Utawala wa Rais Samia unarudi kwa kasi kwenye udikteta

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,559
41,077
Wakati awamu ya 5, ambayo Rais Samia alikuwa makamu wa Rais, ilidhihirika wazi kuwa utawala huo ulikosa uvumilivu wa kisiasa, na hivyo kuegemea kwenye nguvu za dola katika kuwaonea watu wanaohoji na kukosoa.

Katika utawala huo, wakosoaji wa Serikali ama walitekwa, kupotezwa, kushambuliwa kwa risasi na wengine kubambikiwa kesi za uhujumu uchumi, na kisha kuwekwa magerezani ambapo ili kutoka walilazimishwa kuununua uhuru wao. Hata hiyo pesa ambayo watu waliitoa kuununua uhuru wao, haijulikani mpaka leo ilipelekwa wapi.

Mara baada ya kifo cha Rais Hayati Magufuli, Samia kwa mujibu wa Katiba aliapishwa kuwa Rais. Baada ya kuapishwa, mwanzoni kabisa alianza kufanya mambo kadhaa ili kuwaonesha watu kuwa yeye ni kiongozi aliyezingatia demokrasia, uhuru wa watu na haki za raia.

Hata hivyo, matendo yake yalionesha unafuu tu lakini hayakudhihirisha kuwa yeye kweli ni kiongozi anayezingatia misingi ya demokrasia na utawala wa sheria. Rangi yake halisi ilionekana pale alipoanza kukosolewa.

CHADEMA waliposimama kuanza kudai Katiba mpya na mabadiliko ya sheria gandamizi, Rais Samia akasema kuwa hayo yote yasubiri, yeye anajenga uchumi. Freeman Mbowe akajibu kuwa hawatasubiria kuidai katiba mpya, Samia akatamka wazi kuwa mtu akimparura na yeye atamparura, akaamuru Mbowe kukamatwa na kisha akambambikia kesi ya ugaidi.

Mbinyo wa mataifa ya Ulaya ndio uliomlazimisha Samia kumfutia Mbowe kesi ya kumbambikia. Samia ili asiaibike, alitafuta kila njia aonekane ni kiongozi mwenye huruma, akapandikiza watu wajifanye wanamwombea msamaha Mbowe, baada ya Mbowe kukataa waziwazi kuwa hawezi kuomba msamaha wakati hana kosa.

Rais Samia, baadaye ili kuzidi kujionesha kuwa ana utofauti na mtangulizi wake, aliwafutia kesi za kubambikiza watu wengi, na wengine hata kuwarudishia pesa zao walizolipa kupitia uporaji ulioitwa plea burgain.

Lakini sasa, rangi halisi za Rais Samia na utawala wake zinaanza kuonekana dhahiri. Anaenda kwa kasi kwenye siasa zilezile za awamu ya 5, na hata kuzidi, ambayo yeye alikuwa makamu wa Rais. Wale wanaomkosoa kuhusiana na uporwaji wa bandari za Tanganyika na kisha kuwagawia waarabu, wameanza kubambikiwa kesi mbalimbali. Wakili Madeleka aliyekuwa amebambikiwa kesi za uhujumu uchumi wakati wa awamu ya 5, na kisha kuingia kwenye plea burgain kuununua uhuru wake amekamatwa na kurudishiwa kesi ya uhujumu uchumi. Na hili limetokea baada ya wakili huyu kutoa ufafanuzi wa vifungu vya hovyo vya mkataba ulioruhusu uporwaji wa bandari za Tanganyika. Wakili Mwambukusi na Dr. Rugemeleza, wote waliokosoa mkataba wa uporwaji wa bandari za Tanganyika, nao wamefunguliwa majalada polisi. Lengo inaonekana ni kuwatisha wao binafsi na wengine wote wanaopaza sauti kuzuia wizi wa mali za asili za Tanganyika.

Samia anaonekana wazi hana uvumilivu wa kisiasa, hana uanademokrasia wowote, wala hana lengo lolote la kuifanya nchi hii iwe na utawala unaozingatia haki na sheria. Mbaya zaidi, inaonekana ana dhamira inayotia mashaka sana juu ya Tanganyika. Wala hana lengo lolote la kuifanya nchi iwe na katiba nzuri mpya. Kilichodhahiri, bila shaka anafanya mambo fulani mazuri kwa nia tu ya kuwapumbaza wananchi na jamii ya kimataifa ili dhamira yake iliyojificha aweze kuikamilisha bila ya kupingwa.

Kauli tata alizowahi kuzitamka Rais Samia, ni pamoja na:

1) akizungumzia tukio la Lisu kushambuliwa kwa risasi alisema.kuwa Lisu hakushambuliwa na askari maana askari wa Tanzania wakimlenga mtu kumpiga risasi, hawawezi kumkosa. Hapa inaonesha kuwa polisi huwa wanaua raia, na Rais Samia anaona ni sahihi.

2) Wananchi hata mkiwachagua hao wapinzani, mnapoteza kura zenu kwa sababu kura hizo zitahesabiwa CCM. Kwa kauli hii alionesha wazi kuwa anafahamu kuwa upigaji kura Tanzania hauna maana, ni kiinimacho. CCM huwa wanapora kura zisizo zao, na yeye anaona ni sahihi.

Na juzi ameyaweka maandamano ya wananchi kwenye kundi moja na ugaidi. Kwake maandamano ambayo yameruhusiwa na katiba kama njia za wananchi kupaza sauti zao dhidi ya watawala pale taasisi nyingine kama vile Bunge na mahakama zinapokuwa zimeshindwa kusimamia maslahi ya umma, Rais anaona njia hiyo ya maandamano ni sawa na ugaidi. Ina maana anapingana na katiba aliyoapa kuilinda. Kauli ile itatafsiriwa na polisi kama agizo la Rais dhidi ya yeyote atakayeandamana kupinga chochote.

Wananchi tusibweteke tukadhani eti tuna utawala unaozingatia haki. Ukweli tupo kwenye lindi la utumwa wa watawala, na huu wa sasa huenda utakuwa mbaya zaidi kuliko wote, kwa maana nchi inauzwa, na anayenyanyuka anadidimizwa na kugandamizwa ili uuzwaji wa mali za asili za Tanganyika usikutane na upinzani wowote wa sauti za wananchi. Tupambanie uhuru wetu, tupambanie haki yetu, tupambanie Taifa letu linalozidi kudumazwa na watawala.
 
Maji yameshazidi unga, mwanzo alitumia gender yake ili kupata uungwaji mkono, akadhani watanganyika tutadanganyika kwa jinsia yake, akachagua kuruhusu mikutano ya siasa ili azidi kujitafutia uungwaji mkono.

Hili la mkataba wa hovyo wa bandari ndio limekuja kuzionesha rangi zake halisi, japo alituonjesha kidogo alivyombambikia Mbowe kesi ya ugaidi, sasa kwa huu mkataba wa hovyo, ndio ameamua kuzitoa rangi zake zote halisi ili tumfahamu.

Kwa hali ya mambo inavyoelekea, ni suala la muda tu kama unavyosema, atageuka kuwa dikteta kamili hasa akishajua wale anaowaongoza, hawana tena imani nae, na hana jinsi ya kuirudisha, hivyo anaweza kuamua kama ubaya uwe ubaya tu.
 
Wakati awamu ya 5, ambayo Rais Samia alikuwa makamu wa Rais, ilidhihirika wazi kuwa utawala huo ulikosa uvumilivu wa kisiasa, na hivyo kuegemea kwenye nguvu za dola katika kuwaonea watu wanaohoji na kukosoa.

Katika utawala huo, wakosoaji wa Serikali ama walitekwa, kupotezwa, kushambuliwa kwa risasi na wengine kubambikiwa kesi za uhujumu uchumi, na kisha kuwekwa magerezani ambapo ili kutoka walilazimishwa kuununua uhuru wao. Hata hiyo pesa ambayo watu waliitoa kuununua uhuru wao, haijulikani mpaka leo ilipelekwa wapi.

Mara baada ya kifo cha Rais Hayati Magufuli, Samia kwa mujibu wa katiba aliapishwa kuwa Rais. Baada ya kuapishwa, mwanzoni kabisa alianza kufanya mambo kadhaa ili kuwaonesha watu kuwa yeye ni kiongozi aliyezingatia demokrasia, uhuru wa watu na haki za raia.

Hata hivyo, matendo yake yalionesha unafuu tu lakini hayakudhihirisha kuwa yeye kweli ni kiongozi anayezingatia misingi ya demokrasia na utawala wa sheria. Rangi yake halisi ilionekana pale alipoanza kukosolewa.

CHADEMA waliposimama kuanza kudai katiba mpya na mabadiliko ya sheria gandamizi, Rais Samia akasema kuwa hayo yote yasubiri, yeye anajenga uchumi. Freeman Mbowe akajibu kuwa hawatasubiria kuidai katiba mpya, Samia akatamka wazi kuwa mtu akimparura na yeye atamparura, akaamuru Mbowe kukamatwa na kisha akambambikia kesi ya ugaidi.

Mbinyo wa mataifa ya Ulaya ndio uliomlazimisha Samia kumfutia Mbowe kesi ya kumbambikia. Samia ili asiaibike, alitafuta kila njia aonekane ni kiongozi mwenye huruma, akapandikiza watu wajifanye wanamwombea msamaha Mbowe, baada ya Mbowe kukataa waziwazi kuwa hawezi kuomba msamaha wakati hana kosa.

Rais Samia, baadaye ili kuzidi kujionesha kuwa ana utofauti na mtangulizi wake, aliwafutia kesi za kubambikiza watu wengi, na wengine hata kuwarudishia pesa zao walizolipa kupitia uporaji ulioitwa plea burgain.

Lakini sasa, rangi halisi za Rais Samia na utawala wake zinaanza kuonekana dhahiri. Anaenda kwa kasi kwenye siasa zilezile za awamu ya 5, na hata kuzidi, ambayo yeye alikuwa makamu wa Rais. Wale wanaomkosoa kuhusiana na uporwaji wa bandari za Tanganyika na kisha kuwagawia waarabu, wameanza kubambikiwa kesi mbalimbali. Wakili Madeleka aliyekuwa amebambikiwa kesi za uhujumu uchumi wakati wa awamu ya 5, na kisha kuingia kwenye plea burgain kuununua uhuru wake amekamatwa na kurudishiwa kesi ya uhujumu uchumi. Na hili limetokea baada ya wakili huyu kutoa ufafanuzi wa vifungu vya hovyo vya mkataba ulioruhusu uporwaji wa bandari za Tanganyika. Wakili Mwambukusi na Dr. Rugemeleza, wote waliokosoa mkataba wa uporwaji wa bandari za Tanganyika, nao wamefunguliwa majalada polisi. Lengo inaonekana ni kuwatisha wao binafsi na wengine wote wanaopaza sauti kuzuia wizi wa mali za asili za Tanganyika.

Samia anaonekana wazi hana uvumilivu wa kisiasa, hana uanademokrasia wowote, wala hana lengo lolote la kuifanya nchi hii iwe na utawala unaozingatia haki na sheria. Mbaya zaidi, inaonekana ana dhamira inayotia mashaka sana juu ya Tanganyika. Wala hana lengo lolote la kuifanya nchi iwe na katiba nzuri mpya. Kilichodhahiri, bila shaka anafanya mambo fulani mazuri kwa nia tu ya kuwapumbaza wananchi na jamii ya kimataifa ili dhamira yake iliyojificha aweze kuikamilisha bila ya kupingwa.

Kauli tata alizowahi kuzitamka Rais Samia, ni pamoja na:

1) akizungumzia tukio la Lisu kushambuliwa kwa risasi alisema.kuwa Lisu hakushambuliwa na askari maana askari wa Tanzania wakimlenga mtu kumpiga risasi, hawawezi kumkosa. Hapa inaonesha kuwa polisi huwa wanaua raia, na Rais Samia anaona ni sahihi.

2) Wananchi hata mkiwachagua hao wapinzani, mnapoteza kura zenu kwa sababu kura hizo zitahesabiwa CCM. Kwa kauli hii alionesha wazi kuwa anafahamu kuwa upigaji kura Tanzania hauna maana, ni kiinimacho. CCM huwa wanapora kura zisizo zao, na yeye anaona ni sahihi.

Na juzi ameyaweka maandamano ya wananchi kwenye kundi moja na ugaidi. Kwake maandamano ambayo yameruhusiwa na katiba kama njia za wananchi kupaza sauti zao dhidi ya watawala pale taasisi nyingine kama vile Bunge na mahakama zinapokuwa zimeshindwa kusimamia maslahi ya umma, Rais anaona njia hiyo ya maandamano ni sawa na ugaidi. Ina maana anapingana na katiba aliyoapa kuilinda. Kauli ile itatafsiriwa na polisi kama agizo la Rais dhidi ya yeyote atakayeandamana kupinga chochote.

Wananchi tusibweteke tukadhani eti tuna utawala unaozingatia haki. Ukweli tupo kwenye lindi la utumwa wa watawala, na huu wa sasa huenda utakuwa mbaya zaidi kuliko wote, kwa maana nchi inauzwa, na anayenyanyuka anadidimizwa na kugandamizwa ili uuzwaji wa mali za asili za Tanganyika usikutane na upinzani wowote wa sauti za wananchi. Tupambanie uhuru wetu, tupambanie haki yetu, tupambanie Taifa letu linalozidi kudumazwa na watawala.
Kama ukisoma kitabu kitakatifu cha Bibilia utakutana na Delila.

Msome Delila vizuri utaelewa awamu ya sita vizuri na yaliyompata mwendazake.
 
Ikiwa hivyo mama atakuwa anafanya jambo la maana sana.

Kila kitu lazima kiwe na mipaka.

Watu wasitumie vibaya neno "demokrasia".

Si awamu ya tano tu. Toka tupate Uhuru kila awamu ilikuja na namna zake za kudhibiti ujinga.

Nyerere ndiyo alifika mbali zaidi, mpaka akapiga marufuku mambo ya vyama vingi, akasema kama mnataka siasa ipo TANU mkalumbane humo kisiasa.

Tena naona mama Samia anawawachia sana wajinga wajinga.
 
Usipotoshe, mipaka lazima iwekwe kisheria, sio kutazama mawazo ya mtu asiyependa kufuata sheria, wala kusikiliza ushauri wa anaowaongoza, ndio aweke hiyo mipaka, Samia ni dikteta.
 
Back
Top Bottom