya watawala.

Kwa sasa kuna maeneo uonevu umeanza kuonekana dhahiri na hakuna kimbilio kwa wale wanaoonewa kwa kisingizio cha kuchapa kazi na kusingizia kuwa anayetendewa uonevu ni mpiga dili.

Tutaanza kurudi kwenye unyanyasaji wa kijinsiasa ,kikabila na kidini kama hatutataka kufuata taratibu za kisheria na hatua za kisheria zichukuliwe bila kumnyanyasa mtu.

Mahakama zipo lakini wakati mwingine haki inapatikana kwa gaharama kubwa.
Kumbe haki hiyo ilikua inaweza kutolewa na mkuu wa mkoa au waziri au mkuu wa nchi bila kumbagua mtu.
Tatizo ni hulka ya ubaguzi wa kivyama na kikanda inayoanza kujitokeza. Yani akitendewa dhulma wa chama X hana pa kukimbilia.Wakurugenzi ,wakuu wa wilaya ,wakuu wa mikoa, mawaziri na hata wajuu zaidi hawaraki kabisa kumsikila mtu wa itikadi tofauti na ya kwao. Wameshindwa kutofautisha majukumu ya chama na mipaka ya chama na ya serikali. Serikali ni ya watu wote lakini chama ni cha wanachama ndio maana hakitoe kadi kwa kila mtu au kumruhusu kila mtu kugombea uongozi lakini serikali ina wenye vyama na wasio na vyama.

Serikali iliyopita ilileta maendeleo makubwa na unafuu mkubwa wa maisha kwa kutoa ajira nyingi kwa kila mtanzania huku wabunge wakiwa na mahela mengi ya kuzungukia majimbo na vikao bwerere na safari nyingi kwa viongozi na kuongeza mzunguko wa fedha nchini huku fursa za kutajirika zikiwa kwa mtu yeyeyote bila kujali kabila ,chama ,dini na kanda.
Watendaji wa serikali wa awamu ya nne walijua kula na vipofu ,kwa kuwa waliwaacha watu wachini nao waokote vile vinavyodondoka mezani.Walijitahidi kulinda haki za mtu mmoja mmoja kwa kufuata katiba na taratibu.

Awamu ya nne ilikosea kwenye usimamizi wa nidhamu ya utumishi tu. Mambo mengine awamu hiyo ilifanya vizuri sana.
 
TumainiEI,
Umebandika andiko ambalo kiukweli halina mashiko na huwezi kutetea(defend) hili andiko dhaifu...!!!
Kama wewe kweli ni Mtanzania Halisi,Mzalendo na Mwanademokrasia basi huwezi kutetea huo ujinga.
Tangu aingie madarakani huyu mtu unayesema,'' ni rais the best of all times'' kila mtu, kila kona kila saa na kila siku watu wanalalamika namna ana vyoipeleka nchi.....!!!

Sijui umetumia vigezo gani kuhitimisha kuwa Magufuli is the best President of all times....!!!Kwa taarifa yako THE BEST PRESIDENT OF ALL TIMES KWA TANZANIA NI BABA WA TAIFA MWALIMU J.K. NYERERE(rip). Fanya a simple comparison between the 2 yaani Nyerere viz-a-viz Magufuli halafu ndiyo uanze kuropokwa....!!!

Rais anayeshindwa kulinda misingi ya UMOJA WA KITAIFA, UDUGU NA MSHIKAMANO iliyoasisiwa na Baba wa Taifa huwezi kumwita ni best...!!!Rais anayeanza kuua na kukandamiza Wapinzani, kuvunja Katiba na Sheria kwa kisingizio cha Kujenga viwanda hawezi kupewa credit ya kuwa best....!!Unless uniambie unampgia debe ili upewe Ukurugenzi, u-RC au u-DC!!!!!!!!!!
 
Aminini ama msiamini Mh Rais hayupo huko mnamtafakarisha. Mkuu wetu yupo bize na maswala ya maendeleo. Kiukweli kabisa kutokana na nidham ya kila taasisi basi kila mtu anawajibika sehem yake tofauti na pale zamani taasisi za umma zilijifanyia mambo hovyohovyo this tm kila mtu anafanya kazi kwa mujibu wa sheria hakuna huruma.

Nini tofauti ya serikali hii na ile iliopita. Serikali iliopita ilikuwa mtu akiadhibiwa na taasisi nyingine alikuwa na uwezo kulalamika ikulu na akapata kaupendekeo au huruma ya juu. This time mkuu tulie nae anataka watu wawajibike kwa yale wanayatenda pasipo kuangalia makunyanzi.
Kiufupi mbele ya serikali hii makosa ni dhambi kubwa na hakuna msamaha. Angalie wale waliokamatwa na dawa za kulevya serikali imeacha washughulikiwe no huruma why wote mwaelewa.

Unajuwa kweli kabisa kunasiku tutajiona wapumbavu maana tunashindwa mtumia huyu rais vizuri. Nataka kuwambia tukiachana na siasa huyu rais is the best of all time. .

Mbona mpaka sasa hakuna fisadi aliechukuliwa hatua? Lowassa, Chenge, Tibaijuka wote wako mtaani mpaka sasa.
 
Wewe nawe acha uongo, mwanzoni mlisema wanaolalamika ni mafisadi na wapiga dili. Sasa imeingia awamu ya viongozi wa dini kulalamika, alianza Kakobe kwa kumwambia atubu, wamefuata baraza la maaskofu na ujumbe wa kwaresma kwamba hali iliyopo nchini hivi sasa inaogopesha, watu wanapotea, wengine wanaokotwa kwenye viroba kando ya fukwe, risasi zinaua mwanafinzi, wasiojulikana wanaua viongozi kwa mapanga, biashara zinakufa, watu wanapoteza ajira, wakati huo huo serikali haijiri, ubaguzi wa kikanda, ubaguzi wa kutopeleka maendeleo sehemu ambazo chama tawala hakikushinda na mengine yanyofanana na hayo. Hakika huyu sio best wa wakati wote kama unavyotaka kutuaminisha.
umesahau kumalizia na US PAMOJA NA EU ..sasa cjui wtasema kuwa na Hawa wanawivu
 
Hawa jamaa wanaendesha kampeni mbaya sana dhidi ya Mheshimiwa Rais Magufuli kwa kutumia lugha ya demokrasia. Huyu ndio kiongozi pekee mwenye maamuzi bila kujali chama cha siasa katika vita dhidi ya ufisadi. Wanasiasa wengi wa nchi hii wapo kwa ajili ya maslahi yao wala sio za wananchi. Hizi hujuma wanazozielekeza dhidi ya Mheshimiwa Rais Magufuli zitaleta maafa kwa watanzania. Ningeshauri watanzania wamuunge mkono Kiongozi huyu kwa dhati.
 
Back
Top Bottom