Mheshimiwa Rais kwanza pole na misukosuko ya kampeni za uchaguzi ambapo unajiwinda kurudi tena. Ila mambo sio mepesi, hata kama utashinda ila utakuwa umejifunza la sivyo utakiacha chama chako tabuni sana kipindi ukiondoka. Mungu akuepushe na mipango ovu ya wapambe wako wanaotaka ubaki madarakani, jambo hili hata mimi linanipa hofu kubwa ila mungu akupe hekima na busara ukimaliza muda wako upumzike.
1. Mheshimiwa Rais JPM. Akingalia hali hii ya kampeni zako zimekuwa ngumu sana hasa kwa wasaka tonge kukudanganya juu ya mipango yao ya kujidai wanatokomeza upinzani kwa kununia madiwani na Wabunge, hapa walisahau kitu diwani anachaguliwa na raia je kuna jipya jema ambalo umemtendea raia. Ukirudi acha kuongea kwa kudharau watanzania, punguza chuki na wapinzania.
2. Endapo utarudi, japo najua utarudi tengeneza taifa la wapendwa, acha kutengeneza mipaka ya maendeleo leta kongamano la upendo wa kitaifa uje uhudumu kama baba mzazi. Jukwaani ongea ukifundisha upendo na mshikamano. La sivyo ukiendelea na tabia yako ya dharau utaiacha CCM katika hali mbaya.
3. Ukirudi tena rudisha pesa kwa kwa Wananchi na endesha nchi kwa uwazi sana. Japo napatwa na hofu kuu hasa juu ya wewe kuachia madaraka maana ulisjasema hii miradi mikubwa uliyoanzisha ukiondoka unadhani itaishia hewani na kuna kila dalili mpaka unaondoka hakuna mradi hata mmoja ambao utakuwa umekamilika kwa asilimia 100. Ukidanganywa ucheze na katiba utakuwa umekosea sana mizimu yetu na wazee wetu. Fanya kwa kiasi chako muda ukimalizika ondoka. Ila nakushauri ubaki kuwa mwenyekiti wa CCM ili uweze kumuendesha mgombea uraisi wenu.
4. Naamini kabisa 2023 kuna watu watakuibukia ndani ya chama chako na uenda ukavaa upinzani mkubwa sana maana utakuwa na mwaka mmoja tu wa kuwa raisi. Hivyo nakuomba ubadilishe aina ya mfumo wa kuendesha nchi. Kinachoendelea ni chuki za wazi juu ya mfumo wako wa kuendesha nchi, hii nchi inahitaji kuungwa upya kutokana na mfumo wa uongozi uliofanya.
5. Muite Lissu unywe nae chai...hapa utaishangaza dunia. Lisu analia Lisu kaumizwa najua fika wewe haukuhusika lakini kumbuka mtoto wa jirani kaumia ndani ya nyumba yako. Na wewe baba mwenye nyumba umekaa kimya ebu onyesha kukemea lakini matokeo yake. Wajomba na baba wadogo wanazidi kutoa maneno ya hovyo kwa majeruhi yaliyompata mtoto wa jirani.
Ukirudi mfukuze Polepole na genge lake hawa hawana jema na wewe.
Nakutakia kampeni njema na ushindi mnono.